CHANGAMOTO KATIKA TASISI
FUNGU: Mwanzo 16:6; Naye Abram akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake. 1.0 UTANGULIZI: Nawasalimu katika jina la Bwana wetu Kristo; Bwana Yesu Asifiwe binti na wana za Mungu. kwan Somo la leo linatoka katika kitabu cha Mwanzo 16:1-15 , na Mwanzo 21:1-21 . Mada itajikita katika tasisi iitwayo familia. Swali: Kwa nini familia iitwe tasisi? Tusome kwanza Mwanzo 16:1-15 , na Mwanzo 21:1-21 kisha tuanze somo. 2.0. KIINI CHA SOMO: Aya zote tulizosoma zinamhusu familia ya Abram ambaye ni Ibrahimu pamoja na mkewe Sarai ambaye ni Sara. Familia ya Ibrahimu na Sarai ilikuwa na mjakazi (mfanyakazi au dada wa kazi) aitwaye Hajiri mwenye asili ya Misiri. Familia hii ya Abram na Sarai haikuwa na mtoto, toka wameoana. Kadri miaka iliposonga, Serai akamshauri Abram mumewe azae na kijakazi aitwaye Hajiri (Mwanzo 16:2-4). Hajiri alijifungua mtoto wa kiume aliyeitwa Ishimael