UTAMBUE MOYO WAKO

“Unaweza kuwa si wa kwanza kwake, wala wa
mwisho kwake, Aliwahi kupenda kabla na anaweza
kupenda tena. Lakini kama anakupenda wewe,
unajali nini tena? Yeye si mkamilifu, na wewe pia
si mkamilifu, na wote wawili hamuwezi kuwa
wakamilifu pamoja, lakini kama anaweza
kukufanya ucheke, anakunfanya ufikiri mara mbili
na anakiri kuwa yeye ni binadamu a anatenda
makosa basi mshikilie yeye na mpe kwa kadiri
uwezavyo. Anaweza kuwa hakufikirii kila sekunde
katika siku, lakini atakupa sehemu ya utu na mwili
wake anayojua utaivunja YANI MOYO WAKE.
Usimbadilishe, usimchambue, usitegemee makubwa
zaidi ya yale awezayo kukupa au yale anayomudu.
Tabasamu pale akufurahishapo, muambie pale
anapokukasirisha, ana ummis pale anapokuwa
hayupo. HAPO UTAKUWA NA FURAHA YA MAPENZI NA WASIWASI WA MAPENZI UTAONDOKA”


“Hakuna haja ya kukata tamaa na kujiona kuwa huna thamani katika mapenzi yako kwakuwa tu kila mahusiano uanzishayo hayawi na mwisho
mzuri au ulioutarajia, maisha ya mapenzi ni maisha dhalimu muda mwingine. Unaweza
kukutana na mtu sahihi katika muda usio sahihi,na unaweza kukutana na aliyesahihi katika muda usio sahihi. Unachotakiwa kufanya si kukata tamaa bali kuwa makini na muda na unaokutana nao. Kila mtu anapacha wake hapa duniani,inapotokea umekutana na pacha wa mtu, ndipo shida na matatizo huanzia hapo. ATAKUJA MTU KATIKA MAISHA YAKO ATAKAYEKUFANYA UGUNDUE KWANINI HUKUDUMU NA ULIOACHANA NAO”


“Kwa mwanamke kuwa na furaha katika mapenzi
unahitaji kupata mtu mnayependana,,mtu
atakayejali sana furaha yako kuliko yake,,mtu
atakayekuwa wa mwisho kukufanya ulie,,mtu
ambaye atakupa kila unachostahili, atakayejitolea
muda wa maisha yake kuishi na wewe kama
mkewe,,mkweli, muaminifu,,mtu asiye na tamaa,
mtu makini katika kufikiri na ajuaye anachohitaji
mwanamke,,mtu pekee ambaye atajisikia fahari
kuwa na wewe popote na kulitetea penzi lenu kwa
namna yoyote ile,,MWANAUME ANAYEKUPENDA
KULIKO WEWE UNAVYOMPEDA. Hawapatikani
kirahisi ila tu ni KAMA WEWE NAWE UTAKUWA
UNAVIGEZO UVITAKAVYO….KUWA SEHEMU YA
MABADILIKO UYATAKAYO”



“Nitakupenda siku zote. Pale nywele zangu
nyeusi zitakapokuwa nyeupe bado nitakupenda.
Pale ngozi yako laini ya usichana itakapokaliwa
na ngozi iliyojikunja ya uzee bado nitahitaji
kukushika. Pale sura yako itakapokuwa na
makunyanzi unapotabasamu bado nitakupenda,
pale ambapo kila chozi ulilolitoa litakuwa
limeacha alama kwenye sura yako mimi
nitabaki kukupenda. Nitakuthamini daima, yote
ni kwakuwa nilikuwa na wewe wakati wote
ukipitia hayo. Nitashiriki maisha yako,
nitashiriki machozi yako, na nitakupenda mpaka
pale pumzi itakapochoka kuishi ndani yako au
ndani yangu. Nilikupenda kabla na nitakupenda
baada. Pale utakapoamua kwenda na kusema
mimi sio faraja yako nitakuwa tayari
kukuangalia ukiondoka kwakuwa nia yangu ni
wewe uwe na furaha hata bila mimi. Kila mtu
anahitaji faraja na upendo, niko tayari
kukupenda kama nijipendavyo. Siku zote, miaka
yote NITAKUPENDA, na hiyo ni kwakuwa tu
KUKUPENDA WEWE NI AMANI YA MOYO
WANGU.” 

Comments

Popular posts from this blog

MAJINA YA WANAWAKE KATIKA BIBLIA ‘A’ HADI ‘Z’

SOMO: MADHARA YA KUKATAA KUMTII MUNGU

MFANO WA MPANGO KAZI