GONJWA LA LEO LINALOENEA KWA KASI KWA WATU WENGI
Utangulizi Pamekuwepo na panazidi kuongezeka magonjwa mengi ya ajabubuajabu katika ulimwengu wa sasa tunaouishi katika dhama za mwisho wadunia; hususani ndani ya sayari yetu Dunia. Magonjwa hayo yamekuwa kikwazo na kusababishwa changamoto nyingi sana katika maisha ya mwanadamu. Ukiachana na magonjwa ya kisaikolojia, kiakili, kimwili na mengineyo mengi sana yanayozidi kubainika na kuongezeka siku hadi siku katika kizazi cha ulimwengu wa sasa; lipo gojwa la muda mrefu, ambalolimedumu karine kwa karine. Gonjwa hilo sugu ni kongwe kuliko magonjwa mengine baadhi yaliyoibuka hivi karibuni. Gonjwa hili limekuwa likienea kwa kasi ya ajabu kulingana kubadirika kwa mitindo ya maisha ya mwanadamu. Gonjwa hili linajibainisha katika na hari na dalili zifuatazo: Kupenda raha na maisha ya bila kutoa jasho, Kupenda kulala kuliko kujibidisha, Kukosa moyo wa kujituma, Kupenda starehe ku...