Posts

Showing posts from July 21, 2016

YATUPASA KUTIANA MOYO SIKU ZOTE

Wakati mwingine watu hujiua au hujinyonga kwa sababu ya kushindwa kuvumilia na kuzikabili changamoto. Jambo hili la kujiua kwa watu wengine husababishwa na kukosa tumaini katika maisha, kwa kukosa uwezo wa kuhimili changamoto na ugumu wa maisha. Kutumia vileo, madawa, sigara na vitu vituleteavyo madhara na kuathiri afya zetu, hutukosesha uhakika wa kuishi tena. Kutojari kanuni na taratibu za afya katika miili yetu juu ya nini tule, tunywe na tuweke juu ya miili yetu husababisha magonjwa katika miili yetu, hivyo hupunguza uwezo wa kuishi maisha marefu. Kuteseka ni lazima kuje ili kuyafikia mafanikio mapya. Ni vigumu kuyafikia mafanikio bila kuteseka kwa namna moja au nyingine. Kupiga hatua na kulikabili jambo fulani kunahita maamuzi yanayoumiza wakati mwingine. Hata kama mengine yanaumiza lazima tukubali, kuyapokea na kufanya badiliko. Kuna muda, mtu hufanya mambo fulani kwa sababu fulani; kila mtu hujikuta katika mkondo au maisha jinsi yalivyomchagulia namna ya kuishi, lakini ...