Posts
Showing posts from June 6, 2016
MAKABURI MAJINI
- Get link
- X
- Other Apps
“Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu” (Kol.2:12). Katika ubatizo wa Biblia mtu anazikwa katika kaburi la maji na kutoka humo akiwa amefufuliwa kuishi maisha mapya katika Kristo kwa nguvu za Mungu, yaani, Roho Mtakatifu. Hivyo ubatizo una maana yenye kina na ni zaidi ya kuzikwa tu ndani ya maji na kutoka. Unawakilisha kifo, kuzikwa na kufufuka kwa Yesu Kristo. Paulo anafafanua kwa kusema, “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi t ue ne nde k ati k a upy a wa uz i ma ” (Rum.6:4). Wokovu wetu unategemea kifo na kuzikwa na kufufuka kwa Yesu Kristo. Kama hatua zote za awali zimechukuliwa, mtu anayebatizwa anatarajiwa kuendelea kuishi maisha mapya ya ushindi dhidi ya d...