TAJI ZA WASHINDI.
Wimbo # 58: Zitakuwa nyota taijini
Fung kuu: 2Timotheo 4:7-8 “7Nimevipiga vita
vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; 8Baada
ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana mhukumu mwenye haki, atanipa siku
ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake”
UTANGULIZI Dunia imejaa mashindano kila kona ya nyanja zote
za maisha. Kama mashindano ya: mbio za
magari, riadha, farasi, ng’ombe, kuku, kuvuta kamba au mashindano ya ubingwa wa
kula upesi, urembo, mpira, ngumi, Mieleka, kucheza mziki, au kuogelea. Mashindano
yote hayo ni kutafuta sifa ya kuvikwa
taji ya ushindi. Taji hizi zaweza kuwa katika mtindo wa medal za dhahabu au shaba au fedha, tuzo
za vyeti, mkanda pamoja na kitita cha pesa! Vyote hivyo ni taji kwa aina
zake, haijalishi kuwa ni taji itokanayo na kitita cha fedha au la!
Taji ni
utambulisho wa juu kupita yote katika ulimwengu wetu huu. Taji ni alama ya
kutambua jitihada za mtu anayepewa taji kama pongezi au stahili/stahiki kwa jambo fulani au mchango wake!
Ukipitia historia za watu kadhaa mashuhuri ulimwenguni ambao taji zao zinaheshimika
sana ulimwenguni. Mfano; Tuzo ya Nobel Prize ya Martin Luther Jr, Marcom X
inahusisha wale wote walioshinda vita vya kupinga ubaguzi wa rangi.
Mambo ya Taji
za ushindi chanzo chake ni Mbinguni. Paulo
anazungumza na kijana Timotheo kuwa
akaze mwendo katika huduma yake ya kichungaji, maana pia Wagiriki (Wayunani) ni watu ambao walikuwa na mashindano
mengi kama vile ngoma, riadha, watoahoja za nguvu (falsafa), n.k. hivyo Paulo
anapoeleza kwa Timotheo aliyaelewa mazingira ya Wakorintho vyema kuwa wataelewa
lugha hii. (2TIMOTHEO 4:7-8)
Kwa mujibu wa Paulo; Taji ni
kwa wote ambao wanapenda mafunuo ya Mungu, na wamekubali kuisikia Sauti ya
Mungu katika maagizo yake yote. Wenye
sifa ya kupokea taji ya Ushindi, Paulo anataja mambo yaliyowastahilishi
kupokea taji kuwa ni Kuhubiri Injili
(SOMA 2TIMOTHEO 4:1-6).
JE, NI WAPI WALIO NA SIFA ZA KUPATA TAJI ZA USHINDI?
1. Wanaoihubiri na kuishindania injili (WAFILIPI 4:3 “Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambayo majina yao yamo katika kitabu cha uzima”).
1. Wanaoihubiri na kuishindania injili (WAFILIPI 4:3 “Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambayo majina yao yamo katika kitabu cha uzima”).
2. Waliosonga mbele bila kukata-tama, kwa kujua majukumu,
wajibu na mamlaka waliyopewa na Kristo. (MATHAYO 28:18-20).
3. Watakao beba neno la AMANI kwa watu waliokata tamaaa na wasio na
matumaini. (SOMA ISAYA 52:7).
4. Wanaoelewa
uthamani wataji ya ushindi (SOMA 2 TIMOTHEO 4:9-18).
TOFAUTI TA TAJI YA ZA KIDUNIA NA KIMBINGU
Taji za kidunia hazina nyota; bali taji ya
mbinguni LAZIMA iwe na NYOTA. MBINGUNI
HAKUNA TAJI BILA NYOTA.
Nyota ni nini??? (Nyota
ni roho za watu:)
1. MITHALI 11:30 “Mazao ya wenye haki ni mti wa uzima; Mwenye hekima huvuta roho za wtu”
1. MITHALI 11:30 “Mazao ya wenye haki ni mti wa uzima; Mwenye hekima huvuta roho za wtu”
2.DANIELI
12:3 “Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga,
na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota mile na milele”.
3. Ellen White katika MATUKIO Uk. 257, 258, & 269 anasema hivi: “Wale 144,000 walisimama juu ya bahari ya
kioo katika mraba kamili. Baadhi yao walikuwa na taji zilizong’aa sana, wengine
hazikung’aa sana. Baadhi ya taji zilionekana nzito kwa sababu ya nyota, wakati
nyingi zilikuwa na nyota chache. Wote waliridhika kabisa na taji zao. Taji ya
uzima itakuwa angavu au iliyofifia, itametameta kwa nyota nyingi
au iangazwe na vito vichache kulingana na jinsi mambo yetu yalivyotendeka.
Mbinguni hakutakuwa na mtu yeyote aliyeokolewa mwenye taji isiyokuwa na nyota.
Ikiwa utaingia, kutakuwa na roho fulani katika makazi ya utukufu ambaye atakuwa
amepata fursa ya kuingia pale kupitia kwako.” …… “Wakati waliokombolewa
watakaposimama mbele za Mungu, roho za thamani wataitikia kwa majina yao ambao
wapo pale kwa sababu ya juhudi ya uaminifu wako, uvumilivu, nguvu
zilizowashughulikia, maombi, ushawishi uliotolewa kwao ili wakimbilie ngome.
Hivyo wale ambao katika ulimwengu huu wamekuwa wafanya kazi pamoja na Mungu
watapokea thawabu yao. 8T 196, 197. Wakati malango ya lile jiji zuri
lililoko mbinguni yatakapofunguliwa na kugeuka katika bawaba zake
zinazomeremeta, na mataifa yale ambayo yameshika kweli yataingia ndani yake,
taji za utukufu zitawekwa juu ya vichwa vyao, na wao watamtolea Mungu sifa, na
utukufu mkuu. Na katika wakati huo, baadhi watakuja kwako na watasema, ‘Kama
isingekuwa ni kwa sababu ya maneno (ya hekima ) uliyonizungumzia katika wema
wako, na kama isingekuwa kwa sababu ya machozi yako na maombi yako na juhudi
zako za uaminifu, kamwe nisingaliweza kumwona Mfalme katika uzuri wake.”
4.
Wimbo wetu wa ibada
HITIMISHO Yaweza kuwa tusiweze kuuona ufalme kwa kuwa tu
hatukupeleka mtu yeyote pale juu mbinguni, maana tutahesabika kuwa hatukuleta
wokovu wowote duniani. Yesu anakuja kumvika taji ya ushindi kila aliyeshinda
vita.
Swali ni nani atakaye nifanya niweze kupata
nyota pale? Tazama hili wote watakaoingia mbinguni kwa juhudi zangu sio wale
waliongoka kisha wakatoka – lazima ile roho iwepo pale! Kama salama yangu ni
kufanya kazi kwa juhudi na kuleta wengi kwa kadri iwezekanavyo maana sijui ni
ipi itaingia pale!
MHUBIRI 11:4-6 “4Mwenye
kuuangalia upepo hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna. 5Kama
vile vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni
mwake mjamzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote. 6Asubuhi
panda mbegu zako, Wala jioni usiuzuie mkono wako”
Comments
Post a Comment
Thanks for viewing and passing through NMEE blog. Keep following the blog