MAISHA NA TABIA YA TAI CHACHU NA SOMO KWA MAISHA KWA MWANADAMU
Utangulizi
Kila
kiumbe kilichopo duniani hapa cha weza kuwa fundisho zuri au baya katika maisha
yetu kulingana na jinsi kilivyotumika katika lugha ya picha. Wanyama kama
Sungura na Tumbili; ni wanyama wanaowakiliaha wanadamu wenye tabia za
ujanjaujanja au wajuaji sana. Simba anasimama kwa niaba ya watu nguli, wababe
na wakali wenye uwezo na mamlaka. Fisi anasimama kwa niaba ya watu warafi.
Twiga kwa watu wenye malingo na mikogo. Njiwa anasima kwa niaba ya utaktaifu,
upendo, uaminifu na upole kwa watu. Nyoka anasimama kwa niaba ya watu wenye
tabia ya uongo; wachonganishi. Ndege aina ya kasuku kusimama kwa watu wenye
kuongea sana.
Wasifu
au Sifa Na Tabia Za Tai
Wanyama
na viumbe mbalimbali wanapotumiwa katika lugha ya picha hutoa na huashiria
tabia na mienendo ya maisha ya kila mwanadamu. Kwa sehemu kubwa nitazungumzia
katika ‘wasifu na mwisha ya ndege Tai’ kama
chachu na somo kwa mwanadau. Ndege tai yupo katika aina au makundi yanayozidi
55. Katika kufuatilia taarifa na mandiko mbalimbali, nilibaini kuwa; Tai ana
wasifu ufuatao ambapo baadhi yake tutajifunza na kupata masomo mengi katika
maisha yetu hapa duniani:
1)
Tai anaurefu unaofika nchi 30(vertical
height) anapokua amesimama.
2)
Tai anaidadi ya manyoya kati ya 7200
kwnye mwili wake
3)
Tai anamwendo kasi mkubwa sana kuliko
ndege wote (48 hadi 89 kwa saa).
4)
Akiwa ametanua mabawa, tai ana urefu
(horizontal height) wa sentimita kati ya 200 hadi 243; saw na futi 6 had 7.9.
5)
Uwezo wa tai wa kuona mbali ni mara tatu
hadi nne ya uwezo wa mwanadamu
6)
Tai hupunguza joto kwa kutanua mbawa
zake pale anapokuwa angani
7)
Tai anamisuri takribani 175; miguu pekee
inamisuli 35. Kwa asilimia 40 hadi 60 ya uzito wa tai, umechangiwa na misuli
iliyopo katika mwili wake.
8)
Tai anauwezo wa kubeba windo lenye uzito
wa kilogram 5 hadi 7 au zaidi kwenda angsani
9)
Anauwezo wa kufika umbali zaidi ya futi
10, 000 kwenda angani
10)
Tai wanaoishi kwenye sehemu za maji,
wanauwezo wa kuogelea vizuri juu ya maji
Kutokana na uwezo na
sifa njema za wasifu wa tai; nchi baadhi na tasisi nyingi zinatumia picha ya
tai kama alama na kielelezo pekee cha uimala, uwezo, ubora na uthabiti. Taifa
la marekani ni miongoni mwa taifa linalotumia nembo ya tai. Sifa au tabia
bainishi za tai ndizo ambazo ni fundisho jema kwa maisha ya mwanadamu;
zimpasazo kuzijua, kuzitambua na kujifunza kwazo kama ifuatavyo:
1.
Tai anauwezo mkuba wa kuona mbali zaidi
2.
Tai anapaa umbali mrefu kwenda juu kuliko ndege wengine
3.
Tai haogopi dhoruba awapo juu angani
(hufurahia dhoruba)
4.
Tai ni mwepesi sana na anaspidi kubwa
5.
Tai hapendelei kula mizoga
6.
Tai hujenga ndoa yenye upendo na
yenyekuaminiana
7.
Tai hulea na kufundisha watoto katika
jujiamina na kuvumilia
8.
Tai anauhakika wa kuishi kwa muda mrefu
9.
Tai ananguvu na bidii
10.
Tai ni mbunifu katika kupambana na adui
zake
SURA
YA KWANZA
UWEZO
WA KUONA MBALI
Kiwawaida
tai anafika umbali mrefu zaidi kuliko ndege wengine. Tai anafika umbali zaidi
ya duti 10, 000 kutoka kwenye uso wa dunia. Japokuwa anakuwa umbali mkubwa sana
kutoka uso wa dunia, lakini tai anauwezo mkuba wa kuona hadi ndani ya maji yam
to au bahari pamoja na kwenye vichaka au nyasi. Kuona kwa tai hata awapo mbali
sana angani juu; humfanya ajue na atambue wapi kitoweo kilipo na wapi kuna
adui. Hivyo tai hujua na huona kabla ya adui au kitoweo kubaini kwa sababu tai
huwa mbali sana. Uwezo wake tai wa kuona mbali humpelekea yeye khuona kwanza
kabla yeye hajaonwa.
Fudisho Tulipatalo
Katika maisha yetu:
Mwanadamu
yampasa awe na uwezo wa kuona mbali pale ambapo wengine hawajapaona bado. Kuona kwanza ambapo wengine hawajapaona ni
lazima kuwa na njozi au ndoto inayolenga mbali kwa kuyafikia malengo ya badae.
