SOMO: UASI WA KANUNI YA KIROHO TUSIOUJUA:
FUNGU: WAEFESO
5:15-21 “15Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu
wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16mkiukomboa wakati kwa
maana zama hizi ni za uovu. 17Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali
mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya bwana. 18Tena msilewe Kwa mvinyo,
ambamo mnaufisadi; Bali mjazwe Roho; 19mkisemezana Kwa zaburi Na
tenzi na nyimo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na
kumshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana Yesu
Kristo; 21hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.
1.0 UTANGULIZI:
1.1.
Katika maisha yangu ya kiroho; Nahau zifuatazo zimenifunda:
1)
Kama hujui mahala unapoelekea uwapo
safarini, njia yoyote miongoni mwa nyingi itakuchagulia uelekeo na Kama hujishughulishi kujua
unakoelekea, njia haiwezi kukuchagulia uelekeo sahihi uutakao.
2) Eneo
lenye giza zaidi kuliko maeneo yote katika mshumaa lipo chini ya mshumaa.
3) Debe
lililo tupu ndilo lipigalo sana kele.
4) Maisha
yetu ya kiro ni sawa na kuendesha baiskeli, ili udumu kuwa na stamina yakupasa
uendelee kuendesha
5) Bahari
isiyo na dhoruba haiwezi kumfanya nahodha awe imara katika ujuzi na uzoefu.
6) Usipojifunza
yale usiyoyajua huwezi kujua usiyoyajua
7) Akili
ya binadamu inafananishwa na mwamvuli, hufanya kazi vyema pale inapofunguliwa.
8) Mpiganaji
mzuri si yule ajilindaye, bali ashambuliaye katika kujilinda
1.2.
Maelezo ya fungu, wimbo.
(a)
Mkatadha
mkuu wa fungu kwa mujibu wa somo la leo juu ya wakati (reje fungu kuu). Kwa kuwa Mtume Paulo alikuwa mhanga katika
kuupoteza muda wake huko mwanzo, hivyo anasisitiza sana juu ya kuukomboa
wakati katika wokovu wa mkristo: Wenye hekima huukomboa wakati kwa kutenda
mema, bali wajinga na wapumbavu hutenda maovu.
Wenye hekima walio na akili hutenga muda wao kwa
ajili ya kumtukuza Mungu hasa katika kuimba, kusemezana kwa zaburi, tenzi,
nyimbo za rohoni, kumshukuru Mungu, Kumshangilia Bwana Moyoni mwao na
kunyenyekeana wao kwa wao katika Kristo ili wajazwe Roho. Lakini waovu na wapumbavu
hulewa mvinyo (aidha mafundisho mapotofu), kufanya kila aina ya ufisadi.
(b)Wimbo
namba 71 katika vitabu vya nyimbo za Kristo (Kesheni Kaombeni-kwa kusoma beti zake) nao pia
umetuhimiza kutenga muda wa kutosha katika wa maisha yetu kwa ajili ya kushikamana
na Mungu katika kuomba.
2.0. KIINI CHA SOMO:
2.1.
Maelezo mafupi juu ya somo:
Mungu alianza na muda katika siku zake zote za uumbaji (Mwanzo 1:1-5) ili
kufanikisha uwekaji wa nyakati/majira kwa ajili kumuwekea kumbukumbu sahihi
minadamu hapo badae. Hivyo huwezi
ukatenganisha muda na uumbaji pamoja na ibada Zetu kwa kwa Mungu aliyetuumba.
Katika nuru yaani mwanga ambao
hufanya mchana pamoja na giza ambaao hufanya usiku hutupatia kujua kuhesabu
massa siku, juma, mwezi, mwaka na miaka. Au kwa sasa kutokana na teknologia
tunahesa wakati katika milsecond, sekunde, dakika, saa, siku, juma, mwezi,
mwaka, mlongo, karne na millennia.
Biblia ambamo limo neno lake Mungu,
limeandikwa kwa kuzingatia wakati aidha, jambo lilishatokea, limetimia,
litatokea. Hivyo Mungu kutupatia wakati alikuwa na makusudi makuu ya sisi
tuweze kuutunza muda kwa ajili ya kumwabudu na kumtukuza kwani sis ni mawakili
tu wa muda.
