VILEO
Vileo
Unywaji wa pombe
huwadhuru hao wanywao magonjwa kama yale yanayo weza kuua seli za lini
(cirrhosis of the liver) pia huathiri familia na jamii kwa njia nyingi. Watu wanapolewa hupoteza uwezo wao wa kuamua
jema na hali hii husababisha huzuni mkubwa.
Heshima hupotea mara tu mtu aliyelewa kutoka kwenye hali ya kulewa na
kuona yale aliyoyatenda wakati alipo kuwa amelewa.
Vileo viko katika
kundi la kemikali ambazo ni vimiminika katika hali ya hewa ya ndani ya
chumba. Vileo viko katika jamii
nyingi. Jamii zote hizo, isipokuwa moja,
huweza kuua hata kwa kunywa kiasi kidogo tu.
Kileo aina ya Ehili (Ethyl) mwili huweza huweza kukivumilia kikiwa ni
kiasi kidogo, lakini huweza kuua mtu ikiwa katika kiwango kikubwa. Ethili ni aina ya kileo inayopatikana katika
vinywaji vyote vyenye kileo ndani kileo hupatikana ulimwenguni hote. Kila nchi na kila jamii ya watu wanayo aina
fulani ya kileo. Tunasoma juu ya kileo
katika Biblia. Mithali 20:1. Sisi kama Wakristo yatupasa kujiepusha na unywaji
wa vileo kwa kuwa hudhuru miili na akili zetu.
Watu wengi hunywa pombe kwasababu wanaamini kwamba vina ndosha matatizo
yao au kuwafanya wayasahau. Wanapotoka
kwenye hali ya kulewa huyahuta matatizo yao yako palepale! Hutokea nini wanapokunywa pombe?
Kwanza huingia tumboni. Pombe ni mojawapo katika vitu visivyo
hitaji kubadilishwa na mwili kabla ya kufyonzwa huingia katika njia ya
damu. Inaenda moja kwa moja kutoka
tumboni hadi kwenye damu. Hii humaanisha
kwamba inaenda kwenye damu haraka sana.
Kama tumbo liko tupu, kileo kuenda na kufika kwenye damu kwa dakika 2 –
3. Wakati pombe imefika tumboni hukera
mfuko wa tumbo. Kero (usumbufu) hii
husababisha mfuko wa tumbo huuma, ama vidonda vyenye mwako au kuvimba. Usumbufu huu huitwa uvimbechungu wa tumboni
(gastritis). Tumbo linapopata usumbufu
huu mara kwa mara huweza kusabibisha vidonda tumboni. Vidonda havitapona kwa muda mrefu iwapo tumbo
litaendelea kupata usumbufu huu wa pombe na vikolezo vikali vya vyakula.
Pombe
isiyofyonzwa kutoka tumboni kwenda kwenye damu, hukamia kwenye damu
taratibu. Pombe husimamisha kufyonzwa
kwa vitamini na protini kwenda kwenye damu.
Vitamini na protini hizi kuhitajika katika mwili kwa ajili ya kulamisha
na kulinda. Pombe hufyonzwa badala ya
vitamini ambavyo hutolewa nje kwa njia ya choo.
Tumbo Damu
Katika njia za damu pombe husababisha chembeche nyekundu za damu
kunata na kusinyaa. Chembechembe
nyekundu za damu luinata pamoja na kushusha au kupunguza mzunguko wa damu. Sehemu nyingi za mwili kukosa oksijeni / hewa
safi inayohitajika katika chembechembe zinazoihitaji kwa wingi na matokeo yake
hizo chembebchembe kufa. Mifupa yetu ni
kama viwanda. Hutengezwa chembechembe
hizi kwa mamilioni kila siku. Kunapokewa
na pombe katika damu, mifupa haifanyi kazi vema kutengeneza chembechembe za
damu. Hivyo mtu anaye kunywa pombe mara
kwa mara anakaribiwa na upungufu wa damu (aneamic). Chembechembe nyeupe za damu (askari)
hutiwa sumu na haiwezi kulinda miili yetu vema hutokana na magonjwa. Damu huchukua pombe hadi kwenye ini. Ini ni kama kiwanda kidogo mahali ambapo
sukari, mafuta na protini hubadilishwa na kuwa mafuta safi ambayo mwili hutumia
kwa ajili ya nguvu na kulamisha (kujenga sehemu zilizo chakaa). Pombe nayo hubadilishwa katika ini na kuwa
hewa chafu (carbon dioxide). Lakini ini
haliwezi kuondosha pombe yote; nyingine hupenya na kwenda katika sehemu zingine
za mwili na kurudi tena kwenye ini baadaye na hubadilishwa hatimaye mwili
huitoa nje. Ini huweza kutoa nje kiacha
ml 10 kwa saa. Kwa hadri mtu anapokunywa
pombe nyingi kwa muda mrefu ndivyo pia inavyo chukua muda mrefu kulolewa
nje. Pombe hutia sumu katika
chembechembe za ini, hivyo huugua na kufa.
