GONJWA LA LEO LINALOENEA KWA KASI KWA WATU WENGI
Utangulizi
Pamekuwepo na panazidi kuongezeka magonjwa
mengi ya ajabubuajabu katika ulimwengu wa sasa tunaouishi katika dhama za
mwisho wadunia; hususani ndani ya sayari yetu Dunia. Magonjwa hayo yamekuwa
kikwazo na kusababishwa changamoto nyingi sana katika maisha ya mwanadamu.
Ukiachana na magonjwa ya kisaikolojia, kiakili, kimwili na mengineyo mengi sana
yanayozidi kubainika na kuongezeka siku hadi siku katika kizazi cha ulimwengu
wa sasa; lipo gojwa la muda mrefu, ambalolimedumu karine kwa karine.
Gonjwa hilo sugu ni kongwe kuliko magonjwa
mengine baadhi yaliyoibuka hivi karibuni. Gonjwa hili limekuwa likienea kwa
kasi ya ajabu kulingana kubadirika kwa mitindo ya maisha ya mwanadamu. Gonjwa
hili linajibainisha katika na hari na dalili zifuatazo:
Kupenda raha na maisha ya bila kutoa jasho,
Kupenda kulala kuliko kujibidisha,
Kukosa moyo wa kujituma,
Kupenda starehe kuliko kujishughulisha,
Kutokujitambua kwa sababu ya kukosa tafakuri, njozi
dira na malengo,
Kutotaka kuteseka ili kuifikia raha ya badae,
Kutojali muda au wakati na hupelekea kuahirisha kufanya
mambo kwa wakati, na
Kupoteza maarrifa
na ubunifu.
Gonjwa hili hakika linatisha, maana
ukilipata; tiba yake inahitaji kujikana nafsi, bila hivyo linaweza kukutesa
hadi wakati wa kufa, unakufa nalo na marehemu usiweze kukumbukwa kwa lolote juu
ya dunia hii. Ukiachana na magonjwa
mengine unayoyafahamu; gonjwa hili la ajabu na linalotisha kuliko magonjwa
baadhi mengi. Gonjwa hili kwa namna ya ajabu huwapata watu wenye afya zao
nzuri, wenye nguvu tele za kufanya kazi, wasio na ulemavu mowote katika miili
yao. Hakika ni gonjwa la pekee na laajabu sana.
Gonjwa hilo linaandikwa na kutamkwa kwa herufi
nne (irabu ni tatu na konsonati ni
mbili). Gonjwa hili linaitwa ‘‘UVIVU’’. Neno UVIVU ni neno ambalo haliwezi
kubadirika maana yake hatakama utasoma kinyumenyume, au ukitumia kioo; ndani
yakioo litasomeka vilevile bila kupoteza maana yake halisi. Gonjwa liitwalo
UVIVU, nitalizungumzi kwa kirefu katika upande wa hasara pekee, hasa linapokuwa
limempata mwanadamu aliye na nguvu, afya, na akili timamu.
Uvivu ni hari inayompata
mtu na asiweze kujituma katika kufanya kazi au kukosa uwezo au ari ya kufanya
kazi kwa bidii. Uvivu ni uzembe, na kinyume cha Uvivu ni kutofanya kazi kwa bidii. Uvivu kwa binadamu mwenye nguvu, afya, na akili timamu
unatokana na mtu mwenyewe kujiendekeza katika kutojibidisha, kutokuwa na moyo
wa kufanya kazi kwa bidii, kukosa ari ya kufanya kazi kutoka moyoni mwake,
kutojitambua kunakoendekeza maisha ya raha bila kujituma katika bidii ya
kufanya kazi. Mtu mwenye nguvu, afya, na akili timamu asipopenda kufanya kazi na kujituma katika bidii ya
kazi, huyo ni mgonjwa mwenyegonjwa
la uvivu.
Taifa lolote likiwa na watu wenye ugonjwa
utokanao na uvivu; tutegemee taifa lenye umasikini wa kutupwa maana watu wake
hawana ari, bidii, na moyo katika kufanya kazi. Uvivu kwa mtu mmojammoja
huzalisha umasikini kwa mtu mmojammoja, hatimae umasikini huo hupanda ngazi
katika familia na mwishowe taifa zima kwaujumla. Taifa la wavivu huzaa taifa
legelege lenyeombaomba na tegemezi hadi ngazi ya kitaifa.
