MANENO YANA NGUVU.
Naanza kwa kuandika kuwa ; “Nayajua mengi kwa kuwa nimempa kila mtu nafasi ya kuwa mwalimu wangu, kila mtu hunifunza kwa yale atakayo. Huwa naheshimu kauli na mawazo ya wote kwa uzito sawa, LAKINI UELEWA NI JUU YANGU” Jua ya kwamba; “Ulemavu wa fikra tulizonazo juu ya maisha na juu yetu wenyewe huzaa mawazo mpauko yasiyoakisi umuhimu na umaana wa utu wetu na malengo yetu. Kuna muda tunafikiri kuwa watu wa aina fulani ndio wawezao kufanya mambo ya maana na yenye maendeleo kwa wao wenyewe, na sisi kujiweka nyuma kwa miakisio ya ubovu wa uteuzi wa fikra sahihi dhidi ya fikra mtambuka. Tunawaza zaidi kuliko kufikiri juu ya hatima ya uzio wa upeo wetu na malengo yetu. Akili zetu hutuongoza katika mwambao wa kukata tamaa na kutojikubali. Tunahangaikia kuona kuliko kutazama na kuyafanya ya mwisho kuwa ya kwanzo. Sisi ni zao la umakini hafifu wenye kichefuc