HATARI KWA LAODIKIA
BY: MWL. FRANK PHILEMON.
Fungu: Ufunuo 3:15-16
A. UTANGULIZI
JUU YA LAODIKIA
Laodikia ni
mji ambao umetajwa katika maandiko matakatifu na umekuwepo kati ya mwaka 261BC na 253BC. Kama vile Kolosai na Hilapoli, mji huu ulikuwa katika bonde
la rutuba upande wa mashariki mwa mji wa Efeso
(Ufunuo 3:14). Baina ya Efeso na Laodikia, palikuwa na umbali takribani maili
40 hivi.
Hapo awali mji wa Laodikia ulikuwa ukiitwa Diospolis baade Rhoas na hatimae Laodicea
ambalo ni jina la mke wa mfalme Antiochus
II wa Syria ambaye alihusika
katika kuujenga mji huo. Mfalme Antiochus II aliuita mji huu jina la
mke wake kama heshima ya pekee kwa mke wake aliyeitwa Laodice.
Laodikia ulikuwa ni mji muhimu, uliokuwa na mwingiliano wa watu wengi na uliochangamka sana katika Asia Minor. Na ulikuwa kituo kikubwa cha biashara na huduma za kibenki, kwani mji huu ulikuwa katikati ya miji mingine. Mji wa Laodikia ulikuwa pia mashuhuri katika utengenezaji wa nguo zitokanazo na nyuzi za mazao ya miti pamoja na manyoya ya kondoo.
Laodkia ulikuwa
imebobea katika masuala ya elimu ya tiba pamoja na utengenezaji wa dawa za
tiba; hivyo Laodikia ilikuwa ina shule kwa ajili ya kuandaa wajuzi na watalaamu
wa mambo ya tiba na dawa.
Mji wa Laodikia
ulikuja kuwa sehemu ya utawala wa Pargamo,
na mnamo mwaka 133BC ulitwaliwa na utawala wa Kirumi (Roman empire). Na Cicero
akiwa kama msemaji na gavana wa kirumi aliifanya Laodikia kuwa makazi makuu
ya jimbo alilokuwa akilitawala.
Wakazi wa
Laodikia walikuwa na jeuri na kiburi cha mali na utajili; mfano, mnamo mwaka wa 60 AD mji wa Laodikia ulipatwa na
janga la tetemeko la ardhi ambapo mji huu uliharibiwa vibaya; kwa sababu ya mali
na utajiri walionao wakazi wa mji huu walikataa msaada kutoka serikali ya Kirumi
iliyokuwa ikitawala ili kufanikisha kuujenga upya tena mji huo.
Mji wa Laodikia
ulikuwa na chemchemu ya maji moto mahali palipoitwa hierapelis mile 6 karibia na bonde la mto Lycus kwa upande wa kusini, ambapo pia maji yaliyokuwa yakitililika
yalijengelewa mifereji iliyofunikwa kwa mawe na maji hayo pia yalitoka kupitia
pipe zilizoegeshwa kwenye chanzo cha maji moto hayo.
Maji moto
yaliyokuwa yakitoka yalikuwa na kiasi kingi cha madini ya calcium hivyo mara nyingi pipe zilikuwa zikiziba. Aidha, bonde la mto Lycus na bonde la mto Kolosae kwa pamoja yalitumika kama njia
za usafiri wa majini.
Wakazi wa mji
wa Laodikia walikuwa na imani zao za kipagani. Kama ilivyokuwa kwa miji mingine.
Mji huu (Laodikia) ulijulikana kama The City of Zeus yaani mji wa baba wa miungu, wanadamu, watawala na
walinzi wa vyote. Baadae
Laodikia ulikuja ukawa mji mkubwa uliokaliwa na Wakristo baada ya kufikishiwa injili kipindi cha mitume wa Yesu (angalia Wakolosai 2:1, 4:15 na Ufunuo
1:11).
