YATUPASA KUTIANA MOYO SIKU ZOTE


Wakati mwingine watu hujiua au hujinyonga kwa sababu ya kushindwa kuvumilia na kuzikabili changamoto. Jambo hili la kujiua kwa watu wengine husababishwa na kukosa tumaini katika maisha, kwa kukosa uwezo wa kuhimili changamoto na ugumu wa maisha.
Kutumia vileo, madawa, sigara na vitu vituleteavyo madhara na kuathiri afya zetu, hutukosesha uhakika wa kuishi tena. Kutojari kanuni na taratibu za afya katika miili yetu juu ya nini tule, tunywe na tuweke juu ya miili yetu husababisha magonjwa katika miili yetu, hivyo hupunguza uwezo wa kuishi maisha marefu.
Kuteseka ni lazima kuje ili kuyafikia mafanikio mapya. Ni vigumu kuyafikia mafanikio bila kuteseka kwa namna moja au nyingine. Kupiga hatua na kulikabili jambo fulani kunahita maamuzi yanayoumiza wakati mwingine. Hata kama mengine yanaumiza lazima tukubali, kuyapokea na kufanya badiliko.
Kuna muda, mtu hufanya mambo fulani kwa sababu fulani; kila mtu hujikuta katika mkondo au maisha jinsi yalivyomchagulia namna ya kuishi, lakini hayo yote huwa ni matokeo ya bahati mbaya ambayo kuna muda huwa kwa uzembe wetu au kwa kuyaamini na kuyaishi tusiyoyamaanisha tukajikuta tumeyatenda vema. Kama umegundua ulipojikwaa yakupasa urudi nyuma na uanze upya tena.
Kila mtu anahistoria yake katika maisha yake lakini ikitokea ukajua unapokosea na kujirekebisha basi hiyo ni faraja ndani ya moyo wa kila mmoja aliyechukizwa na tabia yako ya awali, hivyo basi waweza kutubu dhambi zako na Mungu atakusikia. na kukusamehe
Kitu kidogo na cha pekee na cha thamani unachoweza kufanya katika maisha yako ni kutafuta nini unachokitumainia, na kikubwa unachoweza kufanya ni kuishi ndani ya matumaini hayo. Siyo tu kuyakubali kwa mbali ila kuyaishi kwa undani wake. Matumaini yanaweza kuwa nguvu kubwa yenye msukumo. Inawezekana kabisa kusiwe na miujiza ndani yake, ila ujuapo unachokitumainia sana na ukakikumbatia kama mwanga ndani yako, basi unaweza kutenda jambo na kufanya mambo yatokee kama miujiza. Kwa hiyo, yafanye matumaini yako yaishi. Jukumu moja wapo la binadamu ni kufikiri kwa niaba yako mwenyewe.
Katika kufanikiwa, binadamu lazima ajipange/wajipange vyema. Kila mtu ananafasi ya kuwa vile atakavyo, haijarishi njia atumiayo ilimradi upo ukweli wa kila jambo. Mafanikio huja tu pale unapoamua kufanya mambo magumu kuwa mepesi unapoamua kulitazama jua kwa ukali wake.
Kila binadam anahadithi na simulizi juu ya maisha yake. Aidha, ya kusikitisha pengine ya kukatisha tama, bali tunatofautiana namna ya kuzikabili huzuni zetu. Kila mmoja alishawahi kupitia jambo gumu la kukatisha tamaa , na wengingine waliteseka na kukubali matokeo ya jambo hilo na walisonga mbele.
Haitupasi kujiona kuwa hatuna bahati katika maisha. Yatupasa kujua kuwa maisha yanamambo mengi ambayo ni msamiati kwenye fikra zetu. Majibu sahihi kwa msamiati ambao hauujui ni kubahatisha jibu la swali ambalo hujalisikia kamwe; hivyo unachotakiwa kufanya ni kuiambia nafsi yako itawale utashi wako.
Maisha hutupa changamoto ili kupima ujasili wetu wa kubadirika. katika muda huo wa changamoto, nafasi ya kufanya kwamba hakuna linalotokea au kusema kuwa hauko tayari kuipokea hiyo changamoto. Changamoto hazisubiri utayali wako na maisha hayaangalii nyuma maana ni kama sheria mpya inayotungwa juu ya jambo fulani; huwa inaanza pale iliposainiwa. Wiki moja ni zaidi ya mudawa kutosha tunaouhitaji ili kuamua kama tunakubali au la. Japokuwa pia kuhitaji kwenda mbele kwenye maisha yako, lakini unaweza kukuta umeweka mguu mmoja kwenye “break”.
Nini thamani ya maisha kama tunaamua kwenda mbele kwa maisha ya kukanyaga breki. Ili uwe huru, lazima ujifunze kusahau na kuacha mambo mengine yaende zake. Acha kuumizwa na machungu, acha yaende kisha sahau. Maumivu yako na maisha yako ya zamani ndiyo yanayokuvuta nyuma na kufanya usisonge mbele. Kubali kuanza upya.
Watu waliofanikiwa zaidi ni wale walioyajua matatizo, walizijua harakati za maisha, waliokumbana na misukosuko na taabu, walioyakabili majaribu ya kila namna na changamoto zake na mwisho wa siku waliweza kusonga bele. Lolote ambalo haliwezekani leo, unaweza kulifany liwezekane kesho endapo utaamua tu juu ya mustakabali wa njia uipitayo.
NA MWL. FRANK PHILEMON 

Comments

Popular posts from this blog

MAJINA YA WANAWAKE KATIKA BIBLIA ‘A’ HADI ‘Z’

SOMO: MADHARA YA KUKATAA KUMTII MUNGU

MFANO WA MPANGO KAZI