UNAUUGUAJE?
Nina Uguaje?
Kuna sababu nyingi tofauti zinazo sababisha ugonjwa. Sababu yenye umuhimu sana ni mfumo
mbaya wa maisha! Kuvunja kanuni
8 za afya na kuishi katika namna isiyo ya kiafya hutuongoza kwenye shinikizo la
damu, kansa, TB, ukimwi, ugonjwa wa moyo (heart attack) mfadhaiko, kisukari na
mengine mengi.
Magonjwa mengine husababishwa na virusi, bakteria na
vijidudu vidogo vya magonjwa. Mifano
michache ni:
- Surua -
Kuharisha - Ukimwi
- Kupooza - Homa - Kichomi
- Homa ya uti wa
mgongo - TB - Upele
na mengine mengi
Magonjwa mengine husababishwa na minyoo na wadudu wanao ambukiza:
- Malaria - Kichocho - Tegu -
Michango - Michango uzi
Magonjwa mengine husababishwa na ajali. Mengine kwasababu ya miili yetu kuzeeka na
kuchakaa. Magonjwa mengine hurithiwa
toka kwa wazazi na mengine wakati wa kuzaliwa.
‘Kuna milango 3’ kwa vijidudu vya magonjwa kuingia mwilini
mwetu.
1. Mdomo: Wadudu huingia midomoni tunapokula chakula
kilicho haribika, kunywa maji mabaya na machafu na kutoosha mikono.
2. Pua:
Wadudu wa maradhi huingia kupitia puani mpaka kwenye mapafu yetu
tunapovuta hewa mbaya.
3. Ngozi na Utando wa Kamasi: Daima ngozi huzuia vijidudu isipokuwa kama kuna kidonda kilicho wazi au kuumwa na mdudu na mara
tunapo endekeza mazoea mabaya ya kutozingatia usafi kwa ujumla.
Mwili daima hushambuliwa na wadudu wa maradhi. Mtu anaugua kutegemeana na kiasi cha wadudu
walio ingia mwilini, jinsi vijidudu
vilivyo na nguvu, na mwili una nguvu kiasi gani. Mtu ambaye ni mgonjwa gonjwa na hali chakula
kifaacho huwa na kinga kidogo kwa vijidudu hivi, hivyo huugua haraka zaidi.
Comments
Post a Comment
Thanks for viewing and passing through NMEE blog. Keep following the blog