Kuona mbali hakuji bila kuwa na mikakati kuweza kuifikia ndoto yako. Binadamu
yeyote mwenye kuhitaji kuyafikia yale ayatarajiayo; yampasa kupanga mikakati
(mission) ya kufanya njozi/ndoto (vision) yake itimie, sawa na tai aonapo
kitoweo toka juu mbali na hupanga mikakati ya kukifikia kitoweo hicho ili
atomize haja au adhima ya njaa yake.
Hivyo, mwanadamu asiye
kuwa na mikakati ili atomize ndoto yake atakuwa anaishi maisha ya kubahatisha
au kwa kufanya yale ambayo wengine wanafanya kwa jinsi ileile (atakuwa hajaona
mbali). Kila mtu yampasa awe na njozi maishani mwake na ajitahidi sana kuifanya
njozi hiyo itimie. Kuona mambo mapya ni kubuni mambo mapya ambayo hajafanyika
bado. Kutokuwa mbunifu ili kuifikia njozi kunamnyima mtu mafanikio, kwa sababu
hajalenga mbali. Tuwe na njozi ili
tuzifikie fursa katika maendeleo ya maisha na taifa letu juu ya misingi ya
wakati na sayansi na teknolojia.
Haijalishi tupo mbali
kiasi gani katika umri, elimu, au maendeleo; twaweza kuona katika njozi na kufanya mikakati na kuyafikia
malengo yetu kwa jinsi na namna yoyote. Umbali wa aina yoyote sio sababu ya
kutukatisha tama. Fanya kama tai kupanga kukifikia kitoweo ukitarajiacho
kukifikia. Kukifikia kitoweo hicho yakupasa uwe na njozi, mikakati, malengo,
ujuzi, ufaham, uelewa, mtazamo chanya na bidii katika kutenda kazi. Kamwe
tusiwaze kushindwa, maana kupanga kushindwa ni kupanga kushinwa kuyafikia
malengo yaliyo katika njozi na ndoto yako.
SURA
YA PILI
UWEZO
WA KWENDA MBALI KULIKO WENGINE
Urefu
na ubali awapo tai, huwezi kuona aina nyingine ya ndege. Zaidi ya futi 10, 000
kwenda juu angani kutoka kwenye uso wa dunia ni urefu mkubwa sana ambapo ndege
wengine hawawezi kuumudu kulingana na changamoto za misukosuko, upepo mkali,
mvua, baridi kali sana, kukokasa uwezo wa kuona chini, maana ni juu sana. Kwa
hiyo maisha ya tai ni ya kusitajabisha sana, kwani yeye huwa juu zaidi ya ndege
wengine wote. Lakini hata awapo juu zaidi hapotezi uwezo wake wa kuona mbali.
Fudisho Tulipatalo
Katika maisha yetu:
Kuna
msemo unasema kuwa “ndege wenye tabia na manyoya ya rangi ya aina moja hupaa
pamoja”. Ukanda wa juu alipo tai huwezi kukutana na ndege wengine zaidi ya tai
pekee. Kwa mtu aliyemakini lazima afanye, afikiri na atende zaidi ya pale
wengine walipofikia. Kufuata mkumbo na kuiga mienendo, tabia, jinsi ya kutenda,
kufikiri na kuiga maisha ya watu wengi, hakuwezi kukuletea tofauti yoyote zaidi
ya kuishi kwa mkumbo. Jua kuwa kila mtu
ni wa pekee kwa jinsi ya ajabu alivyoumbwa. Kuepuka mkumbo na kunakili maisha
na mienendo yaw engine; yatupasa kuwa tofauti au zaidi ya wawazavyo, waishivyo,
wafikiriavyo na watendavyo. Kama tai jinzi walivyo wa pekee katika ndege
wengine; na sisi tuwe wa pekee kwa kila namna.
Kama alivyo tai katika kuumbwa na Mungu; pia
binadamu anamjumuiko wa maajabu na vipawa na vipaji vingi ambapo Mungu kampatia
kwa jinsi ya ajabu na kustaajabisha. Binadamu yeyote akitulia vyema katika
kufikiri, anaweza kufanya mambo makubwa katika maisha yake endapo atakubali
kutumia uwezo mkubwa na vipaji alivyopewa na Mungu. Mungu kampa mwanadamu akili
na uwezo mkubwa kuliko viumbe vyote alivyoviumba. Kutojitambua kwa mwanadamu
ndicho kikwazo kikubwa cha kutokuwa na upekee.
SURA
YA TATU
KUTOOGOPA
DHORUBA NA CHANGAMOTI
Kutoogopa
kwa tai juu ya dhoruba awapo juu angani ni mojawa ya sifa ya pekee kuzipenda na
kuzimudu changamoto . Zipo changamoto nyigi anazokutana nazo tai pale awapo juu
angani. Mfano wa dholuba au changamoto hizo ni; mvua, baridi, ngulumo, radi na
upepo mkali. Nyakati mbaya za dholuba
yeye tai husherekea, hufurahi na wakati huu hutulia na hutandaza mbawa zake
bila wasiwasi. Wakati tai ufurahiapo dholuba au changamoto, ndege wengine
hukimbia ili kujiokoa.
