TAMTHILIYA YA KWELI



FungU: Ayubu 42:10 “Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Auyubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza”.

01: UTANGULIZI
Hapa duniani zipo tamthiliya lukuki zilizoandaliwa na wanadamu kwa njia za maigizo katika majukwaa ya sanaa; maandishi katika vitabu, majarida na magazeti; sauti katia redio na katika sinema.

Tamthilia hizo kwa sehemu kubwa zina sifa za kufanana kimuundo wake na zinatofautiana kimtindo (yaani namna ilivyowasilishwa tamthiliya hiyo). Muundo wa tamthiliya hizi unasifa kuu nne:
1.     Tamthiliya ya aina yoyote lazima iwe na majibishano (yaani daiolojia)
2.     Tamthiliya lazima iwe na wahusika (wahusika wakuu (aweza kuwa nguli), wahusika wadogo (bapa au mviringo), pamoja na mtoa maelezo au mfafanuzi (maranyingi huwa ni sauti).
3.     Tamthiliya lazima iwe katika muundo wa pembe tatu, japo si tamthiliya zote (yaani socretic plays): Mwanzo (maisha mazuri na kuibuka kwa mgogoro); Kilele cha mgogoro; Mshuko/hitimisho/suluhisho la mgogoro.
4.     Mzingira/mandhari inapofanyikia tamthiliya hiyo.

Leo naweletea tamthiliya ya kweli iliyowahi kutokea zama za kale huko mashariki ya kati. Tamthiliya hii ni ya kale, lakini haijawahi chuja ubora wake. Tamthiya hiyo imegusa na inaendelea kugusa maisha ya watu wengi ulimwenguni, hivyo ni tamthiliya bora kuliko tamthiliya za kidunia.

Hakika tamthiliya hii hua ni mpya kila siku, kwani hutoa uzoefu ktika imani na wokovu wetu. Katika tamthiliya hii pamebainishwa pande kuu mbili za pambano kuu. Pande kuu mbili hizi za pambano kuu ni: 1. Mungu (master), mwanadamu (stering) na 2. Shetani na mawakala zake (jambazi).

Mazingira/mandhari ya tamthiliya hii ni kutoka nchi ya Usi. Muundo wa tamthilia hii kwa sehemu kubwa ni dialojia na monolojia kwa sehemu ndogo. Mtindo wa tamthiliya hii ni masimulizi, kioo, methali na moja kwa moja. Hadhira ya tamthiliya hii viumbe wa mbinguni.

Wahusika katika tamthiliya hii ya kweli ninayokuletea siku hii ya leo ni: 1. Mungu (Master wa stering), 2. Ayubu (stering mwenyewe), 3. Shetani (jambazi), 4. mke wa Ayubu (hakutajwa jina), 5. Rafiki watatu wa Ayubu (Elifazi Mtemani, Bildadi mshuhi na Sofari Mnaamathi), 6. Elihu (kijana mwenye hekima), 7. Watoto wa Ayubu na 8. Wafanyakazi.

Mwandishi/msimulizi (fanani) wa tamthiliya hii ni Musa (akiwa katika nchi ya Midiani. Midiani ni miongoni mwa watoto wa mzee Ibrahimu. Midiani alizaliwa na mke wa Ibrahimu baada ya Sara kufariki (nyongeza ya maelezo).

Ombi:

02: KIINI CHA SOMO (MGAWANYO WA TAMTHILIYA HII)
Tamthiliya hii ya kitabu cha Ayubu inamgawanyo wa sehemu kuu tisa (9) kama zinavyojipambanua:

