SOMO: MADHARA YA KUKATAA KUMTII MUNGU
FUNGU KUU: (Mwanzo
6:6-8). “BWANA akaghairi kwa kuwa
amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. BWANA akasema, nitamfutilia
mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na
kitaambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi kwamba nimewafanya. Lakini
Nuhu akapata neema machoni pa Bwana”
UTANGULIZI:
Katika
somo hili “Madhara ya kukataa Kumtii
Mungu” limehusisha kitabu kilicho andikwa na Musa hususani sura ya 3, sura
ya 4, sura ya 5, sura ya 6 na ile sura ya 7. Katika sura hizi kunamambo makubwa
ya kujifunza ili yatujenge katika safari yetu ya wokovu. Tutaona jinsi gani
anguko la mwanadamu linavyotokea kwa sababu tu ya kukataa kumtii Mungu pamoja
na madhara yake. Katika sura hizo zote; visa vyake vimefupishwa mno katika biblia,
hivyo wengi huwa wanashindwa kuelewa mambo mengi na yamsingi.
KIINI CHA SOMO:
1.
Dhambi iliingia duniani kwa sababu Adamu na Hawa hawakuweza kutii taratibu na
sheria za Mungu (Mwanzo 3:1-3). Ukisoma
kwa umakini katika Mwanzo 3:3 Hawa
alijua ni kosa kwa kuwa yeye na Adamu walikuwa wameonywa na kufundishwa madhara
yake, ndiyo maana Hawa ananukuu kauli ya Mungu anapojibishana na nyoka (Shetani)
….. Mungu
amesema “msiyale wala msiyaguse, msije mkafa” (Hawa ananukuu kauli ya
Mungu)
2. Shetani anamchanganyia
uongo na ukweli hawa ili kumpotosha na kumwaminisha kuwa maelelekezo ya Mungu
hakuyaelewa vizuri (Mwanzo 3: 4)
3. Shauku ya hawa ya
kujua maarifa (mema na mabaya) pamoja na kuutamani kutoka mchoni; Hawa
anachukua jukumu la kuchuma matunda katika ule mti wa ujuzi wa mema na mabaya,
kisha anakula na kumpelekea Adam mumewe. (Mwanzo
3:6)
4. Kwa makosa waliyotenda
Hawa na Adamu wanajificha uso wa Bwana (Mwazo
3:8) ili asiweze kuwaona.
5. Kutupiana lawama
kunaanza; Adamu anamtupia lawama Hawa, Hawa anamtupia lawama Nyoka (Mwanzo 3:12).
6. Mungu mwenye huruma
anapanga mpango wa wokovu katika anguko la mwanadamu (Mwanzo 3:15).
7. Kwa mala ya kwanza
mnyama anachinjwa ili kutengeneza nguo za ngozi kustili miili yao (Mwanzo 3:21).
8. Mungu anawafukuza Hawa
na Adamu kutoka nje ya Bustani ya Edeni ili kupusha kula tena matunda ya ujuzi
wa mema na mabaya ili asije kuishi milele katika dhambi (Mwanzo 3:22-24).
9. Watoto wawili
wanazaliwa ‘Kaini, Habili’ (Mwanzo 4:1).
Kaini mtoto wa kwanza (Mrithi wa haki
ipatikanayo kwa imani) na mkulima. Habili mtoto wa pili na mfugaji wa
kondoo. Katika biblia habili kama mtoto wa pili ametajwa tu kwa makusudi makuu
kama mfia dini.
10. Makundi mawili ya
ibada ya kweli na ya uongo yanajitokeza baina ya Kaini na Abili (Mwanzo 4:3-5).
11. Mungu anamuonya Kaini
kutokana na kukengeuka kwake (Mwanzo
4:6-7).
12. Kaini anamuua mdogo
wake Habili kwa sababu ya wivu wa kiibada (Mwanzo
4:8).
13. Kutomsikiliza Mungu,
Kaini banakuwa jeuli hata katika majibu yake (Mwanzo 4:9).
14. Mungu anampatia Kaini
laana kuwa mbali na uzao wa familia ya watakatifu (Mwanzo 4:10-16).