Fudisho Tulipatalo
Katika maisha yetu:
Wanadamu
wengi mara zote tumekuwa tukipatwa na hofu, mashaka, wasiwasi wkutwapo na jambo
gumu na zito (changamoto). Mtu mwenyekuziogopa changamoto hawezi kuwa na uwezo
wa kuthubutu hata kidogo, maana maisha yake yamejaa mashaka na hofu. Woga ni
adui mkubwa wa mafanikio ya binadamu. Kama pangelikuwa na watu wengi
wanaothubutu kuzikabili changamoto bila kukata tama ndani ya nchi
zinazoendelea, umasikini ungelitoweka katika nchi hizo.
Wakati wa changamoto,
ndilo wakati wa kufikiria na kupumzisha akili ili kupata jambo jipya na mbadala
au mwarobaini wa kutatua changamoto zinazokukabili. Hofu, woga na kutojiamini
wakati wa matatizo au changamoto zozote humkwamisha mwanadamu kupiga hatua.
Kuna msemo unasema kuwa “Uoga wako ndiyo umaskini wako”. Tabia ya uoga hujenga
hofu na tabia ya kutojiamini. Kutojiamini ndiko kunakoleta hofu ya
kutokuthubutu.Godbless Lema (Mbunge Arusha mjini) yeye husema “uoga ni dhambi”
Endapo maisha yetu
yakitawaliwa na hofu, hatuwezi kufanya wala kupiga hatua katika jambo lolotete.
Uoga kwa mwanadamu humsababishia; hofu, mashaka, kukosa imani, kutojiamini na
kitete katika kulikabili jambo fulani au
kutenda kitu. Uoga ulikithiri huzaa magonjwa ya mpoyo na kifikra. Msingi wa
kujiamini kwa mwanadamu hunzia katika malezi ya mtu toka utotoni, na sio vinginevyo.
Tuwalee watoto wetu katika kusimamia na kujiamini kwa kile kinacho wakabili kwa
muda.
SURA
YA NNE
TUWE
WEPESI NA SHAPU KATIKA KUTENDA
Tai
ni mwepesi, shapu katika utendaji na wmenye kasi kubwa katika kuendea jambo
fulani. Tai hupaa kwa mwendo wa kasi wa maili 30 hadi 55 kwa saa, sipidi
anayorudia aridhini (diving speed) ni maili 100 kwa saa, ambayo ni sipidi isiyo
ya kawaida. Ushapu na kasi kubwa, ni sifa inayomtabanaisha tai kuwa tofauti na
ndege wengine. Wepesi na ushapu wa tai hutokana na kufikiria kwa kasi, maana
kufikili kunaanza kabla ya kutenda. Tai anauwezo wa kukamata nyoka au samaki,
ashukapo kwa kasi toka angani juu, hivyo nyoka au samaki hushindwa kujiokoa kwa
sababu ya ukasi na ushapu wa maamuzi ya tai tofauti na samaki au nyoka. Sio kwa
samaki tu au nyoka pekee, hata vitoweo (viumbe) vingine hukamatwa kwa jinsi
hiyohiyo.
Fudisho Tulipatalo
Katika maisha yetu:
Mara
zote mtu asiyekuwashapu katika kufikilia, hawezi kufanya maamuzi ya ghafla na
haraka. Uwezo wa kufikiri huendesha maamzi na kutenda; hivyo, wale wanaofikiria
polepole huchelewa kutoa maamuzi na hata utendaji wao wa kazi huwa wa polepole
sana. Kutembea na kutenda hutegemeana na ushapu wa mtu katika kufukiria.
Jambo lolote lampasa
mwanadamu kufanya hima na kwa ushapu au kasi ili kulikabili na kulikamilisha
kwa wakati muafaka. Haina haja ya kuchelewa, maana wakati hausubiri na hautoshi
daima. Lipaswalo kukamilika leo lisingoje kesho kwani muda sio rafiki, na hiyo
kesho haijulikani itakuwaje. Kukosa ushapu na umakini wa kutoa maamuzi ya
haraka, hupelekea kutofanikisha jambo kwa muda mahususi. Katika kazi na
biashara; ushapu na wepesi ndio utakaomwezesha mfanya kazi au mfanya biasha
ahudumie wateja wengi au kufanya kazi nyingi ili kuokoa muda na kuwahisha
huduma.
SURA
YA TANO
TUWE
WATAFUTAJI ILI TUSILE MIZOGA
Tai
hali mizoga bali hula kipaya (yaani freshi). Sifa na tabia mojawapo nyingie ya
tai ni kutokula mizoga (vimudu). Tabia hii ni ya pekee kaw sababu anajituma na
kujibidisha katika kutafuta vitoweo kwa nguvu zake mwenyewe. Tai sio mzembe, ni
mwenye bidii kati utafutaji au uwindaji wa chakula chake mwenye. Hana tabia ya
kula vitoweo vilivyojifia maana sio salama kiafya. Pia hali masazo kwa sababu
anaouhakika wa kufanikisha kupata chakula. Kujiamini kwa tai ni kutona na bidii
na uwezo mkubwa alionao wa kutafuta kwa nguvu na maarifa yake aliyonayo.
Hategemei kutafutiwa au kula vyakula vya bila Jasho Lake.