Tabia au sifa ya uvivu uliokithiri kwa
watu, hupelekea wengi kupenda maisha ya mteremko na mepesi, ambapo hutafta
mafanikio yao kwa njia zisizohalali kwa kupata pesa zipatikanazo kinyume cha sheria,
utaratibu na maadili ya jamii. Ujambazi, biashara za kujiuza mwili, utapeli,
ukabaji, wizi, uzulumaji, kamali, kuombaomba ndizo shughuli za wengi
waliowavivu katika kuchapa kazi ili wapate pesa kwa uhalali. Mtu aliye mvivu na
asiyejishughulisha hufanya mambo mengi katika muda mwingi yale yasiyo na tija
ambayohuathiri uwezo, moyo na ari ya uchapa kazi. Mfano; kuzululaji, kukaa
vijiweni kupiga ili soga, umbea, utumiaji wa madawa ya kulevya, kuambatana na
makundi au marafiki wasiokuwa na mwelekeo wowote, n.k.
Vitabu vingi vya kiulimwengu na vya
kiroho/imani vinasisitza kufanya kazi kwa bidii ili kupata mafanikio au kupata
mali zilizo za halali zitokanzo na jasho la mtu husika anayechakalika. Huko
nyuma, zamani kabisa; kazi zikuwa mbili tu; ya kwanza ilikuwa ni kulima/kilimo pakifuatiwa na ufugaji wa wanyama. Leo hii kuna kazi
nyingi sana halali duniani ambazo mwanadamu awezafanya ili kujipatia kipato
kitakachomwezesha kuendesha maisha yake ya kila siku bila kutegemea serikali.
Kwa mujibu wa Bibulia Takatifu; kazi
ya kwanza ya mwanadamu wa kwanza (Adam) ilikuwa ni kulima (kulima na kuitunza
bustani ya Edeni) Mwanzo 2:15.
Shamba lako la weza kuwa karamu, ‘computer’,
gari, duka, soko, ajira, fani, ujuzi, kipaji n.k kiwezacho kukupatia kipato na
kukuletea mafanikio; hivyo basi, kwa aina yoyote ya shamba au kazi; fanya kazi
kwa bidii na kwa moyo wako wote. Yesu mwenye kabla ya kuanza kufanya kazi ya
injili, alifanya kazi ya uselemala aidha akiwa anamsaidia baba yake (Yusufu) au
yeye mwenye (Mariko 6:3); maana pia
Mungu hufanya kazi bila kuchoka (Yohana
5:17). Mitume wa Yesu nao walifanya kazi huku wakiipeleka injili. Mtume
Paulo anasema katika 2Wathesalonike 3:10,
“….ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi,
na asile chakula”. Ili ile, yakupasa ufanye kazi na ule jasho lako, na sio
uwe unakula jasho la wengine walohangaika kutafuta.
Sifa
na tabia za mtu mvivu pamoja na changamoto zake
Zifuatazo ni tabia na sifa bainishwa za mtu
mvi. Endapo mtu mwenye afya, ananguvu, hana ulemavu wowote wala matatizo ya
kiakili; akiwa katika sifa na tabia baadhi zifuatazo, basi mwanadamu huyo
gonjwa la uvivu:
1.
Mtu mvivu hupenda
kulala na huthamini usingizi kuliko kujituma
Mvivu yeyote hutumia muda mwingi kulala
(usiku na mchana) kama ilivyo nafsi yake, jua huchomoza yeye bado yupo kitandani
kila siku. Usingizi kwake ni starehe. Mvivu anaependa usingizi, njaa kwake ni
kawa maana hutumia muda mwingi kulala kuliko kutafta mkate (chakula) wake wa
kila siku. Mithali 19:15 ‘’Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na
nafsi yake mvivu itaona njaa’’. Mfalume Sulema anaonya na kututahadharisha katika Mithali
20:13; anasema “Usipende usingizi usije ukawa masikini;
Fumbua macho yako nawe utashiba chakula. Mvivu hujigeuzageuza kitandani
kama ilivyo kwa bawaba za mlango; ufungwapo na kufunguliwa (Mithali 26:14)
2.