Ufanano wa kaini na
Habili na Kaini:
Wote
walifundishwa na wazazi wao jinsi ya utoaji wa sadaka katika ibada zao kwa
Mungu
Wote
walitengeneza madhabahu kwa ajili ya kutoa sadaka zao kwa Mungu
Wote
walisimama kama wafanya ibada mbele za Mungu wa Mbinguni.
Utofauti wa Kaini na
Habili:
Kaini
alikengeuka na kufanya matakwa yake badala ya yale ya Mungu katika ibada
Habili
alienenda katika taratibu na sheria za Mungu katika ibada na utoaji wa sadaka
Kaini
anawakilisha kanisa/mtu asiyefuata taratibu alizoziweka Mungu
Habili
anasimama kama kanisa au mtu ambaye ni mtiifu na mfuata taratibu na sheria za
Mungu
Fundisho kutoka kwa kaini
na Habili:
Habili
ni mfia dini
Mungu
haangalii matukio au matendo yako ya nyuma ili akuhesabie haki na kufuta makosa
ya hivi karibuni
Mungu
anaangalia katika utii wa kufuata taratibu na maagizo yake
Mungu
anapokea ibada zetu, endapo tutaenenda kwa utaratibu na utii juu yake
Dini,
madhehebu na watu watungao ibada zao wenyewe zisizompendeza Mungu, kwa Mungu
hazipokelewi
Kabla
ya kumwendea Mungu, yatupasa kujua kuwa ni kitu gani kitasababisha ibada zetu
zisipokelewe na Mungu
Tunapofanya
makosa katika ibada zetu na Mungu asitujibu haitupasi kushupaza shingo kama Kaini
hatimae tukapotea milele
Siku
zote yatupasa kujitahidi ili ibada zetu ziweze kupokelewa na Mungu.
Mtu
asiyetii juu ya sheria na maonyo; Mungu huongeza laana badala ya Baraka, hivyo
mkono wa Mungu huondoka juu yake.
KAZIO LA MAARIFA
Hawa na Adamu wanapoteza watoto wao wote
wawili; mmoja kuwa mtangatangaji na mwingine kwa kufa kifo. Hivyo hapakuwa na yeyote aliyemlithi wa haki
ipatikanayo kwa imani. Kumbuka hata Habeli kutajwa ni kwa sababu ya kuifia
dini.
Kaini alikuwa anamke toka mwanzo hata kabla ya kulaaniwa. Na kipindi hicho walioana ndugu (hivyo Kaini alikuwa ameoa dada yeke maana kwa kipindi hicho hapakuwa na jamii nyingine tofauti na jamii ya familia ya Hawa na Adamu).
Kaini alikuwa anamke toka mwanzo hata kabla ya kulaaniwa. Na kipindi hicho walioana ndugu (hivyo Kaini alikuwa ameoa dada yeke maana kwa kipindi hicho hapakuwa na jamii nyingine tofauti na jamii ya familia ya Hawa na Adamu).
Mtoto wa kwanza wa Kaini ni Henoko (Mwanza
4:17) Adamu naye alizaa watoto wengine tofauti ya wale wawili. Uzao wa kaini na
uzao wa Adamu ulitengeneza makundi mawili:
Uzao
au ukoo mtakatifu mrithi wake ni Sethi
Uzao
au ukoo wa wana wa wanadam mrithi wake ni Henoko
Kuna
Henoko pia kutoka ukoo mtakatifu tofauti na Yule mtoto wa Kaini (Mwanzo 5:18) na huyu alitwaliwa (Mwanzo 5:24). Henoko huyu kabla ya
kutwaliwa alimzaa Methusela aliyeishi miaka 969 (METHUSELAH “Muth” and “Shalach” = “His death shall bring judgment).
