Posts

NGUVU YA MSAMAHA

Katika injili ya Marko 11:25-26 kusameheana kumesisitizwa kama ifuatavyo: 25 ”Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili Baba yenu aliyembinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. 26” Lakini kama ninyi hamsamehi, wala Baba yenu aliye Mbinguni hatawasemehe ninyi makosa yenu” Kwa Nini ni Muhimu Kusamehe? Zipo sababu nyingi za kusamehe, zifuatazo ni miongoni mwazo: 1.       Kusamehe ni tabia ya Mungu, na wamchao: Mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu ( Mwanzo 1:26 ). Mwanadamu amchae Mungu kwa kweli yote, lazima awe na tabia ya Mungu kwa maana Mungu ni kielelezo cha kwanza cha kusamehe kwa mwanadamu ( Isaya 43:25. Isaya 1:18, 1Yohana 1:9). 2.       Kusamehe ni hali ya Upendo: Kama tunda la roho ni upendo vivyo hivyo kusamehe ni tunda la upendo ( 1Wakorintho 13:4-7 ) . Tabia ya mtu amchae Mungu ni upendo kwa wengine hata kama atakwazwa. Mungu ni pendo, hata mwanadamu pia yampasa awe na upendo utokanao na Mungu. Kusamehe ni ishara na kielelezo

MAISHA NA TABIA YA TAI CHACHU NA SOMO KWA MAISHA KWA MWANADAMU

Utangulizi Kila kiumbe kilichopo duniani hapa cha weza kuwa fundisho zuri au baya katika maisha yetu kulingana na jinsi kilivyotumika katika lugha ya picha. Wanyama kama Sungura na Tumbili; ni wanyama wanaowakiliaha wanadamu wenye tabia za ujanjaujanja au wajuaji sana. Simba anasimama kwa niaba ya watu nguli, wababe na wakali wenye uwezo na mamlaka. Fisi anasimama kwa niaba ya watu warafi. Twiga kwa watu wenye malingo na mikogo. Njiwa anasima kwa niaba ya utaktaifu, upendo, uaminifu na upole kwa watu. Nyoka anasimama kwa niaba ya watu wenye tabia ya uongo; wachonganishi. Ndege aina ya kasuku kusimama kwa watu wenye kuongea sana. Wasifu au Sifa Na Tabia Za Tai Wanyama na viumbe mbalimbali wanapotumiwa katika lugha ya picha hutoa na huashiria tabia na mienendo ya maisha ya kila mwanadamu. Kwa sehemu kubwa nitazungumzia katika ‘wasifu na mwisha ya ndege Tai’ kama chachu na somo kwa mwanadau. Ndege tai yupo katika aina au makundi yanayozidi 55. Katika kufuatilia taarifa na m

SOMO: MADHARA YA KUKATAA KUMTII MUNGU

Image
FUNGU KUU : ( Mwanzo 6:6-8) . “BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. BWANA akasema, nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitaambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi kwamba nimewafanya. Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana” UTANGULIZI : Katika somo hili “Madhara ya kukataa Kumtii Mungu” limehusisha kitabu kilicho andikwa na Musa hususani sura ya 3, sura ya 4, sura ya 5, sura ya 6 na ile sura ya 7. Katika sura hizi kunamambo makubwa ya kujifunza ili yatujenge katika safari yetu ya wokovu. Tutaona jinsi gani anguko la mwanadamu linavyotokea kwa sababu tu ya kukataa kumtii Mungu pamoja na madhara yake. Katika sura hizo zote; visa vyake vimefupishwa mno katika biblia, hivyo wengi huwa wanashindwa kuelewa mambo mengi na yamsingi. KIINI CHA SOMO : 1. Dhambi iliingia duniani kwa sababu Adamu na Hawa hawakuweza kutii taratibu na sheria za Mungu (Mwanzo 3:1-3). Ukisoma kwa umakini kati