Wakati tai anapokuwa
amekwama kupa kitoweo, marachache huchukua mfupa wa kiumbe chocho huupasua kwa
jitihada zote, kasha hula zile “bone barrow’ zilizo ndani katikati ya mfupa
huo. Hata hivyo kuupasua mfupa kwa kuruka juu kasha anabamiza kwenye jiwe sio
shughuli nyepesi, inahitaji ushupavu na biidi iliyotukuka. Iwe katika kuwinda
au kupasua mifupa; tai hufanya kazi kwa biddi ili kufanikisha mlo wake.
Fudisho Tulipatalo
Katika maisha yetu:
Maisha
siyo rahisi, hayanyooki siku zote; tunatakiw tuwe imara muda wote katika
kutafuta ili kufanikiwa. Hakuna ambaye hafurahii kufanikiwa kwa jasho lake
mwenyewe. Wengi wanaposhindwa kufanikiwa humlaumu Mungu, na husahau kuwa;
kumuomba Mungu pekee bila kujibidisha hakutoshi, bali yampasa afanye kazi kwa
bidii na moyo wake wote. Kila mwanadamu anasehemu kubwa sana ya kufanya ili
kuleta maendeleo na mafanikio binafsi.
Kila jambo linafanywapo
kwa bidii zote na moyo wote huleta uhakika wa mafanikio hapo baadaye. Jambo la kufanya kazi kwa bidii ni jambo la
msingi katika kuyatafuta mafanikio. Mafanikio hayaji kwa mtu kwa kuendekeza
kulala, kuzulula, kushinda kwenye vijiwe na kupenda starehe bila kujibidisha
katika kufanya kazi. Mwanadamu akifanya kazi kwa bidii na kuipenda kazi yake,
atafanikiwa kwa namna ya ajabu sana.
Kufanya mambo makubwa
hakuji hivihivi bila kufanya kazi kwa bidii zote na kujituma kwa moyo wote.
Tuwe na tabia ya tai ya kutafuta na kutumia vitu tulivyovitafuta kwa jasho letu
wenyewe, na wala sio kutumia vya watu wengine. Binadamu hawezi kuwa na uchungu
wowote juu ya mali, vitu au mafanikio kama hajavitafuta kwa jasho lake. Kutumia mali au vitu vya watu wengine ni aibu
na huzaa masimango mengi; uhuru haupo kwani sio vyako, bali ametafuta fulani.
Wavivu na wazembe
hawaishi kulalamika na kuhitaji misaada kila kukicha, hali kwamba hana ulemavu
na nguvu anazo tena mwenye afya tele. Hakuna mtu wa kumletea mafanikio mtu
mwingine tofauti na yeye mwenye kujishughulisha, kujituma na kufanya kazi kwa
bidii kwa moyo wote. “Asiyefanya kazi na
asile” ni msemo tuliouzoea masikioni petu na kuuona ni wakawaida tu. Msemo huo
ukikaa ukautafakari, ni msemo wenye maana pana sana katika namna ya kumtia
mtu hamasa ya kutafuta vya kwake, na sio
kudandidandia vya watu wengine katika kutumia kama kupe au chawa (parasites)
waishivyo kwa kutegemea viumbe wengine ili maisha yasonge mbele.
Angalau asilimia 40 tu
ndani ya taifa (Tanzania) tukiwa watafutaji kama tai, tutaweza kuwa mbali
kimafanikilo. Sehemu kubwa ya watanzania
sio wazalishaji, nitegemezi. Yaani ukichukua wanafunzi, watoto, wazululaji,
wafungwa, wazee, wakinamama wa nyumbani, na wazembe wengine wengi, twaweza kuwa
na asilimia 10 hadi 25 tu ya wanaozalisha na kulisha taifa letu. Sisi kama
Wazarendo wa taifa, tukiamka, tunaweza kupiga hatua. Tusilalamikie serikali
hali kwamba hata kwa mtu mmoja mmoja anao wajibu wa kulisukuma taifa, aidha kwa
maendeleo ya yeye binafsi au taifa kwa ujumla.
SURA
YA SITA
TUWE
WENYE UPENDO NA WAAMINIFU KATIKA NDOA ZETU
Tai
hujenga ndoa yenye upendo na yenyekuaminiana. Maisha ya tai katika kujenga
mahusiano au ndoa ya mke na mme kabla ya kutafuta watoto, huanza na mitihani au
majaribio ili kuthibitisha upendo wa kweli. Kipimo hutolewa na tai jike ili
kujua kuwa tai dume atakuwa na upendo, utiifu na mwaminifu katika ndoa. Tai
dume anapofudhu mitihani kadha wa kadha ya kupima uaminifu na upendo wake kwa
tai jike, ndipo hatua na mikaka ya kupanga kuzaa pamoja hufuatia.
Tai (bibi na bwana)
wanapotaka kukutana (kuzaa), tai dume humfuata tai jike juu, kasha tai jike
agunduapo adhima ya tai dume ndipo neye (tai jike) hushuka chini na kuchukua
gome la mti, jani au tawi na kupaa nalo juu kwa tai dume. Tai jike amfikiapo
tai dume, ndipo huliachia hilo gome (jani, tawi) na kudondoka kuelekea chini;
hivyo tai dume huliendea kwa kasi na
kuli kamata kasha kulirejesha kwa tai jike. Zoezi hili hufanyika mara kadhaa
takribani muda wa nusu saa hadi lisaa limoja ili tai jike kumkubali tai dume na
kukutanA kimwili (kujenga ndoa).