Methusela alimzaa Lameki na Lameki alimzaa Nuhu. Ikumbukwe
kuwa yupo pia Lameki upande wa ukoo wa kaini ambaye ni mwanzilishi wa kuoa mke
zaidi ya mmoja. (Mwanzo 4:19)
Mchangamano na mwingiliano kati ya wana wa
Mungu na wana wa wanadamu uliathiri sana mwenendo mzima wa ulimwengu na
kuongezeka maovu kwa kasi kubwa kwa pande zote. Kwa sehemu kubwa Mwanzo sura ya
sita (6) inazungumzia ongezeko la watu ulimwenguni kwa kipindi hicho. Mwingiliano
uliotokana na kuoleana kwa pande mbili hizo kulisababisha kuongezeka kwa maovu
na uovu kuongezeka sana.
Upande wa wana wa wanadamu palizaliwa watoto wengi bila mpangilio na
wengi wakiwa watoto wa kike. Pia upande huu palikuwa na kuoana katika umri mdogo
pamoja na uoanaji usiokuwa na mpangilio hasa kuoa wanawake wengi. Upande wa
wana wa wanadamu palizaliwa watoto waliokuwa wazuri mno wa sura, hivyo kuvutia na kupelekea watoto wa kiume kutoka
upande wa wana wa Mungu au ukoo mtakatifu kwenda kuoa mabinti kutoka upande wa
wana wa wanadamu (Mwanzo 6:1-2). Kuoleana
kwa pande hizo mbili, kulisababisha kuzaliwa kwa vizazi vyenye watu hodari
wenye sifa (za ajabu) na majitu au Manefili (Mwanzo 6:4)
Maovu
yalipo enea kutokana na kuingiliana kwa pande zote mbili, Mungu alipanga mpango
wa wokovu kwa wanadamu, na kwa kindi hicho Nuhu
ndiye aliyepata neema machoni pa Mungu (Mwanzo
6:5-8). Pia kutokana uovu ulipozidi katika dunia, Mungu alipunguza umri wa
wanadamu kuishi miaka mingi (Mwanzo 6:3)
Nuhu
alihubiri injili kwa miaka 120, hatimae gharika ikaja na wengi wao waliangamia
kwa kutotii ujumbe wa Mungu. kutokana na tukio la kuigharikisha dunia, watafiti
na wataalamu wengi wa masuala ya miamba na mafuta wanaamini kuwa huenda miaka
ya nyuma palitoke vifo vya viumbe hai vingi ndiyo maana kunakuwepo na mafuta,
gesi, makaa ya mawe na chokaa na kurejea jambo la gharika kutoka katika biblia.
NASAHA:
Wokovu
ni wa mtu binafsi wala sio wa kirafiki au kundi
Tusikilize
maonyo ya Mungu na tufanye toba za kweli
Mungu
katupa nafasi nyingine kama kipindi cha Nuhu ili tuokolewe
Tusifungiwe
mlango wa rehema kwa kukataa maonyo, wito na sauti ya Mungu
Wapo
waliokuwa karibu na Nuhu na Kumsaidia kutengeneza safina ili hali kumbe nao walikuwa
wasindikizaji (ndivyo hivyo kwetu sisi)
Dhambi
ya kaini ilipelekea ulimwengu kuangamizwa kwa gharika, vivyohivyo dhambi zetu
zaweza kupelekea wengine kuangamizwa katika ziwa la moto.
Kuoleana
na wana wa wanadamu kunapeleke kuzaa watoto wengi wasiokuwa imara katika imani
na kumjua Mungu vyema.
Tujitahidi kuwa na NEEMA Machoni pa MUUNGU. Mwanzo
6:6-8. “BWANA akaghairi kwa kuwa
amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. BWANA akasema, nitamfutilia
mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitaambaacho
na ndege wa angani; kwa maana naghairi kwamba nimewafanya. Lakini Nuhu akapata
neema machoni pa Bwana”
HITIMISHO:
Hatari ya kukataa kutii kwa wanadam, imesababisha
gharama kubwa sana kwa Mungu ili kuunusulu upotevu wa mwanadam. Mkakati wa
ukombozi kwa wanadamu anaubeba Yesu Kristo aliyemwana na Mwokozi wetu.
BWANA ATUTETE
Mwl. Frank Philemon
Comments
Post a Comment
Thanks for viewing and passing through NMEE blog. Keep following the blog