MAKABURI MAJINI

“Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua  katika  wafu”  (Kol.2:12). Katika ubatizo wa Biblia mtu anazikwa katika kaburi la maji na kutoka humo akiwa amefufuliwa kuishi maisha mapya katika Kristo kwa nguvu za Mungu, yaani, Roho Mtakatifu.  Hivyo ubatizo una maana yenye kina na ni zaidi ya kuzikwa tu ndani ya maji na kutoka.  Unawakilisha kifo, kuzikwa na kufufuka kwa Yesu Kristo.

Paulo anafafanua kwa kusema, “Hamfahamu  ya  kuwa  sisi  sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi t ue ne nde  k ati k a  upy a  wa  uz i ma ” (Rum.6:4).  Wokovu wetu unategemea kifo na kuzikwa na kufufuka kwa Yesu Kristo. Kama hatua zote za awali zimechukuliwa, mtu anayebatizwa anatarajiwa kuendelea kuishi maisha mapya ya ushindi dhidi ya dhambi kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.Ubatizo waweza kuwa ni kwa sababu ya kutimiza haki yote kama Yesu alivyobatizwa katika mto Yordani.  Yeye hakuwa na dhambi zo zote kuweza kustahili kubatizwa.  “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwaYohana ili abatizwe.  Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa,  kwa  kuwa  ndivyo  itupasavyo k uti mi z a  hak i  yot e . Basi akamkubali.  Naye Yesu  alipokwisha  kubatizwa  mara ak apanda  k ut ok a  maj i ni ,  na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye” (Mt.3:1317).  Ikiwa ubatizo ulikuwa ni wa lazima kwa Yesu ili kutimiza haki yote, je! ni vipi kwetu sisi wenye dhambi?

Kwa kawaida sababu kuu ya kubatizwa  ni  dhambi.  “Ndipo walipomendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani; naye akawabatiza katika mto wa Yordani; huku wakiziungama dhambi zao” (Mt.3:5).  Watu wanaobatizwa wanapaswa ku“zaa matunda yapasayo toba” (Mt.3:8). Vinginevyo ubatizo utakuwa hauna maana kwao maana watakuwa hawajabadilika tabia zao.
Yesu  alimwambia  Nikodemo, “Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu” (Yn.3:5). Roho anaanza kufanya kazi ndani ya mtu ili kumbadilisha kabla ya ubatizo. Anamwonesha dhambi zake na kumvuta atubu na kumpokea Yesu kwa imani kama Bwana na Mwokozi wake. “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yn.1:12). “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya,  ya  kale  yamepita;  tazama! yamekuwa mapya” (2 Kor.5:17).

Hao huzaa matunda yapasayo toba na kuendelea kuishi maisha mapya baada ya kubatizwa.  Huenda wengi wanaorudi nyuma baada ya ubatizo hawakupitia hatua hii kabla ya ubatizo wao.  Wengine husahau  kiapo  chao  wakati wanapobatizwa. Wengine hawajasalimisha maisha yao kabisa kwa Yesu.  Kuna hatua za kufuata kabla ya ubatizo.

“Basi,  enendeni,  mkawafanye mataifa yote kuwa wanaf unz i , mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na  k uwaf undis ha  k uy as hi k a  y ot e  ni li y owaamur u  ninyi; na, tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari” (Mt.28:19,20). Kabla mtu hajabatizwa sharti la kwanza awe mwanafunzi, afundishwe yote aliyoamuru Yesu na akubali kuyashika yote (kiapo cha ubatizo). Baada  ya  kujifunza  Neno  la Mungu  imani  inazaliwa  ndani  yake, anampokea  Yesu  kama  Bwana  na Mwokozi wake kwa imani. “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe, Aaminiye na kubatizwa,  ataokoka;  asiyeamini atahukumiwa”” (Mk.16:15,16).  Hatua hizo mbili – kufundishwa na kuamini – ni za lazima kwa kila anayetaka kubatizwa. Mafundisho ya Biblia yako zaidi ya ishirini; mtu akiyaelewa yote atakubali kuishi  kwayo  kwa  nguvu  ya  Roho Mtakatifu.