Swali
la kujiuliza: Je, sisi ni mawakili waaminifu wa muda wa
Mungu aliotupatia? Kushindwa kumpatia kipaumbele Mungu kwa kuhodhi muda
Wake kwa kufanya mambo yetu binafsi kinyume na ufanywaji wa wakati kama
yalivyokuwa makusudi yake ili kumwabudu na kumtumikia Yeye hatufanyi dhambi ya
kumwibia Mungu kama tunavyomwibia mali zake (yaani zaka na sadaka)?
2.2.
Muda katika mambo ya kiroho
Muda ni miongoni mwa aina sita za
uwakili. Muda unasehemu kubwa katika wokovu wetu, maana unaashiria mambo
yafuatayo:
a) Wakati
unaweka bayana Ukombozi wetu,
b) Wakati
unaonesha kikomo chetu cha rehema,
c) Wakati
unabainisha kutumika kwetu kwa Mungu,
d) Wakati
unapima ukomavu na ukuaji wetu kiroho,
e) Unatuelekeza
kutimiliza mpangilio wa maagizo ya Mungu,
f) Wakati
unatudhihirishia nini tufanye na kipi tusifanye,
g) Wakati
unatutanabaisha mambo yaliyopita katika histori yanayotufunza yaliyopo na
yajayo ili yatimie katika unabii,
h) Wakati
ni kumbukumbu kwenye hatima ya hukumu; maana kila jambo na kila tendo kwa
wakati ulipolitenda litaletwa hukumuni.
2.3.
Je, huwa unakuwa naye Bwana kila muda?:
Muda wako ni zawadi ya thamani sana ambayo
Mungu amekupatia kwa makusudi ya kumtumainia Yeye. Muda ni mali, muda
sio rafiki unapochelewa kutimiliza jambo, muda ni mstari hivyo kuwa nao
makini sana kwa ajili ya wokovu wko. Mkristo asiyetunza muda na
kuutumia vizuri katika kuweka uhusiano wake na Mungu avunja sheria kwani
anamwibia Mungu Muda wake. NB: Tasisi
za kidunia zimeweka watunza muda, je vipi sisi tusiojari na kutunza muda tupo
salama? (Kisa cha interview)
2.4.
Mpango wa Mungu kutupatia Muda wanadamu ni nini?
1. Tuwajibike
kwake yeye: Waefeso 5:16 “mkiukomboa wakati kwa maana zama hizi ni za
uovu”
2.
Tuyafuate maelekezo yake: Waefeso 5:8 “Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza,
bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru”
3.
Tupange ratiba kwa ajili yake yeye: Zaburi
55:16-17 “16Nami
nitamwita Mungu, Na Bwana ataniokoa; 17Jioni, asubuhi, na adhuhuri
nitalalama na kuugua, Naye atasikia sauti yangu”
4.
Tuwe katika utaratibu sahihi: Kutoka 40:1-16
“…...16Musa
akafanya hayo yote; kama yote Bwana aliyoagiza ndivyo alivyofanya”
5.
Tujikite katika hekima yake: Zaburi 90:12
“Basi utujulishe
kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima”
6.
Tuutafute ufalme: Mathew 25:34-35 “34Kisha Mfalme atawambia
wale walioko mkono wake wa kuume, Njooni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini
ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; 35kwa maana
nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa
mgeni, mkanikaribisha”
7.
Atuponye na maovu katika nyakati zote: Zaburi
31:15 “Nyakati
zangu zimo mikononi mwako; Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia”
8.
Kuwashuhudia na kuwahubiri wasio mjua:
Yohana 9:4 “Imetupasa
kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana; usiku waja asipoweza
mtu kufanya kazi”
8.
Tuyajue mazingira na hari yake: Mhubiri
3:1 “Kwa
kila jambo kuna majira yake, na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu” (waweza
soma hadi fungu la 8)
9.
Tukumbuke kuzishika amri zake: (Soma
mafungu yafuatayo; Kutoka 20:8-11,
Kutoka 20:12)
10.
