HIV/UKIMWI
HIV/UKIMWI
AIDS (Ukimwi)
upungufu wa kinga mwilini.
Hii humaanisha
kwamba ugonjwa hudhoofisha mfuno wa kinga.
Kwa sababu mfuno wake wa kinga ni dhaifu, watu wenye ukimwi hujenga hofu
ya maisha katika magonjwa na maambukizi ya kifua kikuu, kansa na magonjwa
mengine. Virusi (HIV) hufanya kazi
polepole na waathirika huweza kuonekana wenye afya njema kwa miaka hata 10
kabla hawajaanza kuugua na kufa. Hakuna
tiba ya virusi / ukimwi. Hivyo kila
apataye virusi vya ukimwi atakufa.
Mamilioni ya watu duniani wameathirika na ukimwi.
Unapokuwa na
virusi, tunasema ni mwathirika na virusi. Unapoanza kuugua bila kupata nafuu tunasema
una ukimwi. Wachunguzi wanasema
kwamba vifo vya waathrika wa ukimwi vitakuwa milioni 1,7 kwa mwaka ifikapo 2006. Badala yake vifo milioni 3 viliripoliwa kwa
mwaka 2001 peke yake!! Kwa kweli ugonjwa
kuu ni mbaya sana kuliko tunavyo dhani.
Katika mwaka 2001 watu zaidi ya milioni 22 walikufa kwa ukimwi. Zaidi ya watu milioni 40 waliambukizwa virusi
vya ukimwi. Nani ajuaye idadi
tunapoingia katika mwaka wa 2004? Jana
hili limekuwa baa kubwa. Wachunguzi husema
kwamba ifikapo 2010 utapunguza miaka ya kuishi Afrika kufikia mwaka 30. Idadi kubwa ya waathrika ni vijana. Kila siku katika Afrika vijana 7, 000 huambukizwa
virusi. Maambukizi husambaa toka kwa
vijana hadi kwa watu wazima wanaojamiiana na vijana. Waganga wengi wa hienyeji huwaambia watu
kwamba ukijamiiana na bikira basi umepona.
Hii siyo kweli. Watu katika
Afrika hawapendi kuzungumzia ukimwi.
Hawawa elezi watoto wao kuhusu kujamiiana na watoto wao wengi
wanakufa. Wakati umebadilika na ni
wakati wetu kuongea na watoto wetu na majirani kuhusu hatari ya kujamiiana nje
ya ndoa. Vijana wana uelewa au ujumbe
potofu na huhatarisha maisha yao wapolala ovyo.
Ukimwi husambaa
vipi?
A. Kwa Kujamiiania:
- Mume kwa mke na mke kwa mume.
- Mume kwa mume.
B. Damu:
- Kuongezwa damu.
- Kuchangia sindano na vifaa vingine.
C.
Watendakazi wa Afya:
- Sindano, majeraha yalivyo wazi.
D. Kuchomwa sindano zisizo chemshwa katika hospitali na kliniki.
E. Watoto:
- Tumboni
- Katika njia ya mzazi
- Kwa kunyonyesha
Iwapo mjaanzito
ana virusi kuna tiba maalum kupunguza hatari ya mtoto kuambakizwa.
Virusi / Ukimwi
hauambukizi kwa hugusana. Na wala hauambukizi
kwa njia ya wadudu. Watu wanaokunywa
pombe wako katika hatari ya kupata virusi/ukimwi kwasababu wanafanya maamuzi
mabaya. Pombe pia hudhoofisha kinga ya
mwili na hufanya maambukizi ya virusi vya ukimwi kuwa rahisi. Mungu anayo njia ya utatuzi wa janga
hili. kwa hakika na utatuzi wa
awali. Kama ulimwengu ungekubali agizo
hili ungeondosha mara moja gonjwa hili.
Agizo la Mungu ni ndoa kati ya mume na mke kwa maisha yote. Mungu anasema kujamiiana nje ya ndoa ni chambi. Kutoka 20: 14 Usizini. Kuna kanuni nyingine zinazopatikana katika
Biblia ambazo kwa hakika zinatulinda.
Mambo ya Walawi 18: 22.
Kumbukumbu la Torati 23: 17.
Kutoka 22: 19. Warumi 1: 24, 26, 27.
1 Wakorintho 6: 9-10.
Mungu anahitaji
sisi sote tuwe wenye afya na furaha.
Yeye hututakia tu lililo jema kwetu.
Sasa ni wakati wa kufuata uongozi wake na kuwambia wengine maagizo yake
kuhusu afya. Kumbuka kwamba watu wenye
virusi vya ukimwi wanahitaji msaada wetu wa hali na mali. Wengi wao walikuwa waaminifu walipoambukuzwa
na wengine wanajuta kwa kufikira walivyotenda vibaya. Tunahitaji kuanza kuzungumza juu ya gonjwa
hili na siyo kuacha na kukwepa ukweli kabla hatujachelewa!
Comments
Post a Comment
Thanks for viewing and passing through NMEE blog. Keep following the blog