CHANGAMOTO KATIKA TASISI
FUNGU: Mwanzo 16:6; Naye Abram akamwambia Sarai, Tazama,
mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai
akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake.
1.0 UTANGULIZI:
Nawasalimu
katika jina la Bwana wetu Kristo; Bwana Yesu Asifiwe binti na wana za Mungu. kwanSomo
la leo linatoka katika kitabu cha Mwanzo 16:1-15, na Mwanzo
21:1-21. Mada itajikita katika tasisi iitwayo familia. Swali: Kwa nini familia iitwe tasisi? Tusome kwanza Mwanzo 16:1-15, na Mwanzo
21:1-21 kisha tuanze somo.
2.0. KIINI CHA SOMO:
Aya zote tulizosoma zinamhusu familia ya
Abram ambaye ni Ibrahimu pamoja na mkewe Sarai ambaye ni Sara. Familia ya
Ibrahimu na Sarai ilikuwa na mjakazi (mfanyakazi au dada wa kazi) aitwaye Hajiri mwenye asili ya Misiri.
Familia hii ya Abram na Sarai haikuwa na
mtoto, toka wameoana. Kadri miaka iliposonga, Serai akamshauri Abram mumewe
azae na kijakazi aitwaye Hajiri (Mwanzo 16:2-4). Hajiri alijifungua mtoto wa kiume aliyeitwa Ishimael
(Mwanzo 16:11).
Japo Sarai alimruhusu mumewe kuzaa na
kijakazi, matokeo hayo hakuyakubari. Baada ya Mungu kufanya agano na Ibrahimu,
Mungu alimpatia mbaraka wa mtoto kupitia kwa mkewe Sara (Mwanzo 21:1-3). Kuzaliwa kwa Isaka, Ibrahimu alikuwa na miaka 100
na Sara miaka 90.
Hivyo, baada ya Sara kuzaa, familia ikawa
na watoto wawili ambao ni Ishimaeli
kutoka tumbo la Hajiri (mjakazi) na Isaka
kutoka tumbo la Sara mke halali wa Ibrahimu. Watoto hawa ndio chanzo cha
mgogoro uliowatenganisha makazi baina ya Hajiri na Sara (Mwanzo 21:8-10),
ambapo Sara alifukuzwa pamoja na mwanae aitwaye Ishmaili.
Kupitia
familia ya Ibrahimu na Sara, kunamambo machache ya kujifunza:
1. Ibrahimu mfano wa mwanamume anayesikiliza
ushauli wenye tija kutoka kwa mkewe (Mwazo 16:2-3), mwenye kusimamia haki
(Mwanzo 16:6, 21:10-11).
2. Sara mfano wa mwanamke mwenye
kigeugeu, (Mwanzo 16:5); mwenye jeuri na asiye na subira (Mwanzo 21:8-10):
3.
Mara zote, Mungu hamuachi mtu anayeonewa
pasipo kutendewa haki (Mwanzo 16:6-15).
4. Mungu mwenye uweza wa kuwapa
watoto hata walio vikongwe (Mwanzo 17:15-17).
5. Ibrahimu kielelezo cha baba mwenye
familia anayefuata maelekezo ya Mungu nje ya utashi wake mwenye (Mwanzo
21:10-12).
6. Ibrahimu mfano wa baba mwenye
huruma katika familia (Mwanzo 21:14).
7.
Mungu husikia sauti ya yeyote anayemwita katika matatizo (Mwanzo
21:15-20).
8. Heshima ya mama wa familia hushuka
pale jukumu lake kwa mumewe linapochukuliwa na kijakazi (Mwanzo 16:4).
9. Uadui wa wazazi huhamia pia kwa
watoto kwani chuki hupandikizwa juu yao (Mwanzo 21:9).
10. Mama mwenye upendo hawezi
kuvumilia kumuona mtoto wake akifa huku akiona (Mwanzo 21:15-16).
3.0 HITIMISHO:
Hareluyaaaa!! Bwana awabariki
Comments
Post a Comment
Thanks for viewing and passing through NMEE blog. Keep following the blog