KWA WANAWAKE WOTE WALIO KATIKA NDOA
Tabia ya mwanada hujengwa au
huathiriwa na mambo mawili; mosi ni nitabia aliyorithi kutoka wazazi (yaani Nature)
2. Ni tabia aliyoipata kutokana na mazingira
aliyokulia na kuishi kwayo (yaani Nuture). Tabia ya kurithi kutoka kwa wazazi yaweza
athiriwa na kubadirika kwa sababu ya mazingira
anayoishi na kukuli, pamoja na jamii inayomzunguka. Hivyo basi, andiko hili linasehemu
na mchango wa kuibadirisha jamii ya kinamama walio katika ndoa zao aidha, kwa muda
mrefu au mfupi, na wale wanaotarajia kuingia katika tasisi hiyo ya wanandoa.
Kwa hiyo, wanawake walio katika ndoa kunamambo
ya kujifunza mengi yenye kujenga ndani ya kitabu cha tano cha Mithali za Mfalme
Sulemani. Ni nukuu ya maneno ya Mfalme Lemueli; Muasia kama alivyofundishwa na
mama yake ambayo Sulemani aliyaandika katika kitabu cha Mithali. Mafundisho
hayo ni ya msingi kwa kiasi kikubwa kwa mwanamke aliye katika ndoa. Pitia kwa
umakini ili upate mambo kadhaa ya kujifunza na yenye kujenga fikra njema na
nzuri kwa ustawi wa ndoa na familia:
1. Mwanamke katika
ndoa yake, anamchango mkubwa wa kuleta mafanikio, hivyo mume yampasa kuweka
imani kubwa juu ya uwezo wa mkewe katika kuleta mafanikio ya familia. Mithali
31:11 “Moyo wa mumewe humwamini, wala hatakosa kupata
mapato”
Kiasi kikubwa cha
maendeleo ya familia kwa wanandoa huchochewa na mwanamke. Mwanamke ni katibu na
mtendaji kazi mkuu wa familia. Mwanamke asiposimama imara katika familia, basi
mambo mengi yatayumba katika familia au kwa wanandoa. Kwa dunia ya sasa, siungi
hoja wala mtazamo juu ya mwanamke kuwa “goal keeper”. Dunia ya sasa ni
kusaidiana katika kusukuma maendeleo na mafanikio ya familia. Maisha yamepanda
na mahitaji yameongezeka katika kulea watoto na kuishi kwa ujumla.
Kunahaja ya mwanamme
kumwamini mkewe kuwa anasehemu kubwa ya kuchangia maendeleo, sio kila mara
atakapo kununua kitu aombe kwa mumewe pesa. Mwanamke kuwa tegemezi kwa mume kwa
kila kitu, ni kuandaa janga kubwa hapo badae; maana mwanamme huyo abebaye
jukumu lote la kuhudumia kunakufariki, kufukuzwa kazi, kuugua kwa muda mrefu, au kufungwa; na hapo yaweza kuwa ndio mwisho
wa watoto kusoma shule za gharama, na mambo mengine kupwaya.
Endapo mwanamke atapewa
nafasi na kuaminiwa katika michakato ya kutafuta, kujishughulisha, mume aamini
familia yake haitalala njaa, au kuombwa pesa mara kwa mara toka ukweni. Mwanamke
mvivu, asiejishughulisha ni mzigo kwa mmewe, anakwamisha maendeleo ya familia
na hafai kuwa mama wa kigwa isipokuwa kwa kukatazwa na mumewe.
2. Mwanamke katika
ndoa yake daima atende mema kwa mume wake pasipo kikomo. Mithali
31:12 “Humtendea mema wala si
mabaya, Siku zote za maisha yake”
Mwanamke mwenye hekima,
anayemtumainia Mungu, hapaswi kumtendea mabaya mumewe siku zote za maisha ya
ndoa. Si vyema kumsema vibaya mume wako, kutoa siri, mapungufu na udhaifu wa
mme wako kwa watu wengine. Sio sawa kumuwazia mabaya mume wako, wala
kutomthamini wala kutomjali, au kumdharau, kumsaliti na kumjibu kwa jeuli mume
wako. Mtendee mema, mazuri, mume wako. Pale anapokukosea nena naye kwa adabu na
hekima.
