MAMBO YA KUTAMBUA (‘A’ TO ‘Z’) KWA MCHUMBA ANAYETAKIWA KUWA Mwenzi wa maisha
MAMBO YA KUTAMBUA (‘A’ TO ‘Z’) KWA MCHUMBA ANAYETAKIWA KUWA Mwenzi wa maisha Kumekuwapo na changamoto nyingi sana za ndoa na hizo changamoto zimesababishwa na kufanya makosa kwa wanandoa katika suala zima la uchaguzi wa wenzi au wachumba wao katika hatua ya uchumba kabla ya ndoa kuja. Changamoto mojawapo katika ndoa imesababishwa na mitazamo tofauti na utashi binafsi wa watu katika kuingia kwenye ndoa. Kutofahamu umuhimu wa ndoa katika wanadamu kumepelekea kuvunjika kwa ndoa nyingi sana maana wengi wao wameoana kwa kuangalia vitu, kazi, mali, sura, kipaji, mvuto, umaarufu au chochote kutoka kwa mchumba kama kigezo cha kumvuta na kuiingia katika mahusiano ya uchumba ili kuifikia hatua ya ndoa. Ndoa (kama tasisi) ni takatifu, na Mungu aliruhusu ndoa kwa makusudi matakatifu. Ndoa ya kwanza iliasisiwa na Mungu mwenyewe katika bustani ya edeni kati ya Adamu na Hawa (mume mmoja na mke mmoja). Hivyo basi mchakato mzima wa kumpata mwenzi wa maisha kunahitaji kumshirikisha Mungu il