MFANO WA MPANGO KAZI
KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO LIWALE MPANGO KAZI WA OFISI YA MAKATIBU/MAKARANI WA KANISA (2015/2016) UTANGULIZI. Idara/ofisi ya karani/katibu ni idara nyeti ambayo inaunganisha shughuli zote za kanisa. Kutokana na wengi wa wahiriki na viongozi wa kanisa au makarani/makatibu wenyewe kutoipa kipaumbele idara hii ni kwa sababu ya kutojua uthamani wake katika ukamilifu wa safari yetu ya kwenda mbinguni. Kazi ya ukarani imeanza toka enzi za kale, ambapo hadi sasa tunapata takwimu, kumbukumbu na taarifa sahihi kwenye biblia (Mfano; Kutoka 1:1-5 n.k.). Bila huduma za kiukarani biblia ingekuwa kitabu kisichojithibitisa maana kingejichanganya kwa kukosa kumbukumbu. Mambo mengi yameandikwa juu ya umuhimu wa kuweka mpango kwa kila jambo afanyalo mtu. Kanisa hali kadhalika lina wajibu wa kujua madhumuni ya uwepo wake pamoja na mazingira yanayolizunguka kwa kuzingatia umuhimu wake kama inavyosisitizwa katika maandiko matakatifu; kuwahubiri mataifa habari njema ya wok