Tuepuke kufikiwa na kikomo cha rehema: Mhubiri
12:1-2 “1Mkumbuke Mungu wako siku za ujana
wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala hazijakaribia miaka utakaposema,
Mimi sina furaha katika hiyo. 2Kabla jua, na nuru, na mwezi, Na
nyota, havijatiwa giza; ………”
2.5.
Tunapotezaje muda wa Mungu?
1. Kwa kufanya mambo maovu na uasi wa sheria: 1Yohana 3:4 “Kila atendaye dhambi, afanya uasi;
kwa kuwa dhambi ni uasi wa”
2.
Kwa kutumia muda mwingi kujiwekea hakiba duniani: Mathayo 6:19-21 “19Msijiwekee
hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; 20Bali
jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi
hawavunji wala hawaibi; 21Kwa kuwa hazina ilipo, ndipo utakapokuwapo
na moyo wako”
3.
Kutokufanya kazi yake Mungu: Mathew 28:19-20
“19Basi,
enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba,
na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20Na kuwafundisha kuyashika yote
niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata
ukamilifu wa hadari”.
4.
Kiburi cha uzima: Yakobo 4:13-14 “13Haya basi, ninyi
msemao, leo au kesho tutaingia katika mji furani na kukaa humo mwaka mzima, na
kufanya biashara na kupata faida; 14Walakini hamjui yatakayokuwako
kesho”
2.6.
Tutunze vipi muda wa Mungu?
1.
Tuyape kipa mbele yaliyo maagizo ya Mungu: Zaburi119:6
“Ndipo mimi
sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote”
2.
Muda wa ibada na huduma uwe kipambele: Isaya
55:6 “Mtafute
Bwana, Maadam anapatikana, Mwiteni, maadam yu karibu”
3.
Tumia muda wako wa starehe na burudani kwa ajili mambo ya kiroho: Luka 4:4 “Yesu
akamjibu, imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu”
4.
Andaa, tambua na fuata ratiba yako: Kutoka
34:21 “Utafanya
kazi siku sita, lakini katika siku ya saba utapumuzika; wakati wa kulima
mashamba, na wakati wa kuvuna pia, utapumzika”, Warumi 13:11 “Naam,
tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekisha kuwadia; kwa
maana sasa wokovu wetu u-karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini”
NOTE: Tumia fomula ya “D-O-I-T-N-O-W” Kwa lugha y Kiingereza na “GA-PA-E-TU-FA-FU-VI” kwa lugha ya Kiswahili unapona ratiba yako na
Mungu huitekelezi:
3.0 HITIMISHO:
Mtumishi
wa Mungu Daudi alijua makusudi ya Mungu kuweka muda: Zaburi
90:12 “Basi, utujulishe
kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima” na
Zaburi
39:4-5 “BWANA, unijulishe mwisho
wangu, na kiasi cha siku zangu ni kiasi zangu”.
Mungu
alipanga mpango wa wokovu, na wakati ulipotimia ikawa: Wagalatia
4:4 “Hata ulipowadia utimilifu wa
wakati, Mungu alimtuma mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezariwa chini ya
sheri, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana”.
Hivyo
tu baada ya dakika tano yesu kufa msalabani palikomeshwa: 1.Sadaka ya dhambi kwa ajili ya ondoleo la dhambi (Yesu alisimama badala yake), 2.Sadaka
ya upatano wa amani ikakoma (Yesu
akawa mbadala), 3.Pasaka ya Israel ikakoma (Meza
ya Bwana ikaanza), 4.Huduma ya upatanisho duniani ikakoma
(maana Huduma ya ukuhani duniani ilikoma;
Yesu akaendelea nayo huko mbinguni kama kuhani mkuu) 5.Ulimwengu ukawekwa pamoja
katika kukombolewa (Kutoka kwa
taifa la Israeli) 6. masabato na miandamo ya miezi ikakomeshwa
(Maana Tunaye roho Mtakatifu anayetukumbusha kutenda mema).
Hareluyaaaa!!
Comments
Post a Comment
Thanks for viewing and passing through NMEE blog. Keep following the blog