Posts
Showing posts from February 14, 2020
SOMO: UASI WA KANUNI YA KIROHO TUSIOUJUA:
- Get link
- X
- Other Apps
FUNGU: WAEFESO 5:15-21 “ 15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati kwa maana zama hizi ni za uovu. 17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya bwana. 18 Tena msilewe Kwa mvinyo, ambamo mnaufisadi; Bali mjazwe Roho; 19 mkisemezana Kwa zaburi Na tenzi na nyimo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana Yesu Kristo; 21 hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo. 1.0 UTANGULIZI: 1.1. Katika maisha yangu ya kiroho; Nahau zifuatazo zimenifunda: 1) Kama hujui mahala unapoelekea uwapo safarini, njia yoyote miongoni mwa nyingi itakuchagulia uelekeo na Kama hujishughulishi kujua unakoelekea, njia haiwezi kukuchagulia uelekeo sahihi uutakao. 2) Eneo lenye giza zaidi kuliko maeneo yote katika mshumaa lipo chini ya mshumaa. 3) Debe lililo tupu ...
CHANGAMOTO KATIKA TASISI
- Get link
- X
- Other Apps
FUNGU: Mwanzo 16:6; Naye Abram akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake. 1.0 UTANGULIZI: Nawasalimu katika jina la Bwana wetu Kristo; Bwana Yesu Asifiwe binti na wana za Mungu. kwan Somo la leo linatoka katika kitabu cha Mwanzo 16:1-15 , na Mwanzo 21:1-21 . Mada itajikita katika tasisi iitwayo familia. Swali: Kwa nini familia iitwe tasisi? Tusome kwanza Mwanzo 16:1-15 , na Mwanzo 21:1-21 kisha tuanze somo. 2.0. KIINI CHA SOMO: Aya zote tulizosoma zinamhusu familia ya Abram ambaye ni Ibrahimu pamoja na mkewe Sarai ambaye ni Sara. Familia ya Ibrahimu na Sarai ilikuwa na mjakazi (mfanyakazi au dada wa kazi) aitwaye Hajiri mwenye asili ya Misiri. Familia hii ya Abram na Sarai haikuwa na mtoto, toka wameoana. Kadri miaka iliposonga, Serai akamshauri Abram mumewe azae na kijakazi aitwaye Hajiri (Mwanzo 16:2-4). Hajiri alijifungua mtoto wa kiume aliyeitwa Ishim...
TAMTHILIYA YA KWELI
- Get link
- X
- Other Apps
FungU: Ayubu 42:10 “Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Auyubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza”. 01: UTANGULIZI Hapa duniani zipo tamthiliya lukuki zilizoandaliwa na wanadamu kwa njia za maigizo katika majukwaa ya sanaa; maandishi katika vitabu, majarida na magazeti; sauti katia redio na katika sinema. Tamthilia hizo kwa sehemu kubwa zina sifa za kufanana kimuundo wake na zinatofautiana kimtindo (yaani namna ilivyowasilishwa tamthiliya hiyo). Muundo wa tamthiliya hizi unasifa kuu nne: 1. Tamthiliya ya aina yoyote lazima iwe na majibishano (yaani daiolojia) 2. Tamthiliya lazima iwe na wahusika ( wahusika wakuu (aweza kuwa nguli), wahusika wadogo (bapa au mviringo), pamoja na mtoa maelezo au mfafanuzi (maranyingi huwa ni sauti). 3. Tamthiliya lazima iwe katika muundo wa pembe tatu, japo si tamthiliya zote (yaani socretic pla...