Ikitokea mume wako
amekukosea, jitahidi kumsamehe na umuombee badala ya kumjengea chuki, au
kumwekea kisilani na kumnunia. Epuka kuwa na hasira juu ya mume wako. Daima
tambua kuwa, wewe na mume wako ni mwili mmoja, hivyo mnene, mnuwie mamoja ili
kustawisha familia yenu. Upendo wako usipungue juu ya mumeo. Upendo wako udumu
bila kujali muda, wakati, mazingira, sehemu na hari ya kimaisha; upendo wako
juu yake utamalaki.
3. Mwanamke katika
ndoa yampasa afanye kazi zake kwa moyo na bidii. Mithali 31:13 “Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo”
Mwanamke mwenye
kumtumainia BWANA, ni mwenye bidii katika kufanya kazi na kutafuta. Hufanya
kazi za nyumbani na za kiuchumi kwa moyo wa bidii, na hakomi kuonesha bidii
katika kutafuta, ilimladi yote hayo anatenda kwa sababu ya ustawi wa familia
yake. Wakati mwingine, haina haja ya dada wa kazi kufanya sehemu ya majukumu
yanayomhusu mmemeo. Mwanamke atawaliwapo na moyo wa upendo utokanao na upendo
wa kimbingu, hana mawaa, kujivunga, kujiona, kujikweza katika suala la majukumu
ya kifamilia, nay ale yote yanayohusu ustawi na afya ya familia yake.
4.
Mwanamke katika ndoa ni mtafutaji na ana moyo wa
kujituma hata kweda maeneo ya mbali. Mithali
31:14 “afanana na merikebu za biashara; huleta chakula chake
kutoka mbali”
Unajua kunawakati wmingine
baba wa familia kukwama na hutingwa na majukumu kadha wa kadha, mwanamke-mwanandoa
chukua sehemu ya majukumu mumeo katika kusimamia na kusaidia majukumu ya
kifamila. Mathalani masuala ya shamba, miradi, kupeleka na kuona watoto shuleni
au kufuatilia maendeleo ya watoto ya kishule hata kama ni mbali kiasi gani.
Jingine, mwanamke awe
radhi kutembea umbali mkubwa ili kutafuta au kuvuna chakula kwa ajili ya
familia yake. Wapo wanawake wanandoa, hawawezi kwenda kisimani kuchota maji,
kwenda shambani kuvuna mazao, kwenda kwenye mradi kusimamia kisa pako mbali na
nyumbani. Aina ya wanawake wa hivyo ni wavivu wa kutupwa na hawana moyo wa
kufanya jambo ili kuhudumia na kustawisha familia yake. Wapo radhhi kulaza na
kushindisha njaa familia wato kwa sababu ya umbali kiasi wa shamba, kisima,
soko n.k.
5.
Mwanamke katika ndoa huamka mapema ili kupangilia na
kuandaa chakula cha familia yake. Mithali 31:15 “Tena huamka kabla
haujaisha usiku; huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi sehemu zao”
Uhai wa familia upo
mikononi mwa mwanamke. Katika masuala ya nini kipikwe, nini kiliwe na kwa kiasi
gani na kwa wakati gani ni jukumu la kifamilia ambalo lipo chini ya mamlaka ya
mwanamke. Tena yampasa mwanamke kuamka
asubuhi ya mapema kuhakikisha uhakika na upatikanaji wa chakula kwa wanafamilia
wote. Haina haja ya kubagua katika utoaji wa huduma ya chakula, wote wapatiwe
hata kwa wale sio wanafamilia ilimradi wapo malango mwa familia.
