Kwanini Tuwe Na Afya Njema?

www.2 lightingtheworld.org


Kanisa lenye furaha, familia yenye furaha, na jamii yenye furaha hufanywa na watu wenye afya.

Mtu mwenye afya:                1.  Ni mchangamfu sana.
                                                2.  Anaweza kupata zaidi.
                                                3.  Anaweza kuzalisha zaidi.
                                                4.  Anaweza kuwasaidia wengine zaidi.
                                                5.  Anaweza kuufahamu upendo wa Mungu vizuri zaidi.
                                                6.  Anaweza kuwaeleza vema wengine kuhusu upendo wa Mungu.
Kwa nini?  Biblia inaelezea sehemu 4 tofauti ndani ya mtu.  Luka 2: 52 Yesu alikua katika:
  1. Hekima                                   -  Anaye fikiri au sehemu ya ubongo.
  2. Kimo                                       -  Aliye na mwili au sehemu ya mwili.
  3. Akimpendeza Mungu           -  Aliye na uhusiano na Mungu au sehemu ya kiroho.
  4. Na wanadamu                       -  Aliye na uhusiano na wengine au sehemu ya jamii.

             
“Hivyo ni kwa ukaribu sana afya inahusiana na furaha yetu ambayo hatuwezi kuipata kwa kutangulia kitu cha pili badala ya cha kwanza.”  (paraphrased) Mrs. E.G. White – Counsels on Health, p. 38

“Chochote kichocheacho afya ya mwili, hu chochea maendeleo ya nguvu ya akili na uwiano mzuri wa tabia.”  (paraphrased )  Mrs. E.G. White – Education, p. 195.

Wakati Yesu alipokuwepo duniani alitambua namna ya umuhimu wa afya, ni kuwa na uwiano kamili.  Kwanza aliwaponya na kisha aliwafundisha watu. 

“Wakati wa huduma yake, Yesu alichagua muda Mwingi kuponya wagonjwa kuliko kuhubiri.”  Mrs. E.G. White – Ministry of Healing, p. 19. 

Enzi za wakati wa Biblia, Mungu aliwaita waisraeli kuwa watu maalumu na wenye huduma maalum.  Mungu aliwapa kanuni maalum za afya ili kuwasaidia katika kazi hii.  Unaweza kuzi soma kanuni hizi katika kitabu cha walawi.  Ili wao waweze kuelewa upendo wake Mungu na kuifanya kazi aliyo ikusudia waitende, walihitajika wawe na akili safi, mwili, na kijamii.  Katika dunia leo kuna watu wengi wanao hitaji uponywaji wa akili zao na miili kabla ya kuweza kukua kiroho na kijamii.  Mungu amewaita watu wake leo kuwa watu wake wa pekee wenye huduma maalum; duniani.  Tunakuwa na afya – kwa kufuata kununi za afya.

N      Nutrition           Lishe
E      Exercise             Mazoezi
W     Water                Maji
S       Sunshine            Mwanga wajua
T      Temperance      Kiasi
A      Air                     Hewa
R      Rest                    Pumziko
T      Trust in God     Kumtumaini Mungu

Tunapokuwa na afya Yesu anaweza kuwasiliana vema nasi.  Tunaweza kuwa saidia wengine kuwa wenye afya na furaha pia. 



Comments

Popular posts from this blog

MAJINA YA WANAWAKE KATIKA BIBLIA ‘A’ HADI ‘Z’

MFANO WA MPANGO KAZI

SOMO: MADHARA YA KUKATAA KUMTII MUNGU