UFUGAJI WA MBUZI NA KONDOO
KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA MBUZI
NA KONDOO
Mbuzi na kondoo wanaweza
kufugwa kwa gharama nafuu na kuishi katika mazingira magumu kama ya maradhi na
ukame ikilinganishwa na ng’ombe. Kutokana na umbile lao dogo wanaweza kufugwa
katika eneo dogo na pia wanaweza kuhudumiwa na familia yenye nguvukazi na
kipato kidogo. Uzao wa muda mfupi unamwezesha mfugaji kupata mbuzi/kondoo wengi
kwa kipindi kifupi. Wanyama hao hufugwa kwa ajili ya nyama, maziwa, ngozi, sufu
na mazao mengine kwa matumizi ya familia na kuongeza kipato.
Ufugaji bora wa mbuzi na kondoo uzingatie kanuni zifuatazo:
i)
Wafugwe kwenye banda au zizi bora,
ii)
Wachaguliwe kutokana na sifa za koo/aina na lengo la uzalishaji (nyama,
maziwa au sufu),
iii)
Wapatiwe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili,
iv)
Kuzingatia mbinu za kudhibiti magonjwa kama inavyoshauriwa na
mtaalam
wa mifugo,
v)
Kuweka na kutunza kumbukumbu sahihi za uzalishaji; na
vi) Kuzalisha nyama,
maziwa au sufu yenye ubora unaokidhi mahitaji ya soko
Zizi au Banda la Mbuzi/Kondoo
Mbuzi/kondoo wanaweza
kufugwa katika mifumo ya huria, shadidi na kwa kutumia njia zote mbili. Zizi
hutumika katika mfumo huria ambapo mbuzi/kondoo huchungwa wakati wa
mchana na kurejeshwa zizini wakati wa usiku.
Zizi bora ni lile lenye sifa zifuatazo:
• Lililo
imara linaloweza kumkinga mbuzi/kondoo dhidi ya wanyama hatari na wezi,
• Lililojengwa
mahali pa mwinuko pasiporuhusu maji kutuama,
• Ukubwa
wa zizi uzingatie idadi na umri wa mifugo. Ni vema mbuzi/kondoo
watengwe
kulingana na umri wao; na •Liruhusu usafi kufanyika kwa
urahisi.
Pale ambapo mbuzi/kondoo
wanafugwa kwa mfumo wa shadidi hufugwa katika banda wakati wote. Banda bora la mbuzi/kondoo linatakiwa kuwa
na sifa zifuatazo:
• Imara,
lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa hatarishi kwa
mfano jua kali, upepo, baridi na mvua pamoja na wanyama hatari,
• Lenye
mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika kwa urahisi,
• Lijengwe
sehemu isiyoruhusu maji kutuama na liwe mbali kidogo na nyumba ya kuishi watu.
Pia ujenzi uzingatie mwelekeo wa upepo ili hewa kutoka bandani isiende kwenye
makazi,
• Liwe na
sakafu ya kichanja chenye urefu wa mita 1 kutoka ardhini (Kwa banda la mbuzi),
• Liwe na
sehemu ya kuwekea chakula, maji na mahali pa kuweka jiwe la chumvichumvi; na
• Liwe na
vyumba tofauti kwa ajili ya majike na vitoto, mbuzi/kondoo wanaokua,
wanaonenepeshwa na wanaougua.
Vifaa vya Kujengea na
Vipimo vya Banda
Inashauriwa
banda la mbuzi/kondoo lijengwe kwa kutumia vifaa vinavyopatikana kwa urahisi
katika eneo husika. Ukubwa wa banda utategemea idadi ya mbuzi/kondoo wanaofugwa humo na ukubwa wa
umbo
• Paa
lijengwe kwa kutumia vifaa kama miti, mbao, na kuezekwa kwa nyasi, makuti,
majani ya migomba, mabati au hata vigae kwa kutegemea uwezo wa mfugaji,
• Kuta zijengwe
kwa kutumia mabanzi, mbao, nguzo, wavu wa waya, fito na matofali. Kuta ziwe
imara zinazoruhusu hewa na mwanga wa kutosha. Mlango uwe na ukubwa wa sentimita
60 x 150,
• Sakafu
inaweza kuwa ya udongo au zege. Sakafu ya kichanja inaweza kujengwa kwa kutumia
miti, fito, mianzi, mbao au mabanzi na iweze kuruhusu kinyesi na mkojo kupita.
