Posts

How to write resignation letter | Learn to Write Resignation letter in E...

Image

FB VIDEO SD 1509640586758

Image

10 Mistakes Most Young People Make & Regret Later in Life

Image

How to Know Your Life Purpose in 5 Minutes Adam Leipzig at TEDxMalibu

Image

WOMEN MUST WATCH by Dr Myles Munroe YouTube 360p

Image

WOMEN MUST WATCH by Dr Myles Munroe YouTube 360p

Image

MWIKO KUVUNJIKA CHUNGUNI

Salamu nawasalimu, Amani nawatakia, Niishikapo kalamu, swali nawaulizia, Si fumbo la kitalaamu, ni hoja nawapangia, Umevunjika chunguni, mwiko wangu, mwiko wangu! Kupika ninavyopika, nikipika vinalika, Vinalika na kulika, na vidole kulambika, Mwiko ninaposhika, Vitu vinakorogeka, Umevunjika chunguni, mwiko wangu, mwiko wangu! Viungo nikiongeza, chumvi na mdalasini, Na ndimu nikinyunyiza, kolienda na komuni, Utamu nikikoleza, harufu tamu chunguni, Umevunjika chunguni, mwiko wangu, mwiko wangu! Sasa nashindwa kupika, mwiko umevunjikia, Nilipokuwa napika, chunguni kumegukia, Mwiko wangu wa hakika, mwingine sitamania, Umevunjika chunguni, mwiko wangu, mwiko wangu! Maana yake ni nini, mwiko kunivunjikia, Niambieni asilani, mizimu imechukia? Nichinje mnyama gani, mkosi kufukuzia, Umevunjika chunguni, mwiko wangu, mwiko wangu! Nawauliza watani, na watani wa watani, Hili jambo ni la nini, kuvunjikia chunguni, Kama ni zuri ni nini, niambieni jamani, Umevunjika chunguni, mwiko wangu

SWEET AND BEAUTY SONG

MATHS' GENIUS

A LITTLE KENYAN GIRL - AN AUTHOR OF THREE BOOKS

A TANZANIA GIRL AT UN

MY DEDICATION TO THE PRESIDENT DR. J.P.M

Image

SOMO: UASI WA KANUNI YA KIROHO TUSIOUJUA:

FUNGU: WAEFESO 5:15-21 “ 15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati kwa maana zama hizi ni za uovu. 17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya bwana. 18 Tena msilewe Kwa mvinyo, ambamo mnaufisadi; Bali mjazwe Roho; 19 mkisemezana Kwa zaburi Na tenzi na nyimo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana Yesu Kristo; 21 hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo. 1.0 UTANGULIZI: 1.1. Katika maisha yangu ya kiroho; Nahau zifuatazo zimenifunda: 1)    Kama hujui mahala unapoelekea uwapo safarini, njia yoyote miongoni mwa nyingi itakuchagulia uelekeo na Kama hujishughulishi kujua unakoelekea, njia haiwezi kukuchagulia uelekeo sahihi uutakao. 2)    Eneo lenye giza zaidi kuliko maeneo yote katika mshumaa lipo chini ya mshumaa. 3)    Debe lililo tupu ndilo lipigalo sana kele. 4

CHANGAMOTO KATIKA TASISI

FUNGU: Mwanzo 16:6; Naye Abram akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake. 1.0 UTANGULIZI: Nawasalimu katika jina la Bwana wetu Kristo; Bwana Yesu Asifiwe binti na wana za Mungu. kwan Somo la leo linatoka katika kitabu cha Mwanzo 16:1-15 , na Mwanzo 21:1-21 . Mada itajikita katika tasisi iitwayo familia. Swali: Kwa nini familia iitwe tasisi? Tusome kwanza Mwanzo 16:1-15 , na Mwanzo 21:1-21 kisha tuanze somo. 2.0. KIINI CHA SOMO: Aya zote tulizosoma zinamhusu familia ya Abram ambaye ni Ibrahimu pamoja na mkewe Sarai ambaye ni Sara. Familia ya Ibrahimu na Sarai ilikuwa na mjakazi (mfanyakazi au dada wa kazi) aitwaye Hajiri mwenye asili ya Misiri. Familia hii ya Abram na Sarai haikuwa na mtoto, toka wameoana. Kadri miaka iliposonga, Serai akamshauri Abram mumewe azae na kijakazi aitwaye Hajiri (Mwanzo 16:2-4).   Hajiri alijifungua mtoto wa kiume aliyeitwa Ishimael

TAMTHILIYA YA KWELI

FungU: Ayubu 42:10 “Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Auyubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza”. 01: UTANGULIZI Hapa duniani zipo tamthiliya lukuki zilizoandaliwa na wanadamu kwa njia za maigizo katika majukwaa ya sanaa; maandishi katika vitabu, majarida na magazeti; sauti katia redio na katika sinema. Tamthilia hizo kwa sehemu kubwa zina sifa za kufanana kimuundo wake na zinatofautiana kimtindo (yaani namna ilivyowasilishwa tamthiliya hiyo). Muundo wa tamthiliya hizi unasifa kuu nne: 1.      Tamthiliya ya aina yoyote lazima iwe na majibishano (yaani daiolojia) 2.      Tamthiliya lazima iwe na wahusika ( wahusika wakuu (aweza kuwa nguli), wahusika wadogo (bapa au mviringo), pamoja na mtoa maelezo au mfafanuzi (maranyingi huwa ni sauti). 3.      Tamthiliya lazima iwe katika muundo wa pembe tatu, japo si tamthiliya zote (yaani socretic plays): Mwanzo (maisha mazuri na kuibuka kwa mgogoro); Kilele