Hoja ya kuamka mapema
asubuhi na kuandaa chakula cha familia, ni jambo la msingi kwa mwanamke katika
ndoa. watoto waendapo shule waondoke wamekula (kunywa chai); baba wa familia aendapo
kazini aondoke nae akiwa amekunywa chai au kula chakula. Kula kwa pamoja
asubuhi kutawaepushia gharama za maisha katika kufanya mgawanyo wa pesa na
matumizi. Haipo sababu ya baba, mama na watoto wa shule kutumia pesa ili kunywa
chai migahawani wakati uwezekano wa mama kuamkana mapema asubuhi kuandaa
chakula cha asubuhi kasha wanaoenda kazini waende na wanao enda shuleni waende.
6.
Mwanamke hutafuta mapato kwa ajili ya kuwekeza na kununua
vitu, mali au miradi itakayonyanyua
uchumi wa familia yake. Mithali 31:16 “Huangalia shamba,
akalinunua; Kwa mapato yake hupanda
mizabibu”
Wapo wanandoa (wanawake)
wengi huwekeza pesa zao katika nguo, kula, mapambo, vipodozi na mambo mengine
ya anasa. Mwanamke mwenye akili huchuma na kuweka kwa ajili ya manufaa ya badae
ya watoto. Mwanamke jitahidi kubana matumizi, tumia pesa palipo na jambo la
msingi. Endapo mama wa familia unapesa na inaweza kutumika kuwekeza kwenye
mradi au shughuli fulai, wekeza; huwezi jua kesho inakuwaje, huo mradi
uliowekeza waweza kusaidia watoto wenu au kuwainua kiuchumi.
Mwanamke mwenye kuipenda
familia yake, huwekeza kwa ajili ya familia aipendayo, ili siku za usononi
papatikane manufaa. Wekeza kwenye elimu ya watoto. Mwanamke uliye katika ndoa
usiache kusomesha watoto utakuwa umewanyima hazina yao ya badae. Haina haja ya
kutapanya pesa ovyo, wekeza kwa ajili ya maendeleo na mafanikio ya familia
yako.
7.
Mwanamke ya mpasa awe shupavu na imara katika suala la
kujituma na kuchapa kazi. Mithali 31:17 “Hujifunga nguvu
viunoni kama mshipi: Huitia mikono yake nguvu”
Mwanamke akiwa mlegevu na
mtepetevu, kwa kila jambo, basi hapana asubuhi katika kufanikisha kuinyanua
familia yake. Hataweza kuwajenga watoto wake katika moyo wa kupenda kazi, maana
yeye hawezi kufanya hivyo. Mwanamke mwanandoa funga mkanda, kibwebwe, mshipi
kiunoni kakamaza mikono ili kuikomboa familia. Mwanamke akijikomboa, amekomboa
familia na taifa, hivhohivyo hata katika kujikomboa kifikra. Kwenye ndoa sio
wakati wa kupiga vijembe na mashosti, huwa ni wakati wa kupambana ili
kuimalisha uchumi, mafanikio na maendeleo ya familia.
Miaka ya nyuma kidogo,
jamii ya wasukuma iliangalia sifa kuu ya mwanamke kuolewa ni uchapa kazi na sio
sura wala uzuri wake, maana ilikuwa ni aibu familia kupata njaa hali kwamba
shamba lipo na nguvu kazi ipo (bibi na bwana). Familiazilizojengwa katika
uchapa kazi zilikuwa na asilimia kubwa
ya kutoka kimaisha, ndio maana anahimiza “Hapa
Kazi Tu” sababu anajua msingi wa jamii ya wasukuma, anaamini na kalelewa
hivyo. Sio kulima tu, kila kitu kinahitaji juhudi na moyo wauchapa kazi.
8.
Mwanamke katika familia yake, awe na akiba ya faida ya
mapato yake ili asipungukiwe. Mithali
31:18 “Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki
usiku”
Mwanamke laziwa awe
mwanauchumi, ajitahidi kuhifadhi faida iliyotokana na nguvu kazi yake. Lakini
pai yampasa afanye mahesabu mazuri kwa
kile anachotaka kuwekeza (katika mali au bidhaa), kufanya na ajue kuwa
kitamletea faida hapo badae na sio hasara. Taa (mtaji) yake ya idumu kuwaka
ikiwa na mafuta tele. Yaani mtaji wake usidi kuongezeka kila siku bila kukata.
