MFANO WA MPANGO KAZI
KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO LIWALE
MPANGO KAZI WA OFISI YA MAKATIBU/MAKARANI WA KANISA (2015/2016)
UTANGULIZI.
Idara/ofisi ya karani/katibu ni idara nyeti ambayo
inaunganisha shughuli zote za kanisa. Kutokana na wengi wa wahiriki na viongozi
wa kanisa au makarani/makatibu wenyewe kutoipa kipaumbele idara hii ni kwa
sababu ya kutojua uthamani wake katika ukamilifu wa safari yetu ya kwenda
mbinguni. Kazi ya ukarani imeanza toka enzi za kale, ambapo hadi sasa tunapata
takwimu, kumbukumbu na taarifa sahihi kwenye biblia (Mfano; Kutoka 1:1-5 n.k.).
Bila huduma za kiukarani biblia ingekuwa kitabu
kisichojithibitisa maana kingejichanganya kwa kukosa kumbukumbu. Mambo
mengi yameandikwa juu ya umuhimu wa kuweka mpango kwa kila jambo afanyalo mtu.
Kanisa hali kadhalika lina wajibu wa kujua madhumuni ya uwepo wake pamoja na mazingira
yanayolizunguka kwa kuzingatia umuhimu wake kama inavyosisitizwa katika
maandiko matakatifu; kuwahubiri mataifa habari njema ya wokovu wa Bwana YESU,
ili wamjue; Na kuwavua watu. Luka 5: 1-11.
Aidha kanisa lina
wajibu wa kutoa huduma mbalimbali za kijamii kama afya, elimu na kisha kutoa taarifa
na takwimu juu ya waliopatiwa huduma hizo. Ofisi ya makatibu wa kanisa iliona
umuhimu wa kupanga ili kuweza kutimiza malengo yake ya muda mfupi, muda wa kati
na muda mrefu. Maandiko Matakatifu yanasisitiza umuhimu wa kupanga kabla ya
kuanza utekelezaji. Kupanga kunaokoa wakati, kunarahisisha mambo na pia
kuepusha migongano na muingiliano wakati wa utekelezaji.
DHUMUNI
LA MPANGO KAZI.
Dhumuni la mpango kazi huu ni
kubainisha njia sahihi na rasilimali zinazohitajika ili kuweza kutambua,
kubaini takwimu na taarifa sahihi za idara na washiriki katika kanisa ili
kulijenga kanisa katika misingi ya mitume na manabii kama walivyotoa taarifa
sahihi, na takwimu sahihi kwa zama zile.
DIRA “Idara/ofisi
yenye kutambua na kufahamu takwimu sahihi za washiki wa kanisa na kuratibu
utekerezaji wa idara zote za kanisa na kuhifadhi kumbukumbu zote za kanisa”
DHAMIRA
“Ofisi/idara
kuwa na utaratibu wa kutunza kumbukumbu na kutoa taarifa, kuandaa vikao,
kusimamia na kuratibu vikao vyote vya baraza na mikutano mikuu ya kanisa”.
KAULI MBIU
“Hati
safi kwa utendaji mzuri wa kazi yeenye Kiango”
Kuwa na mifumo mizuri na ya kisasa na taratibu nzuri za kutunza
kumbukumbu za kanisa.
MALENGO.
Kutokana na uhitaji wa utendaji kazi mzuri,
idara/ofisi imekusudia kutekeleza malengo yafuatayo:
Kuandaa na kusimamia kikamilifu kalenda
za vikao vya mabaraza na mikutano mikuu ya kanisa.
Kutoa na kuweka wazi taarifa zote za
kanisa na washiriki wa kanisa wanapotoka na kuingia.
Kuhakikisha ufuatiliaji wa ushirika kwa
kila mgeni ajaye na kukaa kwa muda mrefu sambamba na kutoa elimu juu ya umuhimu
wa kuwa na ushirika katika kanisa mahalia
Kujenga uhusiano mzuri na idara zingine
za kanisani katika kupokea na kutoa taarifa mbalimbali zinazohitajika
Kuandaa na kutengeneza benki ya takwimu
sahihi za kanisa na idara zote za kanisa.
