SAMAKI
Samaki
Miaka kadhaa
iliyopita watu walisikia kuwa kula samaki kuli leta afya sana. Watu wengi waliacha kula nyama nyekundu na
kuhamia kula mlo wa samaki. Kiwango chao
cha mafuta mabaya kwenye damu (cholesterol) kilipungua na walikuwa wakijisikia
furaha. Watumiaji wa vyakula vya mimea
walianza kutumia samaki na viwango vya (cholesterol) vilipanda kidogo! Je, hasa samaki ni kitu kizuri kwako? Tuta angalia jambo hili kwa ukaribu. Kuna visa viwili katika jambo hili.
Watu walihamasika
kuhusu ulaji wa samaki kwa wingi kwasababu ya baadhi ya mafuta yanayo patikana
ndani ya samaki wakubwa na wanene.
Mafuta hayo yanaitwa omega 3
fats. Yaani aina 3 muhimu za
mafuta. Na yana weza kupigana dhidi ya
magonjwa ya moyo. Tatizo ni kuwa samaki
ni kundi la nyama na kwahiyo ina cholesterol ndani yake. Hivyo unapokula samaki una inua cholesterol
yako mwenyewe katika damu yako. Na kama
unataka unufaike zaidi ni heri ujiepushe kabisa na ulaji wa mafuta yato kanayo
na wanyama badala yake na uwe mtumiaji wa vyakula vya mimea tu. Kwa nini?
Kwa kuwa aina kuu tatu za mafuta zinapatikana katika vyakula vya mimea
ambayo ndani yake havina athari ya cholesterol.
Hapa kuna mifano ya vyakula vyenye aina kuu tatu za mafuta: Maharage
ya soya; mafuta ya soya; spinachi; parachichi; viazi vitamu; ndizi; apples;
viazi mviringo; tango; mkate wa ngano kamili.
Hapa kuna mfano
mwingine wa njia nyingine ya ajabu ambayo Mungu ali tuandalia lishe kamili katika
vyakula vya mimea. Kitu kingine tunacho
paswa kufahamu ni uchafu. Siku za leo
Bahari nyingi zimecha fuliwa pamoja na mito mikubwa na maziwa. Wana sayansi wamegundua kuwa samaki wamejawa
na sumu (toxins) ambazo zina kuwa na nguvu.
Hivyo maji yaliyo na mchanganyiko na uchafu yanaweza kusababisha samaki
walio wachafu zaidi. Kwanini ni vibaya
kula samaki walio katika maji yaliyo chafuliwa hivyo? Sumu zipatikanazo ndani
ya samaki mwenyewe zimekuwa na usababishi wa kansa kwa mwanadam na inatakiwa
kuzuiliwa. Kwa ajili ya afya ni vizuri
zaidi kula mlo wenye afya wa chakula cha mimea.
Kumbuka siri ya kuwa mtumiaji wa vyakula vya mimea ni kula aina
mbalimbali nzuri za vyakula vyenye afya.
Comments
Post a Comment
Thanks for viewing and passing through NMEE blog. Keep following the blog