Mwanamke mwenye fikra pevu, huwekeza kwenye mambo yaletayo faida na sio yatayo
hasara.
9.
Mwanamke katika ndoa, mikono yake iwe shupavu katika
kutenda na kufanya kazi. Mithali 31:19 “Hutia mikono yake
katika kusokota; na mikono yake huishika pia”
Hapana kitu kizuri kama
kuona maufaa na mafanikio yatokanayo na kazi ya miko yaklo. Vivyohivyo kwa
mwanamke kutia mkono katika kujenga
maendeleo ya famila yake. Mwanamke atakuwa na amani, umiliki na amrijuu ya mali
au mapato ya familia yake maana akili na mkono wake utakuwa umechangia
kuyaleta. Mwanamke uliye na ndoa penda kujishughulisha kwa kutumia uwezo na
mikono yako, kufanikisha ukuaji, ustawi, mafanikio na maendeleo ya familia
yako. Usimuachie mume wako, ukaja kukosa sauti, amri na haki ya umiliki katika
mali za familia yako.
10. Mwanamke katika
ndoa na familia yake, awe na moyo wa ukalimu, huruma, kutoa na kusaidia wengine
(wahitaji na masikini). Mithali 31:20 “Huwakunjulia
masikini mikono yake; Naam, Huwanyoshea wahitaji mikono yake”
Wanawake wengi wanaongoza
kuwa na roho mbaya kwa kukosa hata tone moja la ukalimu na moyo kusaidia
wengine. Huwanyanyasa na kuwasimanga wale wasio wa upande wa familia yake. Dada
wakazi , kaka wa kazi, wageni n.k. huchambwa, hunyanyaswa, huonewa na huteswa
na hawa mama wa familia. Hapana, mwnamke mwanandoa usifanye hivyo, mwanamke
ameumbiwa roho ya huruma yenye rehema nyinngi.
Mwanamke anaemcha Mungu ni
sehemu kisima cha busara na msaada wa mawazo kwa jamii na wanafamilia
wanaomzunguka. Roho ya kutoa, kusaidia wahitaji na masikini pamoja na kukalimu
wageni ndivyo hufungua mibaraka ya familia. Roho mbaya na ukali hukimbiza
wageni katika familia, na kupelekea kufunga mibaraka kutoka kwa Baba wa Mianga.
Hata kama umetokea ukulyani, roho yenye huruma ndiyo sifa kuu na tabia ya
mwanamke. Mwanamke mwanandoa jenga tabia ya kuvaa viatu vya matatizo yaw engine
(aweza kuwa mumeo), hurumia na kumbuka kuwaombea walio katika shida. Kufanikiwa
kwako usigeuke na kuwachapia na
kuwatesea wengine mali zako.
11. Mwamke ahakikishe
usalamawa wa afya ya familia yake.
Mithali 31:21 “Hawahofii theluji watu wa nyumani mwake; Maana wote
wa nyumbani mwak huwavika nguo nyekundu”
Kuwavika nguo nzito
wanafamilia wakati wa baridi kari, ni moja ya jambo linaloelezea kitendo na
hari ya ujalifu (kujali) kwa mwanamke miongoni mwa wanafamilia wake. Ni jukumu
la mwanamke kujali, kuzingatia suala la usalama wa kiafya la wanafamilia wote.
Mfano kunya maji yaliyochemshwa, motto yupi amechemka kwa sababu ya homa, tiba,
chanjo, na lishe kwa wanafamilia. Kwa hiyo kwa sehemu kubwa, mwanamke ndiyo
mwangalizi na mfuatiliaji wa mambo mengi ya kifamilia kuliko baba wa familia.
Hivyo basi uhai na usalama wa kiafya upo kwa mama wa familia hata kama kuna
dada wa kazi.
12.
