MAMBO YA KUTAMBUA (‘A’ TO ‘Z’) KWA MCHUMBA ANAYETAKIWA KUWA Mwenzi wa maisha
MAMBO
YA KUTAMBUA (‘A’ TO ‘Z’) KWA MCHUMBA ANAYETAKIWA KUWA Mwenzi
wa maisha
Kumekuwapo na changamoto nyingi sana za ndoa na hizo
changamoto zimesababishwa na kufanya makosa kwa wanandoa katika suala zima la
uchaguzi wa wenzi au wachumba wao katika hatua ya uchumba kabla ya ndoa kuja.
Changamoto mojawapo katika ndoa imesababishwa na mitazamo tofauti na utashi
binafsi wa watu katika kuingia kwenye ndoa. Kutofahamu umuhimu wa ndoa katika
wanadamu kumepelekea kuvunjika kwa ndoa nyingi sana maana wengi wao wameoana
kwa kuangalia vitu, kazi, mali, sura, kipaji, mvuto, umaarufu au chochote
kutoka kwa mchumba kama kigezo cha kumvuta na kuiingia katika mahusiano ya
uchumba ili kuifikia hatua ya ndoa.
Ndoa (kama tasisi) ni takatifu, na Mungu aliruhusu ndoa kwa
makusudi matakatifu. Ndoa ya kwanza iliasisiwa na Mungu mwenyewe katika bustani
ya edeni kati ya Adamu na Hawa (mume mmoja na mke mmoja). Hivyo basi mchakato
mzima wa kumpata mwenzi wa maisha kunahitaji kumshirikisha Mungu ili akupatie mtu
mwenzi wa maisha wa kufanana naye. Vijana wa kike na wa kiume wanaotegemea
kuingia katika ndoa wanatakiwa wajue kuwa, panahitajika umakini mkubwa sana ili
kumpata mchumba na mwenzi sahihi wa ndoa.
Hivyo; ni vyema kutambua cha kuzingatia kumpata mchumba
afaaye kuwa mke mwema. Mithali 2:11 inatuambia
kuwa “Busara
itakulinda; Ufahamu utakuhifadhi” hivyo na mimi naomba kuwapa elimu,
busara ufahamu ambao vijana wa kike na wa kiume utawahifadhi kwa kufuata hatua
zitakazokuwatia mchumba anayestahili kwa ajili ya ndoa njema na kuishi maisha
ya ndo kwa furaha:
‘A’
Azima ya kuingia kwenye ndoa uitambue
Azima
na nia ya kuingia kwenye ndoa yampasa mtu aitambue. Jambo la kuwa
katika ndoa halikwepeki, muda ukifika wakufanya hivyo yampasa mtu kuazimia kwa
dhati kabisa. Biblia inasema kwenye kitabu cha Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake na wakati kwa
kila kusudi chini ya mbingu”. Kunuia kwa mtu na kuwa tayali kutamwandaa kisaikolojia pamoja na
kujipanga kwa ajili ya azima hiyo. Kwa namna nyingine, kuingia kwenye ndoa sio
suala la kuigiza wala kujaribu, bali kunahitaji kunahita azima ya kuingia
kwenye ndoa.
‘B’
Bidii katika kazi
Mchumba anayefaa ni Yule
mwenye bidii katika kazi nasiyo alichonacho, mali alizonazo, kazi aliyonayo
mchumba. Mtu mwenye bidii katika kutafuta anauhakika wa kufanikiwa, hivyo
mchumba huangaliwa katika kufanya kazi kwa bidii na mipango thabiti kwa ajili
ya kuyatafuta mafanikio kwa nia halali. Mithali 10:4 na Mithali 12:27 mafungu
haya yamesadiki juu ya bidii katika kazi. Kulingana na mfumo wetu wa elimu
(miaka 16 na zaidi hutukika kwa ajili ya elimu toka chekechea hadi chuo kikuu)
kumpata kija aliyefanikiwa kuwa na funguo tatu yaani nyumba, ofisi na gari ni
nadra sana.