Mtu mvivu hafanikiwi,
kwa sababu hana moyo wa kujituma
Yeyote aliyemvivu kufanikiwa kwa jambo
lolote kwake ni nadra sana, hiyo ni kutokana na kukosa ari ya kujituma kwa
bidii katika kufanya kazi yoyote na nasfi yake imefanyika kutopata na kufanikiwa.
Tofauti na mvivu, mwenye bidii hubarikiwa na hufanikiwa katika kujibidisha
kwake. Mithali 13:4 “Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu;
Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa”. Mara zote mtu Yule ajitumae
katika kufanya kazi kwa bidii, Mungu humbariki katika kupata mafanikio, maana
Mungu ameahidi “…. kubarikia kazi yote ya
mkono wako….” (Kumbukumbu la Torati
28:12)
3.
Mtu mvivu ni mzembe
wa kutupwa; hata kwa vitu au kazi isiyohitaji nguvu na maarifa yeye humshinda
Mvivu hata ukimsogezea fursa mlangoni kwake
umefanya kazi bure. Hata kama fursa zipo kila mahali, mvivu hawezi kuthubutu
katika kujisumbua kufanya jambo lolote, maana yeye kila jambo kwake ni kero na
usumbufu. Mtu mvivu ni sawa na mtu asiyeweza kufunga goli katika mpira wa
miguu, hata kama klinda mlango (goal keeper) akiondoka, yeye hawezi akafunga. Mithali 19:24 “Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini;
Ila hataki hata kuupeleka hata kinywanipake”. Pia Mithali 26:15, inazungumzia jambo lilelile.
4.
Mtu mvivu hujiona sahihi
kwa hali aliyonayo, hata kama akishauliwa hachukui hatua
Mvivu hawezi akashaulika kwa jambo lolote
la mafanikio yake, hujiona sahihi jinsi alivyo, hata ufanye vipi hawezi
akabadirika, maana kwake uvivu ni gonja linalomshambulia daima. Mithali 26:16 “Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake, kuliko watu saba wawezao
kutoa sababu”.
5.
Mvivu kutumika au
kwake kujituma ni kuchungu
Daima mvivu hapendi kutumika na kujituma
katika bidii ya kazi. Mvivu hukeleka,
huumia pale aambiwapo kufanya kazi au kutumwa kufanya kazi, na huwa mkali au
hulalamika sana apewapo majukumu ya kufanya kazi. Mithali 10:26 “kama siki
menoni, na moshi machoni, ndivyo alivyo mtu mvivu kwao wamtumao”.
6. Mvivu hutawaliwa, hufanywa mtumwa na wale wenyebidii na
waliofanikiwa.
Mvivu haheshimiki, hugandamizwa na
kunyonywa na wale waliofanya bidii katika maisha yao na kufanikiwa. Kwa kuwa
uvivu huleta umasikini, basi mvivu ni mtumwa kwa wale walifanikiwa au
kujibidisha katika kazi. Sanjali na kunyonywa, waliofanikiwa hufanya lolote kwa
waliowavivu. Mithali 12:24 “Mkono wa mwenye bidii utatawala; Bali mvivu atalipiswa kodi”
7.
Mtu mvivu ni
ombaomba; hali na kutumia vya jasho lake mwenyewe
Mvivu hawezi kujibidisha ili apate pesa,
vitu, au mali itokanayo na nguvu zake; bali yeye haishi kuomba kila kukicha. Kwa
kukosa fikra yakinifu za kujitambua pamoja na kujituma atika kutafuta na
kufanya kazi, mtu mwenyegonjwa la uvivu haishi kuombaomba kwa wale wenye
kuzitafuta pesa kwa nguvu zao. Mithali
12:27 “Mtu mvivu hapiki mawindo yake;
Bali mwenye bidii anamali za thamani”. Neno la Mungu pia linawaonya watu
wavivu wanaokula, kutumia na kuishi kwa kutegemea jasho la watu wengine. 2Wathesalonike 3:10, 12 “10Kwa kuwa hata ule wakati
tupokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi,
basi, asile chakula 12Basi twawagiza hao, na kuwaonya katika Bwana
Yesu Kristo, watende kazi kwa utulivi na kula chakula chao wenyewe”
8.