Mwanamke katika ndoa yake awe hodari katika ubunifu na
na unadhifu katika mavazi yake. Mithali
31:22 “Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani
safi na urujuani”
Mambo ya upambaji, usafi
wa nyumba, usafi wa vyombo, mpangilio wa vitu ndani, na utunzaji wa mali za
ndani, sehemu kubwa ya jukumu la mama wa familia. Ubunifu wa mapambo ya ndani,
mfano kusuka na kufuma vitambaa, kudalizi mashuka n.k. ni jukumu linalosimamiwa
na mama wa nyumba pia.
Mama wa familia lazima
ajijali katika usafi wa mwili na mavavi pia. Avae mavazi nadifu yenye kuvutia
hata kama sio ya bei ya gharama kubwa, bali mpangili na usafi pekee ndio
kinachomata. Kuolewa kwa mwanamke sio kuwa ndiyo kikomo cha kujiweka safi
katika hali ya unadhifu. Usivae nguo zinazokushushia heshima, bali vaa nguo
zinazostili mwili vyema. Usivae nguo zikupasazo kuvaa wakati mkiwa wawili; wwe
na mme wako. Kuvaa nguo zisizo za heshima na za kuaibisha, ni kujiaibisha,
kujidhalilisha, kujipunguzia heshima na kumdhalilisha mmeo na wanao pia.
13.
Mwanamke katika ndoa amletee na kumjengea heshima mumewe.
Mithali 31:23 “Mume wake
hujulikana malangano; Aketipo pamoja na wazee wa nchi”
Mke mwenye uchaji wa Mungu
ni yule asiyeuaibisha ubavu wake, bali huuletea heshima kwa jamii inayomzunguka
kutokana na matendo yake mema na mazuri. Sifa njema za mwanamke ni fahari kwa
mume wake, na tabia mbaya nia aibu kwa
mumewe. Tabia mbaya kama usengenyaji, uchonganishi, uvivu, kiburi, matusi,
majigambo, wizi, utapeli, ulevi kupita kiasi, umalaya, uasherati, utumiaji wa
madawa ya kulevya kwa mwanamke, yote humchafua mumewe na aibu humjaa na asiwe
na jambo la kujivuni juu ya mke wake.
Tabia njema kama ukarimu,
hekima, busara, maarifa, uchapa kazi, matumizi mazuri ya lungha, heshima n.k.
ni sifa kwa familia na mume wake. Mwanamke mwanandoa epuka kumuaibisha mme wako
kwa mambo, mienendo na tabia mbaya na mbovu kuelezeka. Hujui tu yaweza kuwa
hata hawezi kuongozana na wewe hata kukutambulisha kwa jamaa na rafiki zake
kutokana na tabia mbaya.
14.
Mwanamke katika ndoa ajitahidi na yeye kujishughulisha
ili asiwe mzigo na tegemezi kwa mume wake. Mithali
31:24 “Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya
biashara mishipi”
Jambo la mwanamke
kujishughulisha ili asiwe mzigo kwa jamii na mme wake, nimelizungumzia kwa kina
katika aya zilizopia huko juu. Hoja ya msingi, nashauli si vyema mwanamke akawa
tegemezi, japo mwanamme ananafasi ya msingi kumhudumia. Swali je, itakuwaje
endapo mtafutaji atafariki, kupata ulemavu na ugonjwa wa akili wa kudumu? Fanya
utafiti na wewe kw suala hilo.
15.
Mwanamke mwye hadhi Na atendae kazi Kwa nguvu, hawazi
jinsi gani aishi kesho, Bali huufulahia wakati ujao maana anajiamini katika
kutafuta. Mithali 31:25 “Nguvu na hadhi,
ndiyo ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao”
Mwanamke mchapa kazi ana
amani na matumaini juu ya kesho yake na familia yake. Kutokana na uchapa kazi,
hana wasiwasi na maisha, maana anamoyo wa bidii ambapo anaamini haishi kwa
kubahatisha wala hawezi kumtegeme mme wake na kukaa akiwaza juu ya kukosa na
kufanikiwa kwa mmewe.mwanamke anaetegemea mafanikio ya mume wake, hanamatumaini
kw a sababu uhakika wa kupata ama kukosa mkate wa familia upo juu ya kupata au
kukosa kwa mme wake.