Wenyeji wa
Laodikia kwa jumla walifanikiwa kwa namna nyingi nao waliridhika na hali yao,
na tabia hiyo ya kuridhika na hali iliingia hata katika kanisa, hivyo
hawakuweza kuonesha kwamba Kristo ndiye anayeridhisha kabisa. Hawakutambua
kwamba Kristo peke yake angeweza kujenga tabia za kweli za kiroho maishani
mwao, hasa kwa kutubu dhambi zao na kutafuta msaada wake kwa unyenyekevu
(Ufunuo 3:15-22).
Ingawa Paulo
alikuwa mtu wa kwanza kupeleka injili Asia, hakuna fununu kwamba alitembelea
mji huo wakati wa safari zake kuu za kueneza injili kama tunavyosoma katika
Matendo ya Mitume (Wakolosai 2:1). Labda
kanisa la huko lilianzishwa wakati wa Paulo alipoishi Efeso kwa muda mrefu, yaani wakati wa safari yake
kuu ya tatu baada ya waamini wa Efeso kuipeleka injili kwa miji jirani na Efeso
(Matendo 19:8-10; Wakolosai4:12-130.
Paulo
alipoandika barua kwa kanisa la Kolosai, vilevile aliliandikia kanisa la Laodikia.
Alitaka makanisa hayo mawili yabadilishane barua zao, ili yote mawili yaweze
kusoma barua zote mbili (Wakolosai
4:16). Hivyo, barua ya Walaodikia haikuingizwa katika mkusanyo wa Maandiko
Matakatifu (imepotea).
Barua nyingine
kwa kanisa la Laodikia ilihifadhiwa. Barua hiyo iliandikwa karibu na mwisho wa
karne ya kwanza (Ufunuo3:14). Ni barua yenye ujumbe wa Kristo kwa kanisa nayo I
namaneno mengi ya kuonya na kukemea kanisa.
Kipindi cha
utawala wa Kirumi; Proconsular Asia lilikuwa ni jimbo,
ambapo mji wa Efeso ulikuwa mji mkuu
hapo awali (soma Matendo 2:9; 6:9; 16:6; 19:10, 22; 20:4, 16, 18 n.k) na baade Asia Minor ulikuja ukawa mji mkuu (soma
Matendo 19:26, 27; 21:27; 24:18;27:2). Jimbo la Proconsular Asia lilikuwa
na makanisa saba yaliyooneshwa katika unabii aliooneshwa Yohana (angalia Ufunuo1:11).
Viongozi (ambao
ni machifu) walikuwa ni wenye mali nyingi, na matajiri pia ambao walichaguliwa
kila mwaka ili kuongoza vikao, michezo, sherehe na shughuli mbalimbali za
kidini katika maeneo waliyosimamia. Biblia
inathibitisha kuwa; Miongoni mwa machifu au viongozi wengine walikuwa rafiki
zake Paulo (Matendo 19:31).
Kwa sasa eneo
la mji huu ni sehemu yenye jangwa linaloitwa “The Turks Eskhissar au Old
castle”. Asia minor ambapo ulikuwepo mji huu kwa sasa panaitwa Uturuki (yaani nchi ya
Uturuki).
Asia-minor
(Uturuki) inakumbukwa hadi leo hii kwa matukio makuu mawili:
(a) Palikuwa ni mahali ambapo serikali ya Rumi ilipatenga kuwa
makao makuu ya nchi za mashariki kulingana na hali hiyo pakaitwa Laodikia yaani hukumu.
(b) Ndipo pale agizo la maaskofu wote lilipotolewa mnamo mwaka 364AD juu ya badiliko la sabato
lililotolewa na Baraza la Laodikia.
B. UWASILISHAJI
WA HUBIRI JUU YA LAODIKIA
Laodikia ni
kanisa la mwisho katika mpangilio wa makanisa saba yaliyotajwa katika Ufunuo 1:11. Mpangilio wa haya makanisa saba unaakisi nyakati
katika unabii na utimilifu wake kama ifuatavyo:
1.