Watoto  wadogo  kwa  kuwa hawawezi kufundishwa yote na kwa hiari yao  kuamini  na  kuamua  wenyewe kubatizwa,  hawabatizwi.  Badala  yake wanabarikiwa tu. “Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea.  Ila  Yesu  alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu; msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto  mdogo  hatauingia  kabisa. Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabar i ki a ” (Mk.10:13-16).
Ukiangalia huku na huku katika ulimwengu wa Kikristo leo unaona kuna ubatizo  wa  aina  nyingi.  Wengine wananyunyiza maji mara tatu juu ya kichwa; wengine wanamwagilia maji mara tatu; wengine wanazamisha mwili wote majini. Wengine wanaruka moto, wengine wanapita chini ya bendera na kadhalika. Jambo hili linazusha maswali mengi moyoni. Je, kuna ubatizo wa aina ngapi? Je, mtu akibatizwa kwa ubatizo usiokuwa wenyewe anahesabiwa kama amebatizwa
au la?  Je, kama ukijulikana ubatizo wa Biblia, hao waliobatizwa kinyume cha huo wabatizwe tena?  Wengine wanasema ubatizo wo wote unafaa tu.  Wengine wanadai kuwa ni dhambi kubatizwa tena. Ukweli ni upi?

Paulo, muumini wa ubatizo wa kuzikwa majini, anasema, “Mwili [kanisa] mmoja, a Roho mmoja,… tumaini moja… Bwana  mmoja,  imani  moja,  ubat iz o  m m oja. Mungu mmoja…” (Efe.4:4-6). Ingeshangaza sana na kuleta utata mkubwa kama Mungu huyo mmoja angeweka njia mbalimbali za ubatizo.  Mwili mzima unazikwa katika kaburi la maji kama alivyozikwa Yesu (Rum.6:4-11; Mt.3:16; Kol.2:12). Mtu aliyezikwa haonekani kwa macho. Amefunikwa kabisa na udongo au na maji. Ubatizo wa kuzamisha unahitaji maji  mengi  ili  mtu  anayebatizwa asionekane mwili wake juu (Yn.3:23).

Agano  Jipya  liliandikwa  kwa Kigiriki. Ubatizo ni neno linalotokana na neno la Kigiriki ‘bapt i z o ’ limanishalo kuchovya  au  kuzamisha  majini. Kunyunyiza maji kwa Kigiriki ni ‘r ant i z o ’. Angesema,  Enendeni  mkawarantize. Kumwagilia maji kichwani kwa Kigiriki ni ‘ek c hao ’.  Angesema,  Enendeni mkawaekchae. Hakusema hivyo.
Mtu aliyebatizwa kwa ubatizo wa kuzikwa majini kama hajui mafundisho makuu  aliyoamuru  Yesu  ayashike, atabatizwa tena baada ya kufundishwa (Mdo.19:1-5).  Mtu akiasi imani au kurudi nyuma au kutenda tendo linaloliaibisha kanisa katika jumuia, akiondolewa katika ushirika wa kanisa anahesabiwa kama Mmataifa  [Mpagani]  (Mt.18:15-18;  1 Kor.5:1-5,9-13).  Huyo atarudi katika ushirika  kwa  njia  ile  ile  mpagani anayoingia katika ushirika wa kanisa, yaani, kwa ubatizo. Huo ndio ukweli wa mambo. Hakuna dhambi kufanya hivyo. Kiapo cha ubatizo lazima kijumuishe mambo  yote  aliyoamuru  Yesu,  sio machache tu. Anayebatizwa anafungwa na yote.

Ndugu msomaji, kama hujabatizwa ubatizo wa Yesu wa kuzikwa katika kaburi la maji, basi amua kuchukua hatua zote na kula kiapo ili upate kuunganika na Kristo katika kifo, kuzikwa na kufufuka kwake na kuishi maisha mapya katika yeye kwa nguvu za Mungu.


         [TOA FOTOKOPI, UMGAWIE MWENZAKO]

Comments

Popular posts from this blog

MAJINA YA WANAWAKE KATIKA BIBLIA ‘A’ HADI ‘Z’

SOMO: MADHARA YA KUKATAA KUMTII MUNGU

MFANO WA MPANGO KAZI