UWEZO WA KWENDA MBALI KULIKO WENGINE
Urefu na ubali awapo tai, huwezi kuona aina
nyingine ya ndege. Zaidi ya futi 10, 000 kwenda juu angani kutoka kwenye uso wa
dunia ni urefu mkubwa sana ambapo ndege wengine hawawezi kuumudu kulingana na
changamoto za misukosuko, upepo mkali, mvua, baridi kali sana, kukokasa uwezo
wa kuona chini, maana ni juu sana. Kwa hiyo maisha ya tai ni ya kusitajabisha
sana, kwani yeye huwa juu zaidi ya ndege wengine wote. Lakini hata awapo juu
zaidi hapotezi uwezo wake wa kuona mbali.
Fudisho
Tulipatalo Katika maisha yetu:
Kuna msemo unasema kuwa “ndege wenye tabia na
manyoya ya rangi ya aina moja hupaa pamoja”. Ukanda wa juu alipo tai huwezi
kukutana na ndege wengine zaidi ya tai pekee. Kwa mtu aliyemakini lazima
afanye, afikiri na atende zaidi ya pale wengine walipofikia. Kufuata mkumbo na
kuiga mienendo, tabia, jinsi ya kutenda, kufikiri na kuiga maisha ya watu
wengi, hakuwezi kukuletea tofauti yoyote zaidi ya kuishi kwa mkumbo. Jua kuwa kila mtu ni wa pekee kwa jinsi ya
ajabu alivyoumbwa. Kuepuka mkumbo na kunakili maisha na mienendo yaw engine;
yatupasa kuwa tofauti au zaidi ya wawazavyo, waishivyo, wafikiriavyo na
watendavyo. Kama tai jinzi walivyo wa pekee katika ndege wengine; na sisi tuwe
wa pekee kwa kila namna.
Kama
alivyo tai katika kuumbwa na Mungu; pia binadamu anamjumuiko wa maajabu na
vipawa na vipaji vingi ambapo Mungu kampatia kwa jinsi ya ajabu na
kustaajabisha. Binadamu yeyote akitulia vyema katika kufikiri, anaweza kufanya
mambo makubwa katika maisha yake endapo atakubali kutumia uwezo mkubwa na vipaji
alivyopewa na Mungu. Mungu kampa mwanadamu akili na uwezo mkubwa kuliko viumbe
vyote alivyoviumba. Kutojitambua kwa mwanadamu ndicho kikwazo kikubwa cha
kutokuwa na upekee.
Comments
Post a Comment
Thanks for viewing and passing through NMEE blog. Keep following the blog