Kusimamia vyema taratibu na kanuni za
kanisa kama zilivyo kwenye muongozo wa kanisa.
UTEKELEZAJI
s/n
|
Malengo
|
Mikakati
|
Mhusika
|
Muda wa utekelezaji
|
Matokeo
|
01
|
Kuandaa na kusimamia kalenda za vikao
|
Kuandaa ratiba na kutoa tarifa kwa vikao vyote
|
Frank Philemon
|
Ifikapo mwezi wa 3 kuwe na karenda/ratiba ya vikao
vyote vinavyotakiwa kufanyika
|
Vikao vilivyo katika mpangilio maalumu
|
02
|
Kutoa na kuweka wazi taarifa kanisa za washiriki
wake
|
Kila wiki ya kwanza ya robo ya mwaka kutoa taarifa
juu ya ukuaji wa kanisa na maendeleo yake.
|
Anitha thobias
|
Mara nne kwa mwaka
|
Kujua tahimini ya ukuaji na maendeleo ya kanisa
|
03
|
Kuhakikisha kila mwadventista mgeni awe na ushirika
endapo atakaa kwa muda mrefu
|
Kutambua wageni wote kwenye siku za ibada
|
Makarani wote
|
Kila wiki
kwa ibada za sabato na za katikati ya juma
|
Kuwabaini wageni ili kuwashawiasi waagize ushirika
|
04
|
Kujenga uhusiano mzuri na idara zingine
|
Kupeana na kupashana habari zinazohitajika na kuingiliana na idara
zingine
|
Anitha Thobias
|
Kila wiki na kila robo ya ya mwaka taarifa kukusanywa
kutoka idara zote
|
Kupata taarifa sahihi za mshiriki kwa kila idara
|
05
|
Kuandaa na kutengeneza benki ya takwimu ya washiriki
wa kanisa
|
Kujua elimu, kazi, umri, hari, jinsi na anapoishi mshiriki wa kanisa
|
Frank philemon
|
Mwishoni mwa mwezi wa 4
|
Kujua uhitaji, wa wa kila mshiriki
|
0606
|
Kusimamia
taratibu na kanuni za kanisa
|
Kila
kikao cha baraza na mkutano mkuu
|
Makarani
wote
|
Kila
Kikao
|
Kufuata
taratibu
|
CHANGAMOTO.
Ofisi ya makarani inaathirika na changamoto
zifuatazo zinazolikabili kanisa:
Mfumo hafifu wa mawasiliano ya kiteknolojia.
kanisa kutokuwa na mpango mkakati wa muda mfupi na mrefu.
Ufinyu wa vyanzo vya mapato (kwani kanisa limejitegemeza sana
katika zaka na sadaka pekee)
Idadi kubwa ya waumini kutokuwa na ushirika
Uhaba na kukosekana kabisa kwa baadhi ya vitendea kazi kwa ajili
ya idara/ofisi ya makarani na idara zingine
Kukosekana kwa ofisi na umeme katika maeneo ya kanisa
BAJETI
(MAHITAJI)
Endapo bajeti ya ofisi ya makarani itatekelezwa, itaondoa
changamoto kubwa zinazoikabili idara/ofisi ya makarani. Mpango wa bajeti wa
idara hii umebainisha katika uhitaji wa mambo yafuatayo hapo chini ili
kukamilisha kujenga msingi wake na hata uwabijibikaji kwa ujumla.
Luka
14: 28-30 “Maana ni nani kati ya ninyi kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi
kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kumalizia? Asije akashindwa
kumalizia baada ya kupiga msingi watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, wakisema
mtu huyu alianza kujenga akawa hana nguvu ya kumalizia”
1. Bajet ya Muda mfupi (Bajeti ya
Dharula)
Bajeti ya muda mfupi
inahitaji kutekelezwawake ndani ya mwezi wa pili kutokana na uhitaji wake
haraka.