Kanisa la Efeso (33 – 100 AD)
(a) Ni kanisa safi, sawa na farasi mweupe
(b) Lilikuwa na upendo uliopoa (Ufunuo 2:4)
2.
Kanisa la Smirna (100 – 313 AD)
(a) Ni kanisa la mateso, sawa na farasi mwekundu (Ufunuo 2:10)
3.
Kanisa la Pergamo (313 – 538 AD)
(a) Ni kipindi ambacho mfalme Constantine anachanganya giza na
Nuru
(b) Ndipo kipindi ambacho ibada ya Jumapili ilianzishwa rasmi
(c) Kanisa lenye upagani, sawa na farasi mweusi (Ufunuo 2:14-15)
4.
Thiatira (538 – 1517 AD)
(a) Kanisa lenye mchanganyiko wa nuru na giza sawa na farasi wa
kijivu (Ufunuo 2:20)
5.
Sard (1517 – 1798 AD)
(a) Kanisa katika kipindi cha matengenezo (Ufunuo 3:2)
6.
Filadefia (1798 – 1844)
(a) Kanisa katika kipindi cha mapumziko ya mateso (baada ya
mateso kuisha)
(b) Kanisa linalotunza neno (Ufunuo 3:8)
7.
Laodikia (1844 – kuendelea)
(a) Kanisa la mwisho (Kanisa la
masalia)
(b) Waumini wake sio wakamilifu
(c) Kanisa la hukumu ya mwisho
(d) Kanisa vuguvugu (Ufunuo 3:15).
C. SIFA ZA
LAODIKIA NA HATARI KWA WASHIRIKI WAKE
Kanisa la
Ladikia halitaharibiwa kwa sababu siyo kamilifu (bali litatapikwa). Zifatazo
ni sifa za Kanisa la Mungu la Laodikia na hatima kwa mstakabali wa washiriki
wake:
1. Kufanana
na ulimwengu - Vuguvugu (Ufunuo
3:15 – 16)
2. Maombi
duni (Ezekieli 9:4)
3. Kutosoma
neno (Ufunuo 3:17)
4. Kuridhika
na hari mbovu za kiroho (Ufunuo
3:17; Isaya 55:1-2). Kuchanganya mambo ya kidunia na mambo ya kiroho na kuhifadhi
dhambi na kupuuzia mambo ya kiroho
5. Umasikini
wa maandiko (Ufunuo 3:17-18;
Marko 4:18-19)
6. Uchi wa
matendo yasiyotengenezwa (Ufunuo
3:17). Kupenda matendo maovu. Matengenezo duni ya kiroho, matendo na vyakula
7. Kanisa la
Laodikia na washiriki wake wamejikita katika kutafuta umaarufu wa mali – Bwana anatutaka tununue dhahabu safi itokayo kwake ili
tuwe matajiri wa mambo ya kimbingu.
8. Kanisa la
Laodikia na washiriki wake wamejikita katika kutafuta umaarufu wa mavazi ya
kidunia – Bwana anasema tununue
mavazi safi na meupe yatakayohifadhi uchi na aibu za matendo yetu.
9. Kanisa la
Laodikia na washiriki wake wamejikita katika kutafuta tiba za macho katika
mambo ya kidunia – lakini Yeye
Bwana anasema tununue kwake dawa ya kujipaka macho yetu ili tupate kuona mambo
ya kiroho. (Ufunuo 3:18)
10.
Bwana Yesu anatualika
tule naye chakula cha jioni (Ufunuo
3:19-20). Neno lililotumika hapa ni “Dine” au “sup” ni sawa na “Deipon” (mlowa jioni): ambapo katika Kigiriki
kuna milo mitatu: Akratisma
(Breakfast), Ariston (Lunch) na Deipon (dinner). na mlo wa msingi ni wa
jiosni
D. HITIMISHO
- WITO
Bwana huwarudi:
Ufunuo 3:19; Waebrania 12:6.
Neema iokoayo imefunuliwa:
Tito 2:11 – 15.
Comments
Post a Comment
Thanks for viewing and passing through NMEE blog. Keep following the blog