Nyerere Archive
Azimio la Arusha ni tamko rasmi la kisiasa lilikosudiwa kuongoza Tanzania katika njia ya ujamaa kadiri ya maelekezo hasa ya Julius Kambarage Nyerere . Jina la azimio linatokana na mji wa Arusha lilipitishwa tarehe 26-29 Januari 1967 .Tarehe 5 Februari 1967 Mwalimu Nyerere alilitangaza huko Dar es Salaam kama uamuzi wa Watanzania wa kuondoa unyonge wao. Tamko la Arusha lina sehemu tano: Itikadi ya chama cha TANU ; Siasa ya ujamaa; Siasa ya kujitegemea ; Uanachama wa TANU; na Azimio la Arusha. Kiini chake ni hiki: "Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliotufanya tuonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi , mapinduzi ya kuondoa unyonge ili tusionewe tena, tusinyonywe tena na tusipuuzwe tena". 5 February 1967 The Arusha Declaration Written: for Tanganyika African National Union by Julius Nyerere, 1967; Transcribed by: Ayanda