16. Mwanamke katika ndoa ajitahidi kuwa mwema
na mwenye hekima. Mithali 31:26 “Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na
sheria ya wema i katika ulimi wake”
Inaaminika kuwa asilimia
kubwa ya wanamke ni waongeaji sana kuliko wanaume. Kubarikiwa kuongea sana kwa
mwanamke sio kigezo cha kinywa chake kukosa hema na utaratibu kunena
yaliyomema. Mwanamke mwenyehekima hatumii ulimi wake vibaya ili kuleta magonvi
ndani ya ndoa yake. Matusi ya ajabu na ya nguoni, lugha isiyo ya staha pamoja
na majibu yasiyokuwa ya hekima na maadili yenye kuudhi si vyema ya katumiwa na
mwanamke aliye katika ndoa juu ya mmewe na watoto wake.
Majibu ya ovyo, matusi
maranyingi huchochea hasira kwa wale wagombanao kwa maneno. Mwanamke
mwenyehekima hunyamaza kimya, na hujibu kwa ustarabu na hekima pale mumewe
ajapo juu na akiwa amepandwa na hasira. Siraha kubwa ya kushusha hasira kwa mtu
juu yako ni kusema nisamehe au naomba samahani. Mwanamke mwanandoa, tambua hekima haiji bila kuiomba kwa
Mungu. Chanzo cha hekima ni kumcha Mungu, maana kwa Mungu ndiko kuliko na
kisima cha hekima alikozitoa mfalme sulemani. Hekima zitokanazo na Mungu
zitakuongoza kujua waka na maeneo ya kujibu, kunyamaza, kunyenyeke na
kujishusha juu y mme wako unapokuwa umemuudhi au kashikwa hasira.
17. Mwanamke katika
ndoa fuatilia kwa ukaribu tabia na mienendo ya watu wa familia yake pamoja na
kufanya kazi kwa bidii ili kuepuka kuwa mzigo au tegemezi kwa kila jambo. Mithali 31:27 “Huangalia sana
njia za watu wa nyumbani mwake; wala hali chakula cha uvivu”
Mwanamke katika ndoa ndiye
aliye makini katika kufuatilia kwa ukaribu mienendo na tabia za watoto pamoja
na wanafamilia wote. Marazote wanaume huwa ni wavivu wa kufuatilia mienendo na
tabia za watoto na wanafamilia wengine, lazima mama wa familia ujue kila kitu
kasha amjulishe baba wa familia kila kitu. Mwanamke ni zaidi ya mwandishi wa
habari katika uwezo wa kufuatilia vitu vingi kwa wakati mmoja, hiyo ndiyo sifa
kuu ya pekee ya mwanamke, tofauti na mwanamke.
Sio kila jambo mke
amfikishie mmewe, mengine yampasa kuyamaliza yeye mwenyewe, na yale ya watoto,
endapo likiwa kubwa liwasilishe na kutolewa taarifa kwa baba wa familia ili
asije akalaumu kwa kutokushirikishwa.
Mwanamke kufuatilia njia za watu wa familia ni jukumu lake la msingi,
maana ndiyo katibu mtendaji wa familia, hivyo ni lazima awe makini.
18. Mwanamke katika
ndoa ahakikishe familia yake inamfurahia kumjivunia na kumsifia kwa mazuri na
mema. Mithali 31:28 “Wanawe huondoka
na humwita heri; Mumewe nae humsifu…”
“Mnyonge mnyongeni, haki
yake mpeni”. Sifa njema ya mama wa familia ni Yule mwenye uwezo wa kuiunganisha
familia katika upendo, umoja, mshikamano, furaha na amani. Mama mwenye kuonya,
kushauri, kukemea na kufundisha kwa lugha ya upole na upendo. Kwa mazuri yote
ayatendayo kwa mumewe na watoto wake hakika hawana budi kujivunia, kumfurahia,
kumpenda na kumsifia.
Mama wa familia apendae
magomvi na hatangulizi upendo kama ngao ya kuleta amani katika familia, hawezi
akasifiwa na mumewe wala watoto, maana yeye kukicha kila siku ni magonvi kwa
kukuza mambo hata kama sio makubwa. Mwanamke amchae Mungu na mwenye hekima,
hutumia upendo kama siraha ya kurejesha amani, umoja na mshikamano katika
familia yake.