Kwa hadiri ini linavyo jaribu kulamisha na kurudishia chembechembe
zilizokufa hukutwa zimekuwa na mahovu.
Ugonjwa huu huitwa (chirrhosis of the liver). (ugonjwa wa kuua celi za ini).
Ini Moyo
Baada ya pombe
huacha ini huhamia kwenye moyo. Moyo husukuma damu pamoja na pombe kwenye
sehemu zote za mwili pamoja na ubongo. Ni katika ubongo ambapo pombe ina madhara makubwa
zaidi. Pombe hupoozesha chembechembe za
ubongo. Hazitaweza kupeleka ujumbe
halika sehemu zingine kama ilivyokuwa awali.
Ujumbe katika ubongo huchanganyika.
Sehemu ya kwanza ya ubongo kuathirika na sehemu ya mbele. Hapa ndipo sehemu ya udhibili wetu na uwezo
wa kuwasiliana na Mungu inaathirika. Hii
ndiyo sababu ni mulimu sana kwa Mkristo anayetaka kujenga uhusiano na Mungu
asitumie pombe. Mtu anayekunywa pombe
sana hawezi kutembea vizuri kama inavyopasa; hawezi kutazama vizuri ilivyo
kawaida. Hawezi kufanya kazi yake
vema. Hawezi kupima umbali vizuri. Kila kitu anacho jaribu kukifanya huwa
kigumu. Mara pombe hufika mgongoni na
sehemu za chini ya ubongo mahali ambapo miondoko hudhibiliwa. Mlevi anaweza kupata tatizo katika kutembea
au kuasimama moja kwa moja katika hali kama hii ni hatari kuendelea
kunywa. Sehemu nyingine ya ubongo
inayoathirika ni sehemu inayodhibiti utambuzi wetu na sehemu zingine zinazo
tufanya uwe hai k.v. kupumua, mapigo ya moyo na msukumo wa damu. Pombe inapozidi huzunguka katika ubongo mtu
huweza kufa.
Iwapo mnywaji ni
mja mzito pombe huweza kuathiri mtoto tumboni.
Watoto hawa huzaliwa na matatizo mengi hawawi na akili kama akina mama
wasio kunywa pombe. Kuna madhara mengine
mengi ya pombe:
1. Msukumo mkubwa wa damu (BP).
2. Kupooza
3. Matatizo ya moyo.
4. Mafuta machafu mwilini (cholesterol).
5. Msukumo ndogo wa damu.
6. Kutofaa katika kuja miiana.
7. Upungufu wa Vitamin E.
8. Uchovu
9. Udhaifu wa mifupa.
10. Upungufu wa damu.
Wanasayansi
wamegundua kwamba kunywa pombe nyingi husababisha ubongo kuwa mdogo katika umbo,
chembechembe za ubongo zimapokufa, hazirudishwi tena. Unywaji wa pombe pia husababisha huzuni
nyumbani. Familia nyingi huvurugika kwa
ajili hii, na ajali nyingi pamoja na vifo visiyokuwa vya lazima husababishwa na
ulevi.
Ni vigumu kuacha
kunywa pombe lakini si mara zote isiwekane!
Pombe kuhitaji msaada mkubwa toka kwa ndugu na marafiki. Mungu ameahidi uwezo wake Wafilipi 4:
13. Nikazi ya Wakristo na kanisa
kuwasaidia ndugu zetu wanao tangatanga katika tatizo hili.
Comments
Post a Comment
Thanks for viewing and passing through NMEE blog. Keep following the blog