Maisha ya mtu mvivu
huwa ni magumu na ya shida sana
Mtu aliyeathirika na gonjwa la uvivu, kwake
siku zote maisha ni magumu na ya shida sana. Mvivu hawezi pata ahueni ya
maisha, kwa sababu yeye hana hasumba ya kujishughulisha katika kutafuta ili
afanikiwe; bali hutumia muda mwingi kwa mambo yasiyo ya msingi, sitarehe,
majungu, anasa, na kulala kwingi. “Njia
ya mtu mvivu ni kama boma la
miiba……..” (Mithali 15:19)
9.
Mtu mvivu hupenda
maisha rahisi, hapendi kujitesa katika bidii ya kutafuta
Mvivu hapendi kujisumbua, kujibidisha
katika kazi, wala kuteseka ili hapo baadae afanikiwe na kufaidi matunda yake;
bali yeye (mvivu) hupenda maisha rahisi yenye mteremko ili aseleleke hadi
mwisho. Maisha ya kupanda mlima kwa mvivu ni machungu mno tena ni zaidi ya
pilipili kichaa. Mithali 20:4 “Mtu mvivu kataki kulima wakati wa baridi; Hivyo
wakati wa mavuno ataomba, hana kitu”
10.
Mikono ya mtu mvivu
hufanya kazi kilegevulegevu
Muhubiri
10:18
“Kwa sababu ya uvivu paa hunepa; Na kwa
utepetevu wa mikono nyumba huvuja”. Kutokana na kukosa moyo au ari ya
kufanya kazi kwa bidii, mtu mvivu hufanya kazi kizembe tena kwa ulegevu na
utpetevu wa mikono. Mikono ya mtu asiyependa kazi ni milegevu na haitaki daima
kutenda kazi. Mithali 21:25 “Matakwa yake mtu mvivu humfisha, Kwa maana mikono yake hukataa kufanya kazi”.
11.
Mtu mvivu hawezi
kuthubutu, kuvumilia wala kuzikabili changamoto ili ayafikie mafanikio.
Binadamu mwenyegonjwa la uvivu ni mwoga,
anatawaliwa na mashaka, sio mvumilivu, hawezi kuthubutu wala kujitesa katika
kuzikabili changamoto, iwalau mwisho wa siku ayafikie malengo yake. Mvivu ni
mvivu hata katika kufikiria, hawezi kufanya kazi, biashara wala jambo lolote
bila kubebwa au kusaidiwa. Mvivu huzungukwa na mashaka, wasiwasi, pamoja na
uoga uliokithiri, hivyo hawezi kuthubutu kwenye kazi au jambo linalohitaji
ushupavu wa moyo, nguvu, akili na uwezo wa maarifa, pamoja na ustahimilivu
kubwa. Mithali 22:13 “Mtu mvivu husema, Simba yuko nje; Nitauawa
katika njia kuu”. (kwa jinsi hiyohiyo; Mithali
26:13, Sulema alizungumzia)
12. Mtu mvivu huharibu, hatunzi, hutumia kwa pupa na kwa
uharibifu vitu au mali zilizotafutwa na wengine.
Kutokana na kutojua uchungu, mateso,
usumbufu, gharama na jasho lililotoka katika kuvipata vitu au mali zilizotafutwa
na watu wengine; mtu mvivu azikutapo mali hizo au vitu hivyo yeye hutapanya,
hufuja, huharibu, hutumia kwa pupa na fujo vitu au mali hizo (zilizokwishatafutwa
na watu wengine tayali). Mithali 18:9
“Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake
ni ndugu yake aliye mharabu”. Mharabu ni mtu mharibifu.
13.
Mtu mvivu ni mzigo
na hunyonya wengine
Tabia ya uvivu, utegemezi, kuombeleza,
kudandiadandia vitu na mali za wengine; mtu mvivu huwa mzigo kwa marafiki,
jamii hata taifa kwa ujumla. Binadamu mwenye gonjwa la uvivu ni mzigo mkubwa na
mnyonyaji kwa wengine wale wanaojibidisha katika kuchapa kazi na kutafuta; wale
ambao usingizi, raha wala anasa kwao hazina thamani, maana kila siku, kila saa,
kila muda; nafsi zao, damu zao, fikra zao huwaza na kusema “Hapa Kazi Tu”. Neno la Mungu linaonya kuwa, tusiwe mizigo na
kunyonya wengine wanaojibidisha. 2Wathesalonoke
3:7-10 “ 7Mwajua wenyewe
jinsi iwapasavyo kutufuata; kwa sababu hatukuenda bila utaratibu kwenu; 8wala
hatukula chakula kwa mtu yeyote bure; bali kwa taratibu na masumbufu, usiku na
mchana tulitenda kazi, ili tusimlemee mtu wa kwenu awaye yote. 9Si
kwamba hatuna amri, makusudi tufanye nafsi zetu kuwa kielelezo kwenu, mtufuate. 10Kwa
kuwa hata ule wakati tupokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu
hataki kufanya kazi, basi, asile chakula”
14.