SEHEMU YA 01: MAISHA YA FURAHA
Ayubu 1:1-5

SEHEMU YA 02: MADA MEZANI SEHEMU YA KWANZA
Ayubu 1:6 - 12

SEHEMU YA 03: MASHAMBULIZI YA MALI NA WATOTO
Ayubu 1:13- 22

SEHEMU YA 04: MADA MEZANI SEHEMU YA PILI
Ayubu 2:1-6

SEHEMU YA 05: SHAMBULIO LA AFYA NA NDOA
Ayubu 2:7-10

SEHEMU YA 06: SHUTUMA ZA MARAFIKI – WAFARIJI
·        Ayubu 2:11 – 13 Siku saba za ukimya wa Ayubu
·        Ayubu 3:1 – 26 Ayubu aongea baada ya ukimya wa siku saba akiilani siku yake ya kuzaliwa.
§  Ayubu 4:1-5:27 Shutuma za Elifazi Mtemani kwa Ayubu. Ayubu 6:1-7:21 Majibu ya Ayubu kwa Elifazi Mtemani.
§  Ayubu 8:1-22 Shutuma za Bildadi Mshuhi kwa Ayubu. Ayubu 9:1-10:22 majibu ya Ayubu kwa Bildadi Mshuhi
§  Ayubu 11:1-20 Shutuma za Sofari Mnamaathi kwa Ayubu. Ayubu 12:1-14:22 majibu ya Ayubu kwa Sofari Mnamaathi.
§  Ayubu 15:1-35 shutuma za Elifazi Mtemani kwa ayubu. Ayubu 16:1-17:16 majibu ya Ayubu kwa Elifazi Mtemani.
§  Ayubu 18:1-21 Shutuma za Bildadi Mshuhi kwa Ayubu. Ayubu 19:1-29 Majibu ya Ayubu kwa Bildadi Mshuhi.
§  Ayubu 20:1-29 Shutuma za Sofari Mnamaathi kwa Ayubu. Ayubu 21:1-34 Majibu ya Ayubu mwa Sofari Mnamaathi.
§  Ayubu 22:1-30 Shutuma za Elifazi Mtemani kwa Ayubu. Ayubu 23:1-24:25 Majibu ya ayubu kwa Elifazi Mtemani.
§  Ayubu 25:1-14 Shutuma za Bildadi Mshuhi kwa Ayubu. Ayubu 26:1-31:40 Majibu ya Ayubu kwa Bildadi Mshuhi kwa Mithali ndefu.
·        Ayubu 32:1-3 Rafiki zake Ayubu walikosa hija bali walimhukumia Ayubu makosa.

SEHEMU YA 07: FARAJA KUTOKA KWA ELIHU KIJANA MDOGO
·        Ayubu 32:4-5 Kwa heshima Elihu aliwaacha wazee waongee yao kwanza.
·        Ayubu 32:6-37 Elihu alinena kwa kirefu tena kwa hekima

SEHEMU YA 08: MUNGU AKATOA JIBU
·        Ayubu 38:1-41:34 Mungu akanena kupitia upepo
·        Ayubu 42:1-6 Majibu ya Ayubu kwa Mungu

SEHEMU YA 09: MAISHA YA RAHA FURAHA NA USHINDI KWA AYUBU
·        Ayubu 42:7-9 Onyo la mungu kwa marafiki watatu wa Ayubu
·        Ayubu 42:10-17 Bwana akageuza uteka wa Ayubu na kumbarik mara dufu katika mali na kumpatia watoto saba (7) wa kiume na watatu (3) wa kike (waliokuwa wazuri).

03: KAZIO: FUNDISHO KATIKA TAMTHILIYA HII YA KWELI
1.     Jiandae kukabiliana na watu wa karibu yako wanaojifanya kukufahamu na kukubashiria hatima yako – wewe na Mungu pekee ndiye anayekufahamu ndani na nje.
2.     Kuwa makini na marafiki wanaofurahia anguko lako – muombe Mungu akuepushe nao.
3.     Si – kila mzee anafahamu na anahekima ya kimbingu, wengi wao ni umri tu na mvi.
4.     Usimkufuru Mungu kwa sababu ya shurutisho la mke, mume ndugu na marafiki juu ya tamthiliya yako ya maisha unayoipitia – simama imara na Mungu wako katika hari zote.
5.     Chochote kibaya, kigumu kinapotokea juu yako amini Bwana anafahamu, mwiite na atakupa njia ya kutokea.
6.     Waombee memea maadui zako, kasha Bwana atageuza uteka wako na kukubariki zaidi.
7.     Katika changamoto zetu za kiimani katika dunia hii, tuamini kuwa lipo tumaini na furaha ya milele pale Bwana atakapotukubali kuwa wake.
8.     Shetani atatuchakaza kwa namna yoyote, ila Bwana atatufanya kuwa wapya na kutuongezea nguvu kama tai.
9.     Tambua kuwa shetani na mawakala zake hapendi kuona furaha, amani, upendo na mshikamano wa wacha Mungu ukitamalaki.
10.            Mungu huruhusu mambo furani yatokee juu yetu ili ajidhihirishe ukuu wetu.
 
03: HITIMISHO: WITO
Mjoli wa Bwana yawezakuwa ipo tamthiliya katika pambano kuu la maisha yako, na upo katika giza nene la kukata tamaa. Amini kuwa Mungu yupo upande wako kama ukiamua kumtegemea na kumkabidhi tamthiliya hiyo, maana Yeye amesema kuwa: 
1.      Wafilipi 4:6: Msijisumbue kwa lolote.
2.      Kumbu 31:8: Naye Bwana, Yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike.
3.      Isaya 41:10: Usiogope, kwa maana Mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana Mimi ni Mungu wako; Nitakutia nguvu, naam, Nitakusaidia, naam, Nitakushika kwa
4.      mkono wa kuume wa Haki Yangu.

Mungu akutie nguvu muhusika mwenza katika tamthiliya ya pambano kuu. Amina!

Comments

Popular posts from this blog

MAJINA YA WANAWAKE KATIKA BIBLIA ‘A’ HADI ‘Z’

MFANO WA MPANGO KAZI

SOMO: MADHARA YA KUKATAA KUMTII MUNGU