Uvutaji wa Sigara na madhara yake
Katika tumbaku
zipo sumu mbaya zaidi ya 4, 000 ambazo wana sayansi wamezipata. Kila wakati mvutaji anapovuta sigara sumu
hizi zote huenda mwilini mwake. Nyingi
za sumu hizi husababisha kansa (carcinogens).
Zinaweza kusabibisha kansa zenyewe tu.
Tumbaku inaweza kuvutwa kama sigara; kwa kiko; kutafuna; kunusa; au
kusokota! Siyo lazima ivutwe tu. Haijalishi mvutaji anatumaije tumbaku. Daima ni mbaya na yenye athari kwa afya
yako.
Moja ya sumu
mbaya ni:
1. Nikotini (Nicotine)
2. Lami
(Tar)
3. Hewa chafu
(carbon monoxide)
Nikotini: Ni dawa inayo ufanya mwili ujisikie haja ya kuvuta na kama mtumiaji
atapunguza uvutaji wake (hasa unapo anza kuacha kuvuta) mwili utaanza kuwa na
dalili ya kutaabika, kama kuumwa kichwa, mapigo ya haraka ya moyo, kutoa
jasho. Kichefuchefu, maumivu ya misuli,
n.k. ni kwasababu ya kutawaliwa na sumu hiyo mvutaji ana taabika kuiacha.
Lami: Katika tumbaku kuna nta ya lami inayo fanana na ile inayo onekana kwenye
barabara ya lami. Ni sumu zenye nguvu. Zina nguvu miongoni mwa sumu tuzijuazo. Wana sayansi wamechukua nta toka kwenye
tumbaku na kuipaka mara moja kwa panya katika kijisehemu kidogo cha ngozi yake. Panya akapata kansa baada ya muda mfupi.
Hewa Chafu (Carbon Monoxide): Ni gesi inayo patikana kwenye eksosi ya gari. Gesi hiyo hujinasa yenyewe kwenye chembechembe
nyekundu za damu hata oksijeni isisambae mwilini kunako hitajika oksijeni. Kama chembechembe nyingi zitatiliwa sana sumu
mtu anaweza akafa.
Tunaweza kufikiri
kuwa huathiri tu mapafu, lakini madhara yake huwa hata sehemu zingine za
mwili. Kuvuta kuna sababisha kansa
nyingi. Kwa mfano:
- Kansa ya midomo - Kansa ya sanduku la sauti
- Kansa ya mdomo - Kansa ya koromeo
- Kansa ya koo - Kansa ya ini
- Kansa ya kibofu cha mkojo - Kansa ya figo
- Kansa ya kizazi - Upungufu wa damu
- Kansa ya utumbo mkubwa - Kansa ya ngozi
- Kansa ya uume
Akina mama wajawazito
hujiweka katika hatari kwa watoto ambao hawaja zaliwa bado na kuwa sababishia
matatizo mengi. Watoto wanakuwa na
matatizo ya kitabia, akili kidogo, kuzaa vitoto vidogo; ugonjwa wa athma,
matatizo ya kupumua. Mama avutaye kuna
hatari ya mimba kuporomoka. Tabia za
mvutaji vilevile huathiri wale wasio vuta.
Kuvuta moshi ulio tolewa na mvutaji hukuhatarisha kwa magonjwa yote
yaliyotajwa hapo juu.
Ni vigumu kuacha
kuvuta, lakini hapa zipo njia 10 za kukusaidia kuacha kuvuta.
1. Wanapaswa wachague kuto vuta.
2. Pasiwe wa sigara zilizo fichwa mahali fulani.
3. Wafanye mazoezi ya kuvuta hewa kwa nguvu na
kupumua.
4. Mazoezi ya kila siku (kutembea).
5. Wapate usingizi wa kutosha.
6. Wawe na maji mengi mwilini (vikome 8 wastani
kwa siku).
7. Maji kwa nje – oga mara kwa mara.
8. Epuka kafeini, milo mizito, vyakula vyenye
ukali sana. Pombe isinywewe kabisa!!
9. Epuka kushirikiana na watu wanao vuta. Epuka majaribu.
10. Saidia mwili wako!!
Ellen White
aliandika zaidi karne iliyo pita kuhusu hatari ya kuvuta. Watu walifikiri ni kitu kigeni na hawa
kuelewa. Lakini, wana sayansi leo wamethibitisha kila kitu alicho kiandika muda
mrefu ulio pita.
Tumbaku si mwuaji
tu. Pia huiba maisha bora ya mtu,
huharibu furaha, husabibisha udhaifu, na hunyang’anya fedha nyingi toka kwa
jamii.
Comments
Post a Comment
Thanks for viewing and passing through NMEE blog. Keep following the blog