Kuanzia sura hii ya tatu na sura kadhaa zitakazofuata zitahusu wanawake baadhi waliotajwa majina yao katika Biblia. Hivyo, wanawake waliotajwa majina yao katika Biblia, nimejaribu kuwagawa kwa kufuata mpangilio wa herufi ya kwanza katika majina yao hadi ya mwisho. Kwa hiyo, unapopitia kila jina la mwanamke kunamambo mengi ya kujifunza katika maisha ya kiroho na ya kawaida, aidha, maana ya jina, tabia, matendo na imani. Abia Jina hili linamanisha “matakwa ya Mungu” . Wakati mwingine jina hili humanisha Baba yangu ni Yehova. Mwanamke huyu alikuwa mke wa Hesroni, aliyemzalia mumewe mtoto wa kiume aitwaye Ashuri, babaye Tekoa. “Tena, baada ya kufa kwake Hesroni huko Kalebu-Efrata, ndipo Abia, mkewe Hesroni, alipomzalia Ashuri, babaye Tekoa” (1Nyakati 2:24). Abiya Mwanamke huy...
Comments
Post a Comment
Thanks for viewing and passing through NMEE blog. Keep following the blog