MISINGI YA UFUGAJI WA KUKU WA ASILI.
FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU WA ASILI (1) Ni chanzo cha haraka cha pesa (2) Nyama ya kuku ni protein tosha (3) Kinyesi cha kuku ni mbolea (4) Maganda na manyoya ni mapambo Qn. Je wewe unajua faida zingine? Basi Zitaje. MAHITAJI MUHIMU KWA UFUGAJI KUKU WA ASILI (1) Mahali pa kuwaweka (2) Mahali pakupata huduma na ushauri (3) Mahali pakupata kuku wa kufuga (waliochanjwa dhidi ya mndonde) NYUMBA YA MALAZI YA KUKU WA ASILI (a) Nyumba iwe mahali penye kivuli (b) Paa liwe Refu kuruhusu kuingia mtu mzima (c) Nyumba iwe na uwezo wa kupitisha hewa (d) Mlango uangalie Kaskazini kupingana na jua(Mlango uruhusu mtu mzima kuingia ) (e) Iwe na mlango madhubuti na kufuli kudhibiti vibaka. NDANI YA NYUMBA YA KUKU...