Baada ya tukio la
kushirikiana kwenye tendo la kuzaa, tai jike anapotaka kutaga mayai (kuzaa); tai
dume na tai jike hushirikiana katika kutafuta eneo la juu ya mlima ili
kuanzisha makazi (kiota/kichali) ambapo maadui hawawezi kufika kwa urahisi.
Kuweka makazi juu ya ncha ya mlima, kwa sababu za kiusalama na urahisi
kuonekana kwa kila akati tai awapo juu angani.
Katika ujenzi wa kiota,
tai dume huenda kutafta miiba, magome, miti, nyasi na ngozi. Kwa kushirikia;
tai jike na tai dume huanza kujenga kwa kutanguliza miiba na kufuatiwa na
magome ya miti, nyasi na mwisho kabisa ngozi inayofunika vyote vilivyotangulia. Kiota hicho hufunikwa kwa miiba mingi
kukizunguka ili kuzuia maadui kukifikia kiota hicho.
Fudisho Tulipatalo
Katika maisha yetu:
Majaribu
huja ili kutupima imani zetu. Ni vyema tukawa na muda wa kutosha wa kupima
upendo wa wachumba zetu na rafiki zetu wa karibu, ili kujua kama wanaoupendo wa
kweli juu yetu. Kutobainisha upendo na uaminifu wa mtu wako wa karibu ni jambo
ambalo sio salama sana katika maisha yetu. Mtu mwenye upendo wa kweli ni yule
mwenye uwezo wa kuzibeba huzuni, shida, matatizo na changamoto zetu. Rafiki wa
kweli na mchumba wa kweli ni Yule ashilikiye na kuvaa viatu vyetu vya maisha
yetu ya kila siku.
Kuanza uhusiano (kuoa
na kuolewa ) na mtu ambaye hujajihakikishia upendo na uaminifu wake juu yako ni
kujipalia moto hapo badae; maana wapo ambao huanzisha mahusiano na mtu fulani
kwa kutimiza haja zao za matamanio au kuchuma kitu fulani katika mtu fulani.
Kwa wale wanaoelekea katika safari ya maisha ya ndoa na ambao bado wanatafuta;
kipindi salama cha kumchuguza tabia mtu, ni kipindi cha urafiki na kidogo
kipindi cha uchumba. Mtu ukisha mtamkia (wanamme) kuwa unataka kumuoa
(mwanamke) atajifanya kuficha tabia zote mbaya kwa maana ya kuficha makucha,
hadi umuoe. Akifika kwenye ndoa (mmeshaoana) anakunja makucaha yake; ndipo
kujuta kwa majuto mjukuu huja.
Ukiweza kumpima kiwango
cha uaminifu mwezi wako talajali wa maisha, utakuwa umejihakikishia ndoa imara
na yenye upendo daima. Huwa ni vigumu kubadirisha tabia ya mtu mkiwa kwenye
ndoa. Wakati wa kupima, kujua na kutibu tabia mbaya za mwenzi, huwa ni wakati
wa urafiki na uchumba pekee. Ni nadra sana kutibu tabia ya mwenzi mkiwa
mmeoana, tofauti hivyo, tegemea ndoa yenye maisha ya kuvumiliana; kila kukicha
aheli ya jana.
Ndoa yenye upendo wa
kweli, ni yenye umoja ambao umejengwa katika misingi ya kusaidiana,
kushirikiana kwa namna moja au nyingine. Kusaidiana na kushikishana kupo kwa
namna nyingi sana; mfano kazi za nyumbani, kupanga bajeti, kufanya maamuzi,
vipato vya familia, mawazo ya kila mmoja. Ndoa ni mwili mmoja hivyo lazima wanandoa
wawe kitu kimoja katika kutenda na maamuzi yao. Hakuna aliye bora, kila mmoja
humtegemea mwenzie ili kuijenga himaya ya familia kwa wanandoa.
Katika ndoa, lazima
kuhakikisha usalama na ulizinzi wa familia na watoto kwa ujumla. Wanandoa
lazima wlinde amani na usalama wa familia zao. Katika familia lazima pawepo na
usalama wa kiafya, uwepo wa amani, uhakika wa furaha kila muda, ulinzi wa Mungu
na uhakika wa chakula na mahitaji mengine ya kifamilia. Amani katika ndoa huletwa na upendo wa kweli.
Upendo usiochosha, upendo wa dhati na kweli; upendo usio wa hofu ya mwingine.
upendo wa pekee ni upendo ulioambatana katika kumcha na kumtumainia Mungu pekee
kwa kila jambo.
Familia yenye upendo ni
ile yenye kubeana madhaifu na mapungu kwa wanandoa, kutiana moyo na sio
kukatishana tama; yaani baba anafanya, mama anatia moyo ili mme wake asonge
mbele. Tujifunze yaliyo makuu na mema kutoka katika upendo wa kimbingu, ili
tuyaishi mema ya ndoa zetu zilizotayali au tuzitarajiazo.
SURA
YA SABA
TUWALEE
WATOTO KATIKA UVUMILIVU, KUJIAMINI NA KUJITEGEMEA
Tai
hulea na kufundisha watoto wake katika jujiamini, kuvumilia na kujitegeme
katika maisha yao. Baada ya watoto wa tai kuwa wakwisha kutotolewa; mama yao
huwatoa kwenye kiota, lakini watoto hurudi tena kwenye kiota. Mama wa watoto
hufanya jambo moja ambalo huwafanya watoto watoke kwe kiota. Jambo hilo huwa ni
kutoa ngozi, nyasi, magome ya miti katika kiota, na hubakisha miiba ambayo
huwachoma watoto na kujihisi maumivu kwa kiasi kikubwa.