19. Mwanamke katika
ndoa awe mfano wa kuigwa kutokana na mazuri yake. Mithali 31:29 [Mumu humsifu
na kusema] “Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita
wote”
Mwamke mwenye kujua
majukumu na kuisimamia familia yake, jina lake kutajwa na kutamkwa kwa mema na
mazuri, kuanzia ngazi ya family na jamii inayomzunguka. Mazuri yake watu wa
jamii imzungukayo imtolee mfano wa kuigwa na barua njema kwa wengine. Mwanamke
mwenyekutenda mema na mazuri, mume wake hujivunia, hana budi kumsifiwa maana
jina lake jema lasomeka vyema kwa watu.
Kama mama wa familia hasomeki
vizuri katika mienendo na tabia yake, hawezi akarisisha mambo mazuri kwa binti
zake, hivyo basi binti zake waweza kukaa bila kuchumbiwa au kuolewa, maanatabia
ya mama yao sio nzuri. Sifa mbaya haiuziki hata kwa kuitembeza.
20.
Mwanamke katika
ndoa; wanafamilia na jamii imsifie kwa ucha Mungu na sio uzuri wake. Mithali 31:30 “Upendeleo
hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchae BWANA, ndiye
atakayesifiwa”
Wanawake wengi walio
katika ndoa huwa na mikoko, ujivuni, kujisikia na kujiona eti kwa sababu ni
wazuri wa sura na umbo, hivyo hawezi kuheshi, kumnyekea mumewe. Marazote uzuri
wa sura hudanganya, hivyo huharibu tabia ya mtu. Mwanamke amtumainie na kumcha Bwana
ndiye apatae sifa maana upendo na uzuri wa moyo watoka kwa Mungu.
Maranyingi wanawake walio wazuri wa sura ndiyo
wanaoongoza kwa roho mbaya na matendo mabaya pia na ndiyo waongozao kuleta migogoro
na kuvunja ndoa, maana anaamini kwa uzuri wake atapata mwingine. Mama mwanandoa
si vyema akatumia uzuri wake kama fimbo ya kumnyanyasa mume wake. Heri uzuri wa
moyo wenyekujenga, kuliko uzuri wa sura udanganyao wenye kubomoa.
21.
Mwanamke katika ndoa hata ukimpatia mapato ya mikono
yake hatabadirika kuiacha tabia yake njema. Mithali
31:31 “Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake ya msifu
malangoni”
Kunawanawake katika ndoa hubadirika
tabia wanapomiliki vipato vikubwa. Tabia hii imewafanya wanaume wengi kuwazuia wake
zao kufanya kazi/biashara ili kujiingizia vipato vyao binafsi na hivyo kuwafanya
kuwa mama wa nyumbani wakiwategemea waume zao kwa kila kitu na kila jambo. Mwanamke
amchae Mungu, habadiriki tabia, habadiriki katika kiwango cha upendo eti kwa sababu
ya mali, kazi, elimu au chochote kinachompatia kipato.
Upendo
wa kweli na tabia njema ya mwanamke kwa mume wake haujalishi kiasi gani cha pesa
au mali alizonazo. Hivyo basi, mwanamke mwenye upendo wa kweli na tabia isiyobadirika
kwa sababu ya pesa, mumewe hawezi kujizuia kumpatia mali, hwala kumzuia kuchakalika
katika utafutaji wa kipato chake binafsi. Si salama mwanamke akamsaliti mume wake
kwa sababu au tamaa ya pesa.
NB: Andiko hili ni sehemu
ya kitabu changu ninacho tarajia kukitoa, hivyo mchango wako wa kunikosoa na kunijenga
unahitajika isipokuwa lugha ya matusi pekee. Bado sijafanya editing, najua kuna
typhos nyingi
Mwl. Frank Philemon © 2016
Comments
Post a Comment
Thanks for viewing and passing through NMEE blog. Keep following the blog