Mtu mvivu hupenda
kufuatilia mambo na mafankio ya wengine.
Mvivu asiyefanya kazi; masikio yake, macho
yake, miguu yake na mdomo wake huwa makini na shapu kufuatilia na kusema mambo
na mafanikio ya wengine (yasiyomhusu hata kidogo). Kutokana na kukosa kazi,
shughuli na mambo ya kufanya, mvivu hufuatilia ya watu wengine na kuyatapakaza
mtaani au kuyasambaza kwa watu wengine. Tabia hii ya mtu mvivu, huzaa tabia ya
umbea, usengenyaji na kuchunguza chunguza
maisha ya wengine au kutumia muda mwingi kwa kuzulula na kukaa vijiwezo kupiga
soga zisizokuwa na maana badala ya kufanya kazi. 2Wathesalonike 3:11 “Maana
twasikia kwamba wako watu kwenu waendao
bila utaratibu, hawana shughuli zao
wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine”
15.
Mtu mvivu hawajali
wala kuwahudumia na kuwatunza walio wa family yake
Kutoka na kuathiriwa na gonjwa la uvivu,
mtu mvivu hukwepa majukumu na hawezi kuwahudumia wala kuwatunza vyema wale
waliowafamilia yake kwa kiwango kinachotakiwa. Apate wapi pesa, mali, maarifa
mtu mvivu hadi aweze kuhudumi walio wa familia yake? Family inayomtegemea mtu
mvivu haina uhakika wa maisha ya kesho wala keshokutwa. Haikosi njaa, haina
akiba wala matunzo yanayokidhi. Paulo mtumishi wa Mungu anasema “Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake,
yaani wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko mtu
asiyeamini” 1Timotheo 58.
16.
Kazi, mali, na vitu
vya mtu mvivu havipo katika utaratibu, matunzo na mpangilio maalumu
Kila jambo, kila kazi, na kila kitu cha mtu
mvivu kipo ‘shaghalabaghala’; hakuna matunzo, hakuna mpangilio, hakuna utaratibu.
Hakuna kipi kianze wala kipi kifuatie baada ya kingine. Muda gani jambo au kitu
gani kifanyike na kifuatiwe na kitu gani kingine. Kazi ipi ifanyike vipi, muda gani na
kwa namna gani, ianzeje na imalizikeje, kitu gani kitunzwe na kihifadhiwe kwa
namna ipi? Muhubiri 10:18 “Kwa sababu ya uvivu paa hunepa; Na kwa
utepetevu wa mikono nyumba huvuja”. Mithali
24:30 “30Nalipita karibu
na shamba la mvivu, na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili. 31Kumbe!
Lote pia limemea miiba; Uso wake ulifunikwa kwa viwavi; Na ukuta wake wa mawe
umebomoka”
17.
Mvivu hapendi
wengine wafanikiwe, anataka wabaki kama alivyo yeye
Kushindwa kwake mvivu, hutamani na wengine
wafeli na washindwe kama alivyoshindwa yeye. Kwa maana nyingine; mvivu huwaonea
wivu wale wanaofanikiwa na hujenga kinyongo na chuki juu yao. Mathayo 25:18, 24-27 “18Lakini Yule aliyepokea moja
alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake. 24Akaja…..aliyepokea
talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna
usipopanda, wakusanya usipotawanya; 25basi nikaogopa, nikaenda
nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyoyako….”
18.
