Wewe ungemuacha nani?


Top of Form
Siku moja katika darasa la jioni la watu wazima, mwalimu wa saikolojia aliingia darasani na kuwaambia wanafunzi;

"Nataka tucheze mchezo, mtu yeyote yule naomba ajitolee aje hapa mbele"

Mwanamke aitwae Cathy akatoka mbele. Mwalimu akamwambia aandike majina 30 ubaoni ya watu ambao anadhani ni wa muhimu katika maisha yake.

Cathy akaandika majina ya wanafamilia yake yaani mumewe na mwanae, ndugu, majirani na marafiki zake.

Mwalimu akamwambia Cathy afute majina matatu ambayo anadhani kwake sio ya muhimu sana kuzidi mengine. Cathy akafuta majina ya marafiki zake watatu.

Mwalimu akamwambia Cathy afute tena majina matano zaidi, Cathy akafuta majina ya majirani zake watano.

Hii iliendelea mpaka alipobakiwa na idadi ya watu wanne tu katika ubao. Haya yalikuwa majina ya wazazi wake, mumewe na mtoto wake wa pekee.

Darasa zima wakabaki kimya, baada ya kugundua kuwa huu sio mchezo wa Cathy peke yake sasa.

Mwalimu akamwambia Cathy afute majina mengine mawili kati ya yale manne yaliyobaki. Ulikuwa uamuzi mgumu mno kwa Cathy. Bila hiyari akafuta majina ya wazazi wake.

"Futa jingine zaidi tafadhali" mwalimu alimwambia.

Cathy akaishiwa pozi, na huku mikono ikimtetemeka na machozi katika macho yake akafuta jina la mwanae wa pekee. Na kubakiza jina la mume wake, Cathy alilia mno!!!

Mwalimu akamwambia Cathy aende akakae. Baada ya muda kidogo mwalimu akamuuliza Cathy "kwanini mume wako? Wazazi wako ndio waliokulea na kukuza, Mtoto wako ndio huyo tu mmoja uliyenae!! Na unaweza ukapata mume mwingine!!! Kwanini??"

Darasa likawa na ukimya wa hali ya juu, kila mmoja akitamani asikie ni nini Cathy atajibu.

Cathy kwa ujasiri na utulivu akainuka na kusema, "siku moja wazazi wangu watatangulia kufariki (Mwenyezi Mungu anisamehe), mtoto wangu pia ataondoka pale atakapokua mkubwa kwenda kuanzisha familia yake.

Mtu nitakayebaki nae kumaliza nae maisha hasa uzeeni ni mume wangu tu!! Yeye ndiye niliyeunganishwa nae na Mungu, mimi na yeye ni mwili mmoja."

Wanafunzi wote wakasimama na kumpigia makofi kwa kushare nao ukweli na msimamo wa maisha yake.

Huu ulikuwa uamuzi wa Cathy, yeye kwa mtizamo wake alimchagua mumewe. Je wewe ungechagua nani?


Comments

Popular posts from this blog

MAJINA YA WANAWAKE KATIKA BIBLIA ‘A’ HADI ‘Z’

SOMO: MADHARA YA KUKATAA KUMTII MUNGU

MFANO WA MPANGO KAZI