Kisa Maarufu Cha Nyama
Daima tumekuwa tukiamini kuwa tunahitaji kula nyama ili tuwe
na nguvu na afya. Kwanini? Kwasababu nyama ina ‘protini’ na ni ya muhimu
sana kwa miili
yetu. Inajenga na kutengeneza miili
yetu. Lakini mwaka 1950 wana sayansi
waligundua kuwa hasa tunaweza tukawa tunakula protini kupita kiasi. Hasa kama tuna kula nyama nyingi. Wana sayansi hawa ni Daktari Hardinge na
Daktari Stare walithibitisha kuwa mtu ambaye anatumia vyakula vya mimea tu
(vegetarian) hupata protini zote ambazo mwili wake unazihitaji. Watu wameamini kuwa kula sana vyakula vya protini za mnyama itatufanya
tuwe na nguvu na uwezo. Vilevile
waliamini kuwa husaidia akili na mwili.
Lakini ni jambo la kweli? Ni wapi
jambo hili la umaarufu wa nyama lilikotokea?
Protini iligundulika 1838.
Protini ni muhimu kwa namna yoyote ya maisha! Ni yamuhimu sana !
Tunahitaji protini ili misuli yetu itende kazi vizuri, kuwa na homoni
nzuri na uwiano wake mzuri, tuweze kukua na kutengeneza sehemu tulizo jikata na
vidonda na vitu vingine vingi. Kwahiyo
umuhimu wa protini hakuna ‘kisa’ ni ya muhimu tu! Lakini watu wamechanganyikiwa na kufikiri
kuwa tunaweza tu kupata protini toka kwa vyakula vya nyama. Protini moja ina kemikali asidi 20 au inaitwa
(amino acids). 12 ya hizi asidi
hutengenezwa miilini mwetu, lakini 8 zinazobaki sivyo. Tunahitaji kupata hizi asidi 8 tokana na
vyakula tulavyo. Watu walifikiri unaweza
kupata kwa kula nyama tu. Lakini hawakujua
kuwa ng’ombe ni kama wanadamu tu! Nao pia wanahitaji asidi 8 na
wanaipata kwa kula majani! Kwa kweli
tunaipata asidi 8 iliyotumika kwa sababu ng’ombe kwanza lazima ale majani. Hatuhitaji kula nyama, hivyo, tunaweza kula
mimea – vyakula muhimu na kupata protini ifaayo ambayo kamwe haijatumika na
ngombe, nguruwe, au samaki!
Wanasayansi vilevile wameona kuwa miili yetu haihitaji
protini nyingi kama ilivyo fikiriwa! Tunaweza
hasa kula protini – protini ambayo ni ya kutuletea afya.
Chakula cha mimea kilicho na matunda, nafaka, mboga za
majani na jamii ya karanga ni vya kiwango cha pekee sana kwa protini! Siyo protini kupita kiasi au pungufu
mno. Tunapo kula nafaka za aina
mbalimbali, mboga za majani, karanga na matunda tutapata zaidi kuliko protini
tu. Tutapata virutubisho vingine ambavyo
ni vyamuhimu pia! Hapa kuna baadhi ya
mifano ya vyakula vyenye uwingi wa protini na vina asidi zote zinazo hitajika
mwilini:
1. Viazi vitamu 2. Viazi mviringo 3. Mchele
wa rangi ya kahawia (au
4. Nyanya 5. Maboga mchele
mweupe usio kobolewa upo
6. Unga wa ngano
kamili 7. Mahindi hapa
Tanzania )
8. Maharagwe 9. Mboga kijani
kibichi 10. Kitunguu saumu
Protini kupita kiasi mwilini vilevile ‘huiba’ virutubisho
vingine vinavyoitwa ‘kasiamu’ kasiamu ni ya muhimu sana kwasababu hutupatia mifupa yenye nguvu na
afya ya meno. Watu husema kuwa
tunahitaji kula nyama nyingi na kunywa maziwa ilikujipatia kasiamu. Lakini wanasayansi wamegundua kuwa maziwa na
nyama hutupatia protini nyingi kupita kiasi na protini hiyo ‘huiiba’
kasiumu. Na hutusababishia udhaifu wa
mifupa hasa kwa akina mama wazee.
Unaitwa osteoporosis – ugonjwa wa mifupa kwa kukosa kalisiumu mwilini.
Tunapokula vyakula vya mimea vyenye wingi wa kalisium,
tutapata kalisium zaidi kuliko kunywa maziwa kwasababu miili yetu haitumi
kwa wingi kama 60%- 80% ya kalisium ya maziwa
kwa vyovyote vile! Ni aina gani ya
vyakula vilivyo na wingi wa kalisium?
1. Dengu 2. Nafaka 3. Mchicha na mgoa kijani
4. Maharage 5. Ufuta 6. Rapu
7. Maharage ya soya 8.
Maziwa ya soya 9. Alizeti
Siri ya kuwa mwana
matengenezo mwenye afya: Kula aina
mbalimbali za vyakula. Kama
ukiamua kula tu ugali na maharage na bila kingine mwili wako utakosa lishe
nzuri na mwishowe utaugua. Kula aina
anwai za mboga na matunda katika juma.
Changanya na vyakula vingine.
Andaa chakula chako vizuri, kionekane kizuri na chenye afya na ufurahie
unapokila!
Vilevile wanasayansi wamethibitisha kuwa nyama pamoja na
uwingi mno wa protini husababisha kansa, ugonjwa wa moyo na athari nyingine
mbaya za afya. Ni wakati wa kufanya
mabadiliko!!
Tafadhali Kumbuka: Ujumbe wa afya ni muhimu sana , lakini tunahitaji daima kumwomba Mungu
atusaidie kuwa na uwiano. Ni
muhimu sana
kuto wa kwaza watu kwa kuwa piga nyundo (gonga – hammering) kuhusu kula nyama
na kuwa ambia vitu vya kijinga kama
‘hutaokolewa kamwe kama si mwana matengeneto!’
Na amini wengi wameukataa ujumbe wa Adventista kwasababu ya
misimamo mikali ya watu kanisani. Wewe mwenyewe
uwe mfano! Onekana unaishi kiafya na
watu wengine watafuata ushauri wako mzuri.
dsaResource:
Comments
Post a Comment
Thanks for viewing and passing through NMEE blog. Keep following the blog