Hivyo kwa wale wanaotafuta
waenzi wenye funguo tatu hasa kwa kijana ya mpasa amtafute mtu mzee, mtu
aliyefiwa na mwenzi wake au kwa binti aingie katika ndoa ya mitala. Mchumba
mvivu na tepetevu na asiyejibidisha hafai kuwa mke au mume kwani dunia ya sasa
inahita kusaidiana katika kutafuta ili kuyafikia maendeleo mapema. Huu ni
ushauli wangu mwenyewe, maana uzoefu unaonesha madhara yake. Mfano baba ambaye
mtafutaji afarikipo au kupata ulemavu wa kudumu au gonjwa la kudumu, familia
huyumba na kusambarati. Hili jambo lipo hata kwa upande wa wanaume, maana wapo
wasiotafuta wala kujibidisha katika kutafut hivyo hulishwa na wanawake (ambapo
sio salama pia).
‘C’ Chunguza Tabia
Kipengele hiki ni nyeti
sana maana ndipo kiini cha mchumba anayefaa kuwa mke kinabeba mkitadha mzima wa
mchumba mwema atokaye kwa Mungu. katika tabia ndipo unaweza kupata wife
material (mke mwema). Wasifu wan je wa mtu kuutambua ni rahisi sana
kuliko wasifu wa mtu wa ndani; vivyohivyo tabia za ndani na tabia za nje kwa
mchumba. Ukikosea kuchunguza tabia ya mchumba katika kipindi cha urafiki, ni
ngumu kuzibaini gtabia katika uchumba maana atazificha ili kifikia lengo la
kuolewa au kuoa.
Tabia ni sawa na ngozi,
kuibadirisha ni vigumu sana. Usijipe moyo kwa kusema na kufikili “ngoja anioe
au nimuoe naye kasha nitambadirisha tabia yake”. Japo pia mwenye uwezo wa
kumbadirisha mtu tabia ni Mungu, hivyo itahitaji maombi mengi ya dhati kwa
kumuombea mchumba au mume/mke. Mafungu yaliyo katika Mithali 7:10-12, Mithali 11:16
na Mithali
12:4 yanaelezea juu ya tabia bainishi zinazofaa na zisizofaa kwa mtu
anayemwabudu na kumcha Mungu wa mbinguni. Kuna aina kuu mbili za tabia kama
ifuatazo:
1. Tabia zinazojipambanua
kwa nje: Tabia
za nje zinajipambanua katika matumizi ya ulimi katika kuongea, faasheni na aina za mavazi avaazo
mtu (Mwanzo 3:7, Kumb 22:5, 1pet 3:1-6,), kujipamba kwake kwa sura au mwi na manukato (Hosea 2:13, Wimbo 1:3,
Ezekiel 23:40), vyakula na vinywaji
apendeleavyo(Mithali 23:20-21). Tabia zote za nje kuzibaini hazihitaji muda
mrefu sana mfano uchafu au usafi wa mtu.
2. Tabia zinazojipanua kwa ndani: Tabia hizi hazionekani kwa urahisi
maana ni za ndani mno; mfano wa hizo ni wivu, upole, uchoyo, kutojali, dharau,
mtazamo. Warumi 3:12 imezungumzia tabia njema. Ugunduzi wa tabia hizi
juu ya mtu, kunahitaji kiawango na ujuzi mzuri wa saikoloji. Kubadilika kwa
tabia hizi za ndani kunahitajika uwezo wa Roho mtakatifu na utayali wa mtu baada
ya kugundua udhaifu na mapungufu yake.
‘D’ Dini/Dhehebu
Dini au dhehebu katika
mahusiano ni kipengele cha kuzingatia na kutilia maanani zaidi. Napendekeza
kuwa, wale wanaotalajia kuwa wenzi ni vyema pakawepo ufanano wa dini au
dhehebu. Kila dini na dhehebu panamafundisho yake (doctrines) ambayo
yanapishana kutoka dhehebu au dini moja kwenda dhehebu au dini nyingine. 1Wakorintho 1:10 na 1Wakorintho
1:12 aya hizi zinatoa umuhimu na faida za wanandoa kuwa wenye dini au
dhehebu moja, maana hawatapisha katika misingi ya mafundisho bila kuwagawanya
watoto katika imani za mafundisho. Ukitaka familia iwe chini ya kiwango katika
mambo ya kiroho, jaribu kuchanganya dini mbili tofaiti katika kuoana miongoni
mwa wanandoa.