S/No
|
Hitaji
|
Kiasi
|
Matumizi Yake Kiofisi
|
Utekelezaji
|
Chanzo Cha Pesa
|
01.
|
Stepula mashini1
|
6, 000/-
|
Kubania karatasi
|
Mwezi wa pili
|
Bajeti ya kanisa
|
02.
|
Counter book 1
|
2, 500/-
|
Mahudhurio ya kikao
|
Mwezi wa pili
|
Bajeti ya kanisa
|
03.
|
Punching mshn1
|
5, 000/-
|
Kutobolea
karatasi
|
Mwezi aa pili
|
Bajeti ya kanisa
|
04.
|
Kalam 10
|
2, 000/-
|
kuandikia
|
Mwezi wa pili
|
Bajeti ya kanisa
|
05.
|
Rula 1
|
500/-
|
Kupigia mistari
|
Mwezi wa pili
|
Bajeti ya kanisa
|
06.
|
File 7
|
14, 000/-
|
Kutunzia taarifa&takwimu
|
Mwezi wa pili
|
Bajeti ya kanisa
|
07.
|
Wino wa printa
|
20, 000/-
|
Copy & printing
|
Mwezi wa pili
|
Bajeti ya kanisa
|
08.
|
Gundi ya maji
|
2, 000/-
|
Kubndikia matangazo
|
Mwezi wa pili
|
Bajeti ya kanisa
|
09.
|
Modem
|
25, 000/-
|
Kwa ajili ya internet
|
Mwezi wa pili
|
Bajeti ya kanisa
|
10.
|
Pesa ya stempu
|
40, 000/-
|
Kutuma&kuagiza ushirika
|
Mwezi wa pili
|
Bajeti ya kanisa
|
11.
|
Rim paper 2
|
26, 000/-
|
Copy, printing & kuandikia
|
Mwezi wa pili
|
Bajeti ya kanisa
|
12.
|
Bahasha katoni 1
|
25, 000/-
|
Kutumia barua
|
Mwezi wa pili
|
Bajeti ya kanisa
|
13.
|
Pesa ya bando
|
15, 000/-
|
Kutuma taarifa
|
Mwezi wa pili
|
Bajeti ya kanisa
|
14.
|
Pesa ya tahadhari
|
30, 000/-
|
Dharula za kiofisi
|
Mwezi wa pili
|
Bajeti ya kanisa
|
15
|
Pesa
ya vocha
|
10,
000/-
|
mawasiliano
|
Mwezi
wa pili
|
Bajeti
ya kanisa
|
Jumla Ya Bajeti Ya Muda Mfupi Ni Tsh. 223. 000/=
|
2. Bajeti ya muda
mrefu.
Bajeti hii utekelezaji wake ni wa muda mrefu kulingana
na upatikanaji wa pesa pamoja na kutokuwa na uhitaji wa haraka sana, japo ni
muhimu kutekelezwa hadi ifikapo mwaka 2017.
S/N
|
Hitaji
|
Kiasi
|
Matumizi
|
Utekelezaji
|
Chanzo Cha Pesa
|
01.
|
Laptop
|
500, 000/-
|
Kuchapa na kutumia taarifa
|
2016/2017
|
Changizo kutoka kwa washiriki
|
02.
|
Printer (3 in 1)
|
350, 000/-
|
Kuprinti, kuskani na kunakilisha nyaraka za kanisa
|
2016/2017
|
|
Jumla ya pesa Tsh. 850, 000/=
|
Jumla kuu ya bajeti =
bajeti ya muda mfupi + bajeti ya muda mrefu
223, 0000 + 850, 000
1, 073, 000/=
Mpango kazi
huu umeandaliwa na idara ya makara (ofisi ya makatibu) wa kanisa
1. Anitha
Thobias (karani mkuu)
_________________________________
2. Frank
philemon (karani msaidizi) _________________________________
Helpful
ReplyDeleteThank you the man kind
DeleteThank you the man kind
DeleteSafi mkuu imekua mbaraka sana kwangu
ReplyDeleteNaweza pata soft copy ya tamplete hii!?
yes wawezapata, nicheki kwa 0762426746
DeleteNaomba Msaada Wa Mawasiliano wa Katibu Mkuu na katibu Msadizi kwa msaada wa uandishi wa Mpango kazi
ReplyDelete