Lengo la mama wa watoto
wa tai sio kuwaaumiza, bali kuwafanya watoto watoke katika kiota ili waanze
maisha mapya, pamoja na kuzoea maisha mateso na raha. Baadae mama yao huwasukuma pembeni ya kilele
cha mlima ili wadondoke. Kabla watoto hawajaanguka, mama yao huwadaka kwa mbawa
zake. Kitendo hicho cha kuwasukuma hufanyika mara kadhaa hadi watoto wote wajue
huruka sawasawa. Mafunzo ya kuruka, hufanyika kwa mantiki hiyo ili kuondoa hofu
na kujenga kujiamini.
Fudisho Tulipatalo
Katika maisha yetu:
Mara
nyingi mateso hutupa ujasili pamoja na uvumilivu. Kupitia magumu katika maisha
hujenga uvumilivu na kuzikabili changamoto katika uzoefu wa maisha. Kuyapitia magumu katika makuzi ya mtoto,
humjengea uwezo mkubwa wa kuzikabili changamoto na uwezo mkubwa wa kutoteteleka
katika magumu ya maisha katika umri wa utu uzima.
Katika maisha; mateso
hutupatia mbinu mpya za kuweza kukabiliana na mambo au changamoto mpya za
maisha kulingana na mazingira mapya, maendeleo, teknolojia na changamoto mpya.
Bila changamoto, mwanadamu hawezi kubuni au kugundua jinsi mpya ya kukabiliana
na matukio mapya. Mateso (miiba), shida, dhiki na adha zitusongazo wakati
mwingine hutupa uwezo wa kuwa bora zaidi kwa ajili ya hatua zingine zaidi.
Changamoto zitukabilizo
hutufanya tukomae kiakili pamoja na kuwa na uwezo wa kupambanua, kufanya
maamuzi na kutatua mambo mbalimbali yatukabiliyo. Akili zetu haziwezi kukomaa
na kuwa na uwezo mkubwa wa maamuzi bila kukutana na changamoto za aina
mbalimbali aidha, rahisi na ngumu.
Mototo ni vyema alelewe
katika maisha ya aina zote; shida na raha zampasa kuzijua katika hatua zote za
makuzi ili baadaye awe na uwezo wa kuzikabili changamoto na kuyaishi maisha ya
shida na raha. Si vyema sana motto akaishi maisha ya raha pekee, siku za
ukubwani yakitokea magumu anaweza akateteleka na kuathili hatua zote za maisha
yake.
Kama alivyo tai kwa
watoto wake; vivyohivyo .Mungu wakati mwingine hujifanya kama haoni yale
yanayotukabili, ili tuweze kupiga hatua na kumtumainia yeye katika imani
isiyokoma.
SURA
YA NANE
TUWE
WENYE UHAKIKA WA MAISHA YETU
Tai
wanaouhakika wa kujiongezea maisha na kuishi tena afikapo umri wa kuchoka au
kupoteza nguvu. Tai anaweza kuishi miaka mingi; kuanzia miaka 30 hadi 70.
Wakati ambapo tai anakuwa ameanza kupoteza uwezo wake, kwa sababu ya kuishi
miaka mingi (afikishapo miaka 30 na kuendelea), uwezo wa kukamata mawindo
hupungua kutokana na kupungua ngu vu zake. Sanjali na kupungua nguvu, tai pia
mdomo au urengu (sehemu za kudonolea) wake hupungua makali na uwezo wake kwa
sababu huwa umepinda sana.
Aidha, kutokana na uzee
na uzito wa mabawa, mabawa, manyoya yanarundikana kuelekea sehemu za kifuani na
kupekea tai kushindwa kurukavyema.
Katika wa hali hii hubakiwa na maamuzi mawili pekee. Mosi; kukubali kufa kwa njaa kwa kukosa
chakula kutokana na hali ya kuchoka alikokufikia. Mbili; kuendelea kuishi kwa kupitia mateso ya takribani 80 au 145
na kuendelea. Ili tai aendelee kuishi, humpasa kupanda juu ya ncha ya mlima
kasha huanza kujitoa ganda la juu la midomo yake kwa kujipigiza kwenye mawe au
kitu chochote kigumu.
Baada ya ganda la mdomo
wa juu na wachini kutoka, tai husubiri hadi ganda la ncha ya mdomo wa juu na
chini liote (iwe katika ugum wote).
Baada ya hapo tai huanza kujitolea manyoa yote katika mwili wake wote.
Baada ya siku kadhaa (miezi miwili hadi mitatu) manyoya huwa yameota na
kuongeza tena maisha mengine ya kuishi aidha, mika 30 au zaidi.
Fudisho Tulipatalo
Katika maisha yetu:
Wakati
mwingine watu hujiua au hujinyonga kwa sababu ya kushinwa kuvumilia na
kuzikabili changamoto. Jambo hili la kujiuwa kwa watu wengine husababishwa na
kukosa tumaini katika maisha kwa kukosa uwezo wa kuhimili changamoto na ugumu
wa maisha.