‘E’ Elimu
Kunaelimmu ya kweli ambayo
inahusu uelewa na maarifa juu ya Mungu wa kweli wa mbinguni na elimu ya kidunia
ambayo tunaipata mashuleni kupitia masomo mbalimbali. Nitazungumzia juu ya
elimu ya kidunia ambayo inaweza ikaleta utofauti kwa wachumba watakapo kuwa
katika maisha ya ndoa. Nashauri wachumba wanaotarajia kuoana wasipishane sana
viwango vya elimu au walingane viwango vya elimu ili kuleta uwiano katika
mitazamo, uelewa na tafakari.
Sanjali na viwango vya
elimu kuwiana au kutotofautiana, kigezo cha elimu lazima kipewe nafasi ili kila
mmoja kati ya wachumba kuridhia wao kwa wao, endapo mmoja hajui kusoma wala
kuandika au hajaenda vidato katika elimu. Suala la elimu pia laweza kutatuliwa
kwa wenzi kukubaliana katika kuendelezana katika masuala ya elimu. Mafungu
yafuatayo yanaelezea juu ya elimu ya kweli na elimu dunia: Mithali 4:13, Waefeso 5:22 na
Esta 1:22.
‘F’ Familia atokayo (historia
yake)
Suala la ufahamu wa
historia na familia atokayo mchumba ni vyema kuifahamu bayana na kujiridhisha
kwayo. Kuifahamu familia atokayo mchumba ni jambo jema sana, kwani litasaidia
kujua endapo kunamagonjwa ya kurithi, malezi mabaya na tabia mbaya za wazazi au
walezi wa mchumba ama sivyo. Mara nyingi tabia ya wazazi/mzazi hubainisha tabia
ya mchumba hususani binti kama anavyoelezewa katika Ezekieli 16:44. Mafungu
mengine yanayoelezea juu ya umuhimu wa kuijua historia ya familia atokayo
mchumba Hosea 2:4-5 2Samweli 13:8-12. Yapo matendo yaliyofanywa na
wazazi na kupelekea matokeo yake kuendelea kuandama vizazi vinavyofuata (Kutoka
20:5).
‘G’
Gharama kwa mchumba
Kila jambo halikosi kuwa na
gharama aidha muda au pesa. Zipo gharama kwa mchumba, hivyo ni vyema (kijana wa
kiume) akazitambua ili kujua endapo atazimudu ama sivyo. Pamoja na gharama
nyigi; ipo gharama kubwa ambayo huwa inawakabili vija wa kiume ni lazima
aipitie ili kuifikia hatua ya kumuoa mchumba aliyempata. Ghara hiyo huhusisha mahali
pamoja na viambata vya zawadi na gharama mbalimbali (Mwanzo 24:48-53). Suala
la mahali linapisha tamaduni na tamaduni, sehemu na sehemu, imani moja kwenda
imani nyingine.
Kunawakati ghara hubebwa na
wazazi, na wakati mwinine kijana badala ya wazazi aweza kuzibeba mwenyewe.
Wakati mwingine gharama za mahali huwa ni kubwa mno, hivyo mchakato wa wachumba
kuoana hushindikana na ndoto za kuwa wezi hukwama kwa sababu ya gharama kubwa
iliyotajwa ili kumuuoa binti. Suala la mahali kuwa la gharama kubwa,
limesababisha madhara makubwa katika jamii nyingi. Mfano: vijana kuoana bila
kufuata taratibu, kkukatisha tama vijana kuoa au kuolewa hivyo kupata mimba na
watoto nje ya ndoa.
