NGUVU YA MSAMAHA
Katika injili ya Marko 11:25-26 kusameheana kumesisitizwa kama ifuatavyo: 25 ”Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili Baba yenu aliyembinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. 26” Lakini kama ninyi hamsamehi, wala Baba yenu aliye Mbinguni hatawasemehe ninyi makosa yenu” Kwa Nini ni Muhimu Kusamehe? Zipo sababu nyingi za kusamehe, zifuatazo ni miongoni mwazo: 1. Kusamehe ni tabia ya Mungu, na wamchao: Mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu ( Mwanzo 1:26 ). Mwanadamu amchae Mungu kwa kweli yote, lazima awe na tabia ya Mungu kwa maana Mungu ni kielelezo cha kwanza cha kusamehe kwa mwanadamu ( Isaya 43:25. Isaya 1:18, 1Yohana 1:9). 2. Kusamehe ni hali ya Upendo: Kama tunda la roho ni upendo vivyo hivyo kusamehe ni tunda la upendo ( 1Wakorintho 13:4-7 ) . Tabia ya mtu amchae Mungu ni upendo kwa wengine hata kama atakwazwa. Mungu ni pendo, hata mwanadamu pia yampasa awe na upendo utokanao na Mungu. Kusamehe ni ishara na kielelezo