Kutumia vileo, madawa,
sigara na vitu vituleteavyo madhara na kuathiri afya zetu, hutukosesha uhakika
wa kuishi tena. Kutojari kanuni na taratibu za afya katika miili yetu juu ya
nini tule, tunywe na tuweke juu ya miili yetu husbabisha magonjwa katika miili
yetu, hivyo hupunguza uwezo wa kuishi.
Kuteseka ni lazima kuje
ili kuyafikia mafanikio mapya. Ni vigumu kuyafikia mafanikio bila kuteseka kwa
namna moja au nyingine. Kupiga hatua na kulikabili jambo kunahita maamuzi
yanayoumiza wakati mwingine. Hata kama mengine yanaumiza lazima tukubali,
kuyapokea na kufanya badiliko.
Yatupasa kuibua mambo
mapya mazuri yenye manufaa kwa jamii yaliyofichika ambayo wengine
hawajayagundua wala kutambua. Lakini pia waweza kuibua mabo mapya mabaya
yaliyofichika ili kuyaweka bayana kwa jamii ili jamii iyafahamu na kuyaacha.
Fanya matengenezo kwa
kurekebisha pale ulipopelea na kukosea ili kufanya uwe mpya katika safari ya
maisha yenye mafanikio. Matengenezo yatakupa nguvu mpya na kukukufanya uanze
upya kwa ari na uwezo mpya kwa kufuta yale yote yaliyokufanya upoe, urudi nyuma
au ukate tamaa.
Tusikubali kufa kizembe
kwa kujitakia kinyume na mapenzi ya Mungu muumba wetu. Kutumi vitu, vyakula,
vileo visivyofaa na vyenye kuhatarisha afya zetu. Utumiaji wa sigara, pombe,
vipodozi vya kikemikali vyenye madhara pamoja na kufanya ngono kupita kiasi.
Chochote unachotumia kwa wingi chenye madhara katika mwili kitakuletea madhara
hatimae kifo. Kubadiri mitindo yetu ya maisha kwa kuiga kutoka nchi za
magharibi na kuacha ulaji wetu wa asili na mienendo ya maisha ya kiafrika.
Kuna muda, mtu hufanya
mambo fulani kwa sababu, kila mtu hujikuta katika mkondo au maisha
yalimchagulia namna ya kuishi, lakini hayo yote huwa ni matokeo ya bahati mbaya
ambayo kuna muda kwa uzembe wetu au kwa kuyaamini tusiyoyamaanisha tukajikuta
tumeyatenda ema. Kama umegundua ulipojikwaa yakupasa urudi nyuma na uanze upya.
Kila mtu anahistoria
yake katika maisha yake lakini ikitokea ukajua unapokosea na kujirekebisha basi
hiyo ni faraja ndani ya moyo wa kila mmoja aliyechukizwa na tabia yako ya
awali, hivyo basi waweza kutubu dhambi zako na kungu atakusikia.
Kitu kidogo na cha
pekee na cha thamani unachoweza kufanya katika maisha yako ni kutafuta nini
unachokitumainia, na kikubwa unachoweza kufanya ni kuishi ndani ya matumaini
hayo. Siyo tu kuyakubali kwa mbali ila kuyaishi kwa undani wake. Matumaini
yanaweza kuwa nguvu kubwa yenye msukumo. Inawezekana kabisa kusiwe na miujiza
ndani yake, ila ujuapo kinachokutumainia
sana na ukakikumbatia kama
mwanga ndani yako, basi unaweza kutenda
jambo na kufanya mambo yatokee kama miujiza. Kwa hiyo, yafanye matumaini yako
yaishi. Jukumu moja wapo la binadamu ni kufikiri kwa niaba yako mwenyewe.
Katika kufanikiwa,
binadamu lazima ajipange wajipange vyema. Kila mtu ananafasi ya kuwa vile
atakavyo, haijarishi njia atumiayo ilimradi upo ukweli wa kila jambo. Mafanikio
huja tu pale unapoamua kufanya mambo magumu kuwa mepesi unapoamua kulitazama
jua kwa ukali ukali wake
Kila binadam anahadithi
na simulizi juu ya maisha yake. Aidha,
ya kusikitisha pengine ya
kukatisha tama, bali tunatofautiana namna ya kuzikabili huzuni zetu. Kila mmoja
alishawahi kupitia jambo gumu la kukatisha tamaa, na wengingine waliteseka na
kukubali matokeo ya jambo hilo na walisonga mbele
Haitupasi kujiona kuwa hatuna
bahati katika maisha. Yatupasa kujua kuwa maisha yanamambo mengi ambayo ni
msamiati kwenye fikra zetu. Majibu
sahihi kwa msamiati ambao hauujui ni kubahatisha jibu la swali ambalo ambalo
hujalisikia kamwe; hivyo unachotakiwa kufanya ni kuiambia nafsi yako itawale
utashi wako.
Maisha hutupa
changamoto ili kupima ujasili wetu wa kubadirika. Katika muda huo wa
changamoto, nafasi ya kufanya kwamba hakuna linalotokea au kusema kuwa hauko
tayari kuipokea hiyo changamoto. Changamoto hazisubiri utaya wako na maisha
hayaangalii nyuma maana ni kama sheria mpya inayotungwa juu ya jambo fulani;
huwa inaanza pale iliposainiwa. Wiki moja ni zaidi yawa kutosha tunaouhitaji
ili kuamua kama tunakubali au la. Japokuwa pia kuhitaji kwenda mbele kwenye
maisha yako, lakini unaweza kukuta umeweka mguu mmoja kwenye “break”.
