HATARI KWA LAODIKIA
BY: MWL. FRANK PHILEMON. Fungu : Ufunuo 3:15-16 A. UTANGULIZI JUU YA LAODIKIA Laodikia ni mji ambao umetajwa katika maandiko matakatifu na umekuwepo kati ya mwaka 261BC na 253BC . Kama vile Kolosai na Hilapoli, mji huu ulikuwa katika bonde la rutuba upande wa mashariki mwa mji wa Efeso (Ufunuo 3:14). Baina ya Efeso na Laodikia, palikuwa na umbali takribani maili 40 hivi. Hapo awali mji wa Laodikia ulikuwa ukiitwa Diospolis baade Rhoas na hatimae Laodicea ambalo ni jina la mke wa mfalme Antiochus II wa Syria ambaye alihusika katika kuujenga mji huo. Mfalme Antiochus II aliuita mji huu jina la mke wake kama heshima ya pekee kwa mke wake aliyeitwa Laodice. Laodikia ulikuwa ni mji muhimu, uliokuwa na mwingiliano wa watu wengi na uliochangamka sana katika Asia Minor . Na ulikuwa kituo kikubwa cha biashara na huduma za kibenki, kwani mji huu ulikuwa katikati ya miji mingine. Mji wa Laodikia ulikuwa pia mashuhuri katika utengenezaji wa nguo zitokanazo