‘H’ Hiari ya Yule mchumba kuishi
naye
Upendo wa kweli hauhitaji
shuruti wala kulazimisha, bali upendo huandamana na hiari juu kuridhia toka
moyoni. Hivyo, mchumba ni vyema akakubali yeye mwenyewe ili kuingia ndani ya
ndoa. Uhuru katika kukubari hakuleti majuto hapo baadae ndani ya ndoa, maana
mtu amefanya maamu mwenyewe. Sio salama sana kutumia ushawishi wa kipesa, mali
au misaada yoyote ili kumtengenezea mazingira mchumba akubali kuolewa, kwa
sababu vitu au pesa vyaweza kuwa mvuto badala ya upendo kutoka moyoni. Rushwa
yenye ushawishi katika uchumba si jambo jema, maana hapo baadae kwa weza tokea
upungufu au ukosefu wa upendo wa dhati ndani ya ndoo. Kunajambo zuri la
kujifunza katika Mwanzo 24:54 ambapo Rebeka alihiali yeye mwenye kwenda kuunga
na mume wake baada ya kutolewa zawadi na mahali.
‘I’ Imani
Suala la imani ni jambo
nyeti sana sawa sawa na kile kipengele cha “D”
juu umuhimu wa wachumba kufana kwa dhehebu au dini kabla ya kuoana. Yapendeza
wachumba wanaotaka kuoana wawe wa imani moja, maana kutofautiana imani huzaa
migogoro katika ndoa. Zipo imani ambazo huruhusu kula vyakula vyote, kuoa na
kuacha (kutalakiana), kunywa pombe, kuoa wake wengi na kuvuta sigara, hivyo
mwingine akiwa na masharati katika hivyo vipengele, kutaleta migogoro mikubwa
ndani ya ndoa. Sambamba na hayo, hata taratibu za ibada kupisha kati ya imani
moja na nyingine kwa weza sababisha makwazo miongo mwa wanandoa
Sio
salama pia kutumia silaha ya kumtangazia mtu (mchumba) kuwa nitaolewa au
nitakuoa wewe endapo utabadiri imani yako na kuja kwenye imani yangu; kwa
sababu mchumba aweza kukubali kubadiri imani yake ili aolewe au kuoa kwa sababu
ya kukidhi hitaji lake na siyo kwa kuikiri imani. Kitabu cha 1 Wafalme 11:4 kinasema hivi:
“Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake,
afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA Mungu wake,
kama moyo wa Daudi baba yake.” Ni vyema
wachumba wanaotarajia kuoana wawaze mamoja, wanuie mamoja, watende mamoja,
waamini mamoja katika imani ili kuondoa mpasuko.
‘J’ Julisha wazizi
Uchumba wa Yusufu na Mariam
ulitambulika nyumbani kwao na jamii inayowazunguka. Wakati mwingine hata
urafiki utambulike kwa wazazi ili wazazi nao wapime uaminifu wa rafiki huyo kama
ilivyotoke kwa Musa (Kutoka 2:16-21). Wachumba wanaotalajia kuoana ni vyema
wakazijulisha pande zote mbili za wazi wao ili kuweka uwazi na kulinda uchumba
wao ili kuepuka kusalitiana kama ambavyo wangekuwa wawili kwa uchumba wa
kisiri. Huwa ni moja ya heshima kubwa sana kwa wazazi kujulishwa juu ya uchumba
wa binti au kijana wao endapo amefikisha umri wa kufanya hivyo ili nao wapate
ya kushauri au kutoa Baraka zao kwa ajili ya hatua zingine kuelekea katika
ndoa.
‘K’
Kasoro alizonazo mchumba zibaini mapema
Kubaini kasoro alizonazo mchumba ni vyema ni vizuri ili
kujipima kama zitaweza kuvumilika au kubailishwa kama ni za kufanyiwa
mabadiliko haraka kabla ya kuamua kuingia kwenye ndoa. Biblia inamzungumzia Lea
kasoro yake ya kuwa na makengeza lakini Yakobo alimkubali kwa kasoro (Mwanzo
29:17). Lea huyo huyo mwenye kasoro na asiyependwa alibarikiwa kupata
motto mapema kuliko Raheli. (Mwanzo 29:31). Yatupasa pia kujua
kuwa hakuna mtu ambaye hakosi kasoro asilimia mia, labda awe malaika.