Kwa tabia ya uvivu,
mvivu hawezi akathaminika wala kuheshimika
Mara zote mvivu haheshimiki, kutokana na
matendo, mienenodo natabia zake zisizokuwa na uelekeo wala malengo. Tabia yake ya uvivu humpunguzia hadhi
ya kuheshimika, kwani kila Nyanja yeye huwa anafeli; kiuchumi, kibidii,
kimafanikio, kiubunifu na kimaarifa.
Mathayo 25:24, 30 “24Akaja…..aliyepokea
talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna
usipopanda, wakusanya usipotawanya;…. 30Na mtumwa yule asiyefaa,
mtupeni mbali katika giza la nje; …….
19.
Mvivu ni mvivu wa
kujifunza maarifa mapya ili aweze kubadirika
Kutokana na uvivu kumtawala; mtu mvivu ni
mvivu kujifunza maarifa mapya ili aweze kufanikiwa na kujikwamua kimaisha. Hata
kama atapatiwa elimu, ushauri na maarifa mapya anaweza kushindwa kutokana na
kuwa mvivu katika kusimamia, kutekeleza na kujibidisha kwa kile alichojifunza
au kushauliwa na wengine. Suleman alitoa ushauli kwa mvivu kuwa apashwa
kujifunza hata kwa wadudu aina ya chungu wafanyavyok kazi kwa bidii. Mithali 6:6-11 “6Ewe mvivu, mwendee chungu, zitafakari njia zake ukapate
hekima. 7Kwa maana yeye hana akida, wala msimamizi, wala mkuu, 8Lakini
hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa
mavuno”
20.
Mvivu anaugonjwa wa
kuahirisha ahirisha kazi na mambo yake
Tatizo la mtu mwenye gonjwa la uvivu ni
kuahirisha-ahirisha kutimiza, kutekeleza mambo na shughuli zake kwa wakati. Huu
ni ugonjwa au tatizo linaloitwa kwa kingereza “Procrastination”. Tatizo hili huwakabili wavivu na huchukua sehemu
kubwa ya maisha yao. Kuwaza na kusema “nitafanya
tu” ndiyo kauli mbiu ya mtu mvivu mwenye tabia ya kuahirisha-ahirisha
mambo/kazi/majukumu. Mithali 6:9-11.
21.
Mvivu hujipataia
pesa, vitu na mali kwa njia zisizo halali
Mtu mvivu hudhulumu, hutapeli, hukaba,
huiba, hunyang’anya vitu, mali, au pesa; hivyo njia azitumiazo hujipatia mali,
vitu, pesa; huwa sio halali. Mvivu aweza dhuru, ua, teka; ili mwisho wa yote
apate kitu, mali, pesa kwa njia hatarishi zilizo kinyume na talatibu. Matokeo
ya kutumia njia zisizofaa, ni kutokana na kutopenda kufanya kazi kwa bidii,
kupenda maisha ya mteremko, hahitaji kuteseka. Kwa tabia hizi, neon la Mungu
limeonya katika Waefeso 4:28.
Suluhisho
la kuondoa, moyo tabia ya uvivu kwa mtu mvivu
Uvivu hujengeka katika moyo, fikra na
mwili, kutokana na mtu mwenyewe alivyokuwa na kulelewa katika jamii au family
atokayo. Pia mfumo wa elimu yetu ya sasa (Tanzani) imejikita kuandaa au
inaandaa taifa la watu wavivu na tegemezi wasiopenda kufanya kazi ngumu,
kujiajili, kwa kupenda kazi nyepesi na rahisi na wanaobagua kazi za kufanya
maishani. Wanafunzi wawapo shuleni, kwa ngazi za shule ya msingi sekondari na
vyou, hawajengewi misingi ya kuzalisha pamoja na kujitegeme. Sijui kama na
magereza yetu yote yanawapatia ujuzi, maarifa na uwezo kujitegemea na kuzalisha
punde watokapo gerezani? Huko sijawahi kufika na siwezi kusemea.