Chumba cha majike na vitoto kiwe na nafasi ya sentimita 1.25 kati ya papi na
papi, fito na fito au mti hadi mti. Chumba cha mbuzi/kondoo wakubwa iwe
sentimita 1.9 kati ya mbao na mbao.
Uchaguzi wa Mbuzi/Kondoo
wa Kufuga Madhumuni ya kuchagua mbuzi au
kondoo wa kufuga ni kuboresha uzalishaji na kuendeleza kizazi bora. Kuna aina
nyingi za mbuzi/kondoo wanaoweza kufugwa kulingana na mazingira na mahitaji ya
mfugaji. Uchaguzi hufanyika kwa kuangalia umbile, uzalishaji na kumbukumbu za
wazazi kama vile umbo kubwa, ukuaji wa haraka, uwezo wa kutunza vitoto na kutoa
maziwa mengi. Mbuzi wanaofaa kwa ajili ya maziwa ni aina ya na pamoja na
chotara wao
Mbuzi wanaofaa kwa ajili
ya nyama ni na chotara wao, mbuzi wa
asili kama vile , Newala na Ujiji. Mbuzi aina ya Malya wanafaa
kwa ajili
ya nyama na maziwa.
Aidha, kondoo aina ya (BHP),
nao wanafaa kufugwa kwa ajili ya nyama.
na hufugwa kwa ajili ya
sufu, wakati na
hufugwa kwa ajili ya nyama na sufu. Hapa Tanzania kondoo wanaopatikana
kwa wingi ni , Masai Red Dopper na kondoo wengine wa asili
.
Mbuzi/kondoo jike wanaofaa kwa ajili ya kuzalisha maziwa na nyama
wawe na sifa zifuatazo:-
• Historia
ya kukua upesi, kuzaa (ikiwezekana mapacha) na kutunza vitoto vizuri,
• Umbo la
mstatili linaloashiria utoaji wa nyama nyingi; na • Asiwe na
ulemavu wa aina yoyote
Sifa za Ziada kwa Mbuzi
wa Maziwa • Awe na
miguu ya nyuma iliyo imara na iliyonyooka na yenye nafasi kwa ajili ya
kiwele; na
• Awe na
kiwele kikubwa na chuchu ndefu zilizokaa vizuri
Sifa za Dume Dume
bora awe na sifa zifuatazo:-
• Miguu
iliyonyooka, imara na yenye nguvu,
• Asiwe na ulemavu wa aina
yoyote,
• Mwenye uwezo na nguvu ya
kupanda; na
• Mwenye
kokwa mbili zilizo kaa vizuri na zinazolingana
Utunzaji wa Vitoto vya
Mbuzi/Kondoo
Utunzaji huanza mara tu
baada ya kuzaliwa. Mfugaji ahakikishe:•
Kitoto cha mbuzi/kondoo
kinapata maziwa ya mwanzo (dang’a) ndani ya masaa 24 tangu kuzaliwa na kwa
muda wa siku 3,
• Kama
kinanyweshwa maziwa, kipewe lita 0.7- 0.9 kwa siku. Maziwa haya, ni muhimu kwani yana viinilishe na
kinga dhidi ya magonjwa,
•Iwapo
mama hatoi maziwa au amekufa, inashauriwa kutengeneza dang’a; mbadala
au kama kuna mbuzi/kondoo mwingine aliyezaa anaweza kusaidia kukinyonyesha
kitoto hicho,
• Kitoto
cha mbuzi/kondoo kiendelee kunyonya kwa wiki 12 - 16. Wiki 2 baada ya kuzaliwa,
pamoja na maziwa, kianze kupewa vyakula vingine kama nyasi laini na chakula cha
ziada ili kusaidia kukua kwa tumbo. Aidha, kipewe maji wakati wote,
• Vyombo
vinavyotumika kulishia vinakuwa safi muda wote,
• Kitoto
cha mbuzi/kondoo kiachishwe kunyonya kikiwa na umri wa miezi 3 hadi 4
kutegemea afya yake; na
• Vitoto vipatiwe
kinga na tiba ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam
wa mifugo.
Matunzo Mengine Utambuzi
Mbuzi huwekewa alama ili
atambulike kwa urahisi na kuwezesha utunzaji wa kumbukumbu zake. Shughuli hii
hufanyika kwa mbuzi/kondoo akiwa na umri wa siku 3 - 14. Njia zitumikazo ni
pamoja na:
• Kuweka
alama sikioni kwa kukata sehemu ndogo ya sikio,
• Kumpa jina kwa wafugaji
wenye mbuzi wachache,
• Kumvisha
hereni ya chuma au plastiki yenye namba kwenye sikio,
• Kumvalisha
mkanda wenye namba shingoni; na
• Kuweka
namba kwa kuunguza sehemu ya ngozi ya mbuzi. Pale mfugaji anapotumia njia hii
inashauriwa aweke alama kwenye eneo ambalo halitaathiri ubora wa ngozi
Kuondoa vishina vya pembe Mbuzi/kondoo
aondolewe vishina vya pembe akiwa na umri kati ya siku 3 hadi 14.
