Maisha ni kama Shamba

“Maisha ni kama Shamba, wapo ambao wazazi wao walifanikiwa kununua shamba hili na wao kwa juhudi wazijuazo wao walifanikiwa kung’oa visiki, kulima, kupanda mbegu na kupalilia na kisha sasa mazao yanamea na wao wananyweshea. Watoto au vijana wenye
wazazi wa namna hii huwa hawana kazi sana,wao huwapokea wazazi wao mpira wa maji na kuanza kumwagilia. Wapo wale ambao wazazi wao walifanikiwa kununua shamba lakini walishindwa kulihudumia na
sasa wao ndio huenda kuanza upya, kazi yao huwa ngumu sana kwani hutakiwa kuanza mwanzo, hawa ni wale waliobahatika tu kupata elimu lakini kwao hakuna uwezo. Ewe ambaye kwenu mmefanikiwa usikatishe ndoto ya mwenzio kwa uwezo wa mzazi wako,USITUMIE PESA KAMA FIMBO YA KUMCHAPIA MWENZIO”

Comments

Popular posts from this blog

MAJINA YA WANAWAKE KATIKA BIBLIA ‘A’ HADI ‘Z’

SOMO: MADHARA YA KUKATAA KUMTII MUNGU

MFANO WA MPANGO KAZI