Tanzania inaasilimia nyingi sana ya watu
wasiozalisha na asilimia ndogo ya watu wanaozalisha; mfano: ukichukua idadi ya
wato wenye miaka 1-14, wanafunzi wenye miaka 15-30 na wazee miaka 64+. Wengi
wao ni tegemezi na sio wazalishaji ndani ya taifa masikini. Mambo ya kuzingatia,
kufanya, kufuata na kujifunza kwa mtu mwenye gonjwa la uvivu ili kukomesha au kutibu ugonjwa au tabia ya
uvivu iliyokithiri:
1. Mvivu na ajitahidi
kuepuka uzembe; ajitahidi kuwa na moyo wa kufanya kazi kwa bidii (Mithali
6:6-10)
2. Mvivu ajenge mazoea
ya kufanya kazi kwa kujituma au kufanya kazi kwa bidii bidii (Mithali 3:27)
3. Mvivu ajitahidi
kutunza na kujali muda. Atambue kuwa muda ni mali na ukipotea haurudi
4. Mvivu ajitahidi
kuweka mambo yake katika mpangilio na ayatekeleze kulingana na mpangilio (Luka
14:25-35)
5. Afanye kazi halali
inayomwingizia mali, vitu au pesa halali
6. Asitumie njia
zisizo sahihi ili kufanikisha kujipatia mali au kipato (Wakolosai 3:25)
7. Yote afanye kwa
kumtumainia na kumtegemea Mungu sambamba na kujibidisha katika kufanya kazi
(Wakolosai 3:17)
8. Atambue faida,
hadhi na umuhimu wa kutumia vitu, mali na pesa alizo zitafuta kwa jasho lake;
ili kuepuka masimango (Waefeso 4:28)
9. Aache kupoteza
wakati na muda kwa kuzulula na kufanya mambo yasiyokuwa na tija wala faida juu
ya maisha yake maana kufanya kazi kunafaida (Mithali 14:23).
10. Ajue kufanya kazi
kwa kutumia akili na mikono yake, atabarikiwana Mungu()
11. Mvivu ajitume na ajitahidi
kupenda kazi maana katika kutenda kazi kwa ustadi kunaleta furaha (Mithali
8:30,31)
12. Atambue kufanya
kazi kunaleta matunda au faida maishani (Mithali 14:23)
13. Afanyaye kazi
hupata kitu cha kusaidia wengine walio wahitaji, hivyo atachuma mibaraka na
kujiwekea hazina mbinguni (Matendo 20:35), kwani anaposaidia huua tabia ya
uchoyo (Mithali 3:27)
14. Mvivu akubali
kutaabika ili kuyafikia mafanikio kutokana na kutenda kazi (Muhubiri 4:6)
15. Wakati mwingine
mvivu ajifunze kufanya kazi kwa mazoea, kwani kunawakati huja; yampasa afanye
kazi zaidi masaa au siku zote alivyozoea (Mathayo 5:41)
Faida
azipatazo mtu katika kufanya kazi, tofauti na mtu mvivu
Kumekuwepo na mitazamo na mawazo potofu kwa
watu wengi, hususani wale wavivu; wanadai kuwa kufanya kazi kwa bidii hasa kazi
zinazohitaji kutumia nguvu nyingi ni kazi za mateso kwao; hivyo kuitaji kazi
nyepesi na rahisi. Kazi ni kazi tu haijalishi kuwa unatumia nguvu, akili,
miguu, mikono au mwili mzima; bali zote ziaitwa kazi kwa namna yake. Hoja ya
msingi ni kufanya kazi kwa bidii na kujituma kwa moyo wote huku ukiipenda hiyo kazi.
Mtu yeyote afanyaye kazi kwa bidii anapata
faida zifuatazo katika maisha yake ya kila siku juu ya utendaji wa kazi yoyote:
1. Kufanya kazi ni
moja wapo ya kufanya mazoezi ili kujenga nakuulinda mwili usishambuliwe na
magonjwa ya kawaida
2. Hujenga moyo wa uvumilivu
na kujituma katika jambo lolote gumu
3. Mtu afanyaye kazi
kwa bidii; Mungu humbariki (tofautisha mibaraka na mafanikio)
4. Hujiepusha
kushiriki, na kuhusika katika mambo, makundi yasiyofaa
5. Kuonesha utii kwa
Mungu, kama alivyoamulu na kuelekeza tangu kwa Adamu
6. Kufanya kazi,
kunasaidia mwanadamu kujenga akili na uwezo kutafakari
7. Kufanya kazi kwa
bidii huongeza uzalishaji ndani tasisi au taifa
8. Kufanya kazi kwa
moyo na bidii, huleta maendeleo kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla.
Comments
Post a Comment
Thanks for viewing and passing through NMEE blog. Keep following the blog