Visipoondelewa hukua na kusababisha kuumizana na kuhitaji nafasi kubwa kwenye
banda. Kazi hii ifanywe na mtaalam wa mifugo.
Kuhasi Vitoto
vya mbuzi/kondoo ambavyo havitatumika kwa ajili ya kuendeleza kizazi vihasiwe kabla
ya kufikia umri wa miezi 3. Kazi hii ifanywe na mtaalam wa mifugo.
Utunzaji wa Mbuzi/Kondoo
wa Miezi 4 - 8 Mbuzi wa
miezi 4 mpaka 8 ni wale ambao wameacha kunyonya mpaka umri wa kupandishwa kwa
mara ya kwanza. Mbuzi wa umri huu wana uwezo wa kula aina mbalimbali za malisho
kama nyasi, mikunde, miti malisho na mabaki ya mazao wakati kondoo hupendelea
zaidi nyasi fupi. Wakati wa kiangazi huhitaji kupatiwa chakula cha ziada au
kupewa pumba za nafaka mbalimbali, mashudu ya alizeti, pamba na dengu, majani
ya mikunde yaliyokaushwa, madini na vitamini.
Katika ufugaji huria ni
vema kuzingatia idadi ya mbuzi/kondoo inayoweza kuchungwa katika eneo, aina na
hali ya malisho.
Ili mbuzi/kondoo aweze
kukua na kufikia uzito wa kuchinjwa/kupevuka mapema, mfugaji anapaswa kufuata
kanuni za ufugaji bora zifuatazo:
• Kumpatia
vyakula vya ziada kwa muda wa miezi 2 mfululizo kiasi cha kilo 0.2 –
0.7 kwa
siku kuanzia anapoachishwa kunyonya,
• Kumpatia
dawa ya kuzuia minyoo kila baada ya miezi 3 na kutoa kinga za
magonjwa mengine kama
itakavyoshauriwa na mtaalam wa mifugo,
• Kuchanja
na kuogesha ili kuzuia magonjwa mbalimbali, • Kukata kwato mara
zinapokuwa ndefu; na • Kuhasi madume yasiyotumika kuzalisha.
Umri wa Kupandisha
Mbuzi/Kondoo Mbuzi/kondoo wakitunzwa
vizuri wanaweza kupandishwa wakiwa na umri wa miezi 8 hadi 12 kwa mbuzi/kondoo
walioboreshwa na miezi 18 hadi 24 kwa mbuzi wa asili kutegemea afya yake. Hata
hivyo, inashauriwa wapandishwe wanapofikia uzito wa kilo 12 au zaidi na wasipandishwe
mbuzi/kondoo wa ukoo mmoja.
Dalili za joto Mfugaji
anashauriwa asimpandishe jike kabla hajafikisha umri wa kupandwa wa miezi 8
hadi 12 kwa mbuzi/kondoo walioboreshwa na miezi 18 hadi 24 kwa mbuzi wa
asilihata kama ataonyesha dalili ya kuhitaji dume. Mbuzi/kondoo aliyezaa
anaweza kupandishwa siku 30-60 baada ya kuzaa. Mbuzi/kondoo aliyeko kwenye joto
huonyesha dalili zifuatazo:-
• Hutingisha/huchezesha
mkia,
• Hupanda na kukubali
kupandwa na wengine,
• Hutoa
ute mweupe ukeni,
• Huhangaika mara kwa mara
na kupiga kelele,
• Hufuata
madume,
• Hamu ya
kula hupungua,
• Hukojoa mara kwa mara,
• Uke
huvimba na huwa mwekundu kuliko ilivyo kawaida; na
• Kwa
mbuzi anayekamuliwa hupunguza kiwango cha maziwa
Mbuzi/kondoo apelekwe kwa
dume mara tu dalili za joto zinapoonekana kwani joto hudumu kwa wastani wa siku
2 (saa 48). Chunguza tena dalili za joto baada ya siku 19 hadi 21 na kama
dalili hazitaonekana tena kuna uwezekano mkubwa
kuwa mbuzi/kondoo amepata
mimba. Mfugaji apange msimu mzuri wa mbuzi/kondoo kuzaa. Msimu mzuri ni mara
baada ya mvua.