‘L’ Linganisha umri wenu
Kipindi cha umri wa miaka 12-21
unapenda anasa na umri wa miaka 40 na kuendelea ni umri ambao watu hutunza pesa.
Umri wa miaka 18 hadi 25 kwa wanawake huwa umri wa mabadiriko makubwa ya
kimaumbile, na wengi wao hunenepeana kutoka umbo la awali kwa sababu ya
mabadiliko ya homoni na maumbile. Umri wa miaka 25 kuendele ndio umri sahihi wa
kutambua umbo la mwanamke maana atakuwa amepitia hatua zote za mabadiriko. Jambo
la msingi kutambua katika umri wanamke hukomaa kiakili mapema, kuliko wanamume;
lakini pia wanamke huchakaa mapema lakini hawazeeki mapema, bali wanaume
hawachakai mapema ila huzeeka mapema. Hivyo basi ni vyema mwanamke awe chini
kidogo ya umri wa mwanamume kutokana na kuchakaa au kukua kwao haraha.
Ulinganifu wa kiumri ni
mzuri ili kubaini umri sahihi wa kuzaa pamoja na kuweza kusimamia majukumu ya
kifamilia. Kiafya inashauliwa kuwa,
mwanamke asiendelee kuzaa afikishapo umri wa miaka 34 hadi 36, hivyo ili
mwanamke aweze kuzaa watoto watatu wenye kutofautiana miaka mitatu, akichelewa
sana aanze kuzaa akiwa na umri wa miaka 25 hadi 26 ili ukijumlisha miaka tisa
ya watoto watu atafikaka au kabla ya miaka 36. Si wote wanaowezakutendewa
miujiza kama Sara kuzaa katika umri wa uzee (Mwanzo 17:17). Suala la
umri kwa wanaume halina changamoto sana, bali sio vyema kulea watoto katika
umri uzee, hivyo angalau akichelewa sana miaka 32 na kurudi numa.
‘M’ Miliki alizonazo mchumba
zitambue
Panatakiwa ukweli na uwazi
kwa wachumba juu ya mali na miliki alizonazo mchumba kila mmoja kabla ya kuoana.
Kukosekana kwa uwazi wa miliki alizonazo mchumba kwa weza kusababisha
kukosekana kwa uaminifu endapo siku moja atabaini kuwa ulukuwa umemficha.
Kumficha mchumba juu ya miliki na mali hupelekea kuotea endapo mmoja atafariki
ghafla waka wawapo katika ndo. Uwazi wa miliki utawaweka huru wachumba wote
wanaotaka kuoana hapo baadae ili kurahisisha mipango ya maendeleo mapema.
Wakati mwingi mali alizonazo mchumba hujulikana bila hata kumuuliza mhusika,
kama ilivyo katika kisa cha kitabu cha Ruthu,
ambapo Ruthu alitambua mali za Boazi kwa kumuona katika usimamizi wa hiyo
miliki (Ruthu2:3-4).
‘N’ Ndoto zake mchumba za
maishani maishani
Kila mwanadamu aliyenahakili
timamu na mwenye uwezo wa kufikiria japo hata kido huwa hakosi kuwa na ndoto za
maisha anazotalajia kuzitimiza katika kipindi cha muda fulani katika maoisha
ysake. Ni vyema ndoto za wachumba zibainike kwa kila mmoja, ili waweze kuona
namna na jinsi yakuweza kuzitimiza aidha ndani ya ndoa au kabla ya ndoa. Endapo
ndoto ya mmojawapo miongoni mwa wachumba itahitajika kutimilizwa kwanza ndipo
suala la ndoa lifuate, itabidi mwingine aheshimu na kusubiria au kama itakuwa
ni vigumu kusubiri, basi huyo asiyeweza kusubiria amuache mchumba wake na awe
huru kutafuta mwingine aliyetayari kuingia katika ndoa.
NA MWL. FRANK PHILEMON
ITAENDELEA, SIKU NYINGINE
Thank you, welcome again
ReplyDeleteThank you, welcome again
ReplyDelete