Nini thamani ya maisha
kama tunaamua kwenda mbele kwa maisha ya kukanyaga breki. Ili uwe uwe huru,
lazima ujifunze kusahau na kuacha mambo mengine yaende. Acha kuumizwa na machungu, acha yaende kasha
sahau. Maumivu yako na maisha yako ya zamani ndiyo yanayokuvuta nyuma na
kufanya usisonge mbele. Kubali kuanza upya.
Watu waliofanikiwa
zaidi ni wale walioyajua matatizo, walizijua harakati za maisha, waliokumbana
na misukosuko na taabu, walioyakabili
majaribu ya kila namna na changamoto zake na mwisho wa siku waliweza kusonga
bele. Lolote ambalo haliwezekani leo, unaweza kulifany liwezekane kesho endapo
utaamua tu juu ya mustakabali wa njia uipitayo.
SURA
YA TISA
KUMKABIRI
ADUI KATIKA UWANJA VITA
Tai
humshinda adui kwa kumbadirishia uwanja wa vita aliouzoea. Harakati za
kujipatia kitowe kwa tai kuwa ni cha kufa na kupona maana anayewindwa huwa ni
adui kwa namna nyingine. Tai anapokuwa katika harakati za kutafuta kitoweo,
hukikamata kitoweo kutoka eneo husika na kupaa nacho angani katika uwanja wa
vita aliouzoea ambao kwa adui (kitoweo) ni mpya. Kitoweo hicho cha weza kuwa
nyoka, samaki au mnyama aliye na ukubwa wa kubebwa na tai. Tai hufanya mbinu
kadhaa ili kumshinda adui/ kitoweo huyo kwa kumuachia angani na kumdaka tena
kabla ya kufika chini. Tendo hili hulifa kwa vitoweo ambao ni hatari kwa maisha
yake kama nyoka ili kumpotezea adui
uwezo na ujasili kukabiliana na tai. Wakati mwingine huwapelekea vitoweo hivyo
watoto.
Fundisho tulipatsalo la
kujifunza.
Wakati
mwingine ili ushinde katika mpambano wa wa kutafuta, ni vyema ukabakia
mazingira hayo hayo uliyoyazoea; maana unayafaham kiundani zaidi. Hivyo basi,
usiruhusu mazingira yakubadirishe, bali jitahidi mazingira uyamudu na
kuyabadirisha wewe kwa namna yoyote.
Mara zote inatupasa
kufahamu uimara au uwezo wetu uko wapi, pia udhaifu wa washindani wetu upo wapi
katika biashara ili kuweza kuwazidi katika ushindani juu ya soko huria
Katika harakati ya
kutafuta mafanikio, waweza kwenda kutafuta mbali kasha ukarejea nyumbanili ili
kula matunda ya mafanikio na wanyumbani kwako badala ya kutapanya hukohuko.
Wengi huenda mbali sana kutafuta nje ya maeneo way ale wanayoishi ili kutafuta,
lakini cha kushangaza hali na walio wa nyumba zao kwani huzamia hukohuko na
wasirudi tena na kuacha familia zao zikiteseka. Kula matunda na wale wa familia
yako kutakuzidishia mibaraka ili uzidi kufanikiwa zaidi; maana mchumia juani
hulia kivulini na wa kwao
Elimu au taaluma
uliyoipata mahala fulani; uichukue hivyohivyo lakini usisahau kujiendeleza
zaidi ya walimu wako walivyokupatia katika kukufundisha. Daima mtazamo wako
uende mbali zaidi ili kuweza kuwapita wengine katika fikra na maarifa yao
katika kiwango walichofundishwa awali, wewe zidi kwenda mbele.
Kama ni mfanyabiashara,
peleka bidhaa au mali uliyoinunua sehemu ambayo unaijua kwa uhakika. Eneo
ambalo unalijua vyema; litakupa uhakika wa faida na kukuzalishia zaidi na
zaidi.
Katika maisha kumbuka
kuhesabu mibaraka badala ya matatizo katika kutafuta mafanikio. Mara nyingi
kutokana na uzoefu, watu wengi huwa “busy” kuhesabu matatizo kuliko mafanikio
yatokanayo na mibaraka. Twaweza kuyaelewa maisha kwa kuangalia nyuma, ila
twaweza kuyaishi maisha kwa kuangalia mbele. Mafanikio huja kwa kuweza,
kushindwa huja kwa kutoweza.
Kuanguka
chini hakukufanyi kuwa ndiyo umeshindwa, bali kuendelea kukaa chini ndiko
kutakuashiria kuwa umeshindwa. Hivyo, kushindwa kwa mtu husababishwa na ukosefu
wa bidii na sio ukosefu wa kipaji. Mafanikio hayaji kwa kila mtu hivihivi, bali
kwa mtu Yule anayejitahidi kuwa mwenye bidii, mwadirifu na mchapa kazi. Naamini
ukifanya sehemu yako kwa bidii na moyo wako wote, Mungu atakuwa nawe katika
mafanikio
NA MWL. FRANK PHILEMON
Comments
Post a Comment
Thanks for viewing and passing through NMEE blog. Keep following the blog