Utunzaji wa Mbuzi/Kondoo
Mwenye Mimba Kwa kawaida mbuzi/kondoo hubeba
mimba kwa muda wa miezi 5. Utunzaji wa mbuzi/kondoo mwenye mimba ni muhimu
kwani ndiyo chanzo cha kupata vitoto vyenye afya bora. Mfugaji anashauriwa
kufuata kanuni zifuatazo:
• Apatiwe
vyakula vya ziada kilo 0.2 – 0.7 kwa siku ili kutosheleza mahitaji yake na
kitoto kinachokua tumboni,
• Apatiwe
nyasi, miti malisho na mikunde mchanganyiko kilo 1.8 – 2.5 kwa siku.
Dalili za Mbuzi/Kondoo
Anayekaribia Kuzaa
• Huhangaika
kwa kulala na kuamka mara kwa mara,
• Sehemu ya nje ya uke
hulegea,
• Hujitenga
na kundi na hutafuta sehemu kavu na yenye kivuli,
• Hupiga
kelele; na
• Hutokwa
na ute mzito ukeni.
Mfugaji akiona dalili
hizi anashauriwa asimruhusu mbuzi/kondoo kwenda machungani, bali amtenge kwenye
chumba maalum, ampatie maji ya kutosha na kumuandalia sehemu ya kuzalia.
Utunzaji wa Mbuzi/Kondoo
Anayenyonyeshan Mbuzi/kondoo anayenyonyesha
huhitaji chakula kingi zaidi ili kukidhi mahitaji ya mwili na kuzalisha maziwa
kwa ajili ya kitoto/vitoto. Pamoja na nyasi, mikunde na majani ya miti malisho
kilo 1.8 – 2.5 kwa siku ni muhimu apewe chakula cha nyongeza kilo 0.3 – 0.8 kwa
kila lita ya maziwa inayoongezeka baada ya lita 2 na maji safi, salama na ya
kutosha wakati wote.
Taratibu za Kuzingatia
Katika Ukamuaji wa Mbuzi wa Maziw
Lengo la ufugaji wa
mbuzi/kondoo wa maziwa ni kupata maziwa mengi, safi na salama pamoja na mazao
yatokanayo na maziwa. Mambo muhimu ya kuzingatia ni:-
• Sehemu
ya kukamulia iwe safi na yenye utulivu,
• Mbuzi/kondoo awe na afya
nzuri, msafi, na kiwele kioshwe kwa maji safi ya
uvuguvugu,
• Mkamuaji
asibadilishwe badilishwe awe msafi, mwenye kucha fupi na asiwe
na
magonjwa ya kuambukiza,
• Vyombo vya kukamulia viwe
safi; na
• Maziwa ya mwanzo kutoka
kila chuchu yakamuliwe kwenye chombo
maalum (strip cup) ili
kuchunguza ugonjwa wa kiwele.
Utunzaji wa Dume Bora
la Mbegu Dume
bora la mbegu ni muhimu litunzwe ili liwe na uwezo wa kutoa mbegu bora, kupanda
na kuzalisha. Dume bora huanza kupanda akiwa na umri kati ya miezi.8 10 kwa
mbuzi walioboreshwa. Katika msimu wa kupandisha dume moja liruhusiwe kupanda
majike 40 hadi 50. Aidha, inashauriwa madume wenye umri wa miezi 8 – 9
waruhusiwe kupanda majike ambao ndio mara ya kwanza kupandwa.
Dume apatiwe:
• Malisho ya kutosha na
vyakula vya ziada kiasi kisichopungua kilo 0.2 – 0.7 kwa siku
na maji ya kutosha,
• Majani
ya miti malisho, mikunde na nyasi mchanganyiko na mabaki ya mazao;
na
• Kilo
0.45 hadi 0.9 za chakula cha ziada za nyongeza kwa siku kulingana na uzito
wake na wingi wa majike anayopanda.wiki 2 kabla na baada ya kuanza kupanda.
Matunzo Mengine Kukata
Mkia
Kumnyoa Kondoo wa Sufu Sufu
hunyolewa wakati kondoo akiwa hai au amechinjwa. Kwa kawaida hunyolewa miezi 6 hadi mwaka 1
ambapo sufu huwa imefikia urefu wa sentimita 15 – 20. Vifaa vinavyotumika ni
pamoja na mikasi au visu maalum. Uangalifu unahitajika wakati wa kunyoa ili
ngozi ya kondoo isiharibike. Unyoaji ufanyike wakati wa kiangazi na siyo wakati
wa mvua, kondoo akiwa na mimba au kipindi cha majani kutoa mbegu.
Udhibiti wa Magonjwa ya
Mbuzi na Kondoo Magonjwa
husababishwa na vimelea jamii ya virusi, bakteria, protozoa na riketsia.
Magonjwa mengine husababishwa na upungufu wa viinilishe, vitamini na protini.
Dalili za mbuzi/kondoo mgonjwa ni pamoja na:-
Manyoya husimama,
Kuzubaa, kusinzia, kukohoa na kupiga chafya, Kukosa hamu ya kula
na kunywa maji,
Kujitenga na kundi,
Kuvimba taya la chini,
Kupumua kwa shida,
Kutokwa na machozi na makamasi, Kuwa na upele au uvimbe kwenye
sehemu ya mwili; na
Kutupa mimba.
• Hatua za
haraka za kumuona mtaalamu wa mifugo zichukuliwe iwapo baadhi ya dalili hizi
zitaonekana,
• Mbuzi na
kondoo wachanjwe dhidi ya magonjwa ya homa ya maapafu. Ugonjwa huu ni hatari
sana na huenea kwa njia ya hewa na unaweza kusababisha vifo kati ya asilimia
60-100,
• Kila
baada ya miezi 6 mifugo ipatiwe kinga dhidi ya ugonjwa wa miguu na midomo na
magonjwa mengine kama Kimeta, bonde la ufa, kutupa mimba na chambavu (BQ)
zitolewe kulingana na ushauri wa mtalaam wa mifugo,
• Kama
kuna wanyama walioathirika watengwe kwenye kundi, wasisafirishwe au kuuzwa,
• Mbuzi/kondoo
wapatiwe dawa ya
minyoo. Vitoto vya
mbuzi/kondoo vipatiwe dawa ya minyoo vinapofikia umri wa mwezi 1.
viendelee kupatiwa
dawa ya minyoo kila mwezi
hadi vinapofikia miezi 5 na baada ya hapo vipatiwe dawa ya minyoo kila baada ya
miezi 3 - 4; na
• Zingatia
usafi wa banda ili kuwakinga na ugonjwa wa kuharisha na kuharisha damu na
magonjwa mbalimbali.
Utunzaji wa Kumbukumbu za
Mifugo Kuweka
kumbukumbu za mifugo ni muhimu katika uzalishaji kwa ajili ya kutambua kosaafu,
gharama za utunzaji na faida. Pia, humsadia mfugaji kufanya maamuzi katika
uendelezaji wa ufugaji wake. Mtalaamu wa mifugo pia anaweza kutumia kumbukumbu
hizi ili kumsaidia mfugaji kuboresha ufugaji wake.
Kumbukumbu muhimu
zinazohitajika kutunzwa ni:-
• Kumbukumbu
za idadi na ukuaji wa wanyamawaliopo, jinsi zao, uzito wa mbuzi/kondoo
kwa kila mwezi
ili kufuatilia ukuaji
wake, tarehe ya
kuachishwa
kunyonya na idadi ya waliouzwa,
• Kumbukumbu ya uzazi
zinazoonyesha tarehe ya kuzaliwa, namba yake, jinsi
yake,
aina (breed), namba ya dume/jike, na uzito wa kuzaliwa,
• Kumbukumbu
za upandishaji zinazoonyesha namba ya
mbuzi/kondoo
anayepandwa, tarehe ya
joto na ya kupandwa, namba ya dume lililotumika kupanda, tarehe ya joto la pili
kama atarudia na tarehe ya kuzaa,
• Kumbukumbu
za chanjo na matibabu zinazoonyesha namba ya mbuzi/kondoo, tarehe ya matibabu,
aina ya chanjo au ugonjwa, dawa iliyotumika, idadi ya waliokufa na waliopona na
jina la mtaalam aliyetibu,
• Kumbukumbu
za maziwa zinazoonyesha namba ya mbuzi/kondoo, tarehe ya kuzaa, kiasi cha
maziwa kwa siku, na kiasi cha maziwa kwa kipindi chote cha kukamuliwa, tarehe
ya kuacha kukamua na idadi ya siku alizokamuliwa,
• Kumbukumbu
za mapato na matumizi zinazoonyesha mapato na matumizi, vitu vilivyouzwa au
kununuliwa kwa siku, kiasi cha fedha unachokuwa
nacho
kila wakati, kiasi cha fedha unachodai na kudaiwa.
Comments
Post a Comment
Thanks for viewing and passing through NMEE blog. Keep following the blog