Posts

Showing posts from April 26, 2016

KWA WANAWAKE WOTE WALIO KATIKA NDOA

Image
MAFUNDISHO KUTOKA KATIKA KITABU CHA ‘ MITHALI 31:11-31’ KWA WANAWAKE WOTE WALIO KATIKA NDOA Tabia ya mwanada hujengwa au huathiriwa na mambo mawili; mosi ni nitabia aliyorithi kutoka wazazi (yaani Nature) 2.  Ni tabia aliyoipata kutokana na mazingira aliyokulia na kuishi kwayo (yaani Nuture). Tabia ya kurithi kutoka kwa wazazi yaweza athiriwa na  kubadirika kwa sababu ya mazingira anayoishi na kukuli, pamoja na jamii inayomzunguka. Hivyo basi, andiko hili linasehemu na mchango wa kuibadirisha jamii ya kinamama walio katika ndoa zao aidha, kwa muda mrefu au mfupi, na wale wanaotarajia kuingia katika tasisi hiyo ya wanandoa.  Kwa hiyo, wanawake walio katika ndoa kunamambo ya kujifunza mengi yenye kujenga ndani ya kitabu cha tano cha Mithali za Mfalme Sulemani. Ni nukuu ya maneno ya Mfalme Lemueli; Muasia kama alivyofundishwa na mama yake ambayo Sulemani aliyaandika katika kitabu cha Mithali. Mafundisho hayo ni ya msingi kwa kiasi